Alichohoji Profesa Muhongo ni kama bei ya umeme itakuwa nafuu kuanzia siku ya kwanza au baada ya kurudisha gharama za uwekezaji?

Alichohoji Profesa Muhongo ni kama bei ya umeme itakuwa nafuu kuanzia siku ya kwanza au baada ya kurudisha gharama za uwekezaji?

Ni kweli kuna bei elekezi, lkn siyo kwa kila kitu. Kuna vitu vingne inaachiwa nguvu ya soko iamue.

Ni kwa vitu vichache ndio bei ya soko imaamua, lakini siku kwa hizo bidhaa muhimu za kijamii.
 
Kuna Uwekezaji wa mtu binafsi au kampuni ambayo nia yake ni fedha ilioyowekezwa irudi kwa muda muafaka na kupata faida. Uwekezaji wa Serikali hauhitaji kurudusha fedha iliyowekezwa au faida, lengo ni kutoa huduma kwa wananchi kwa manufaa mapana. Ni kama ujenzi wa mabarabara, madaraja, mashule, vyuo, meli na kadhalika. Mtu binafsi akiwekeza maeneo hayo anategemea kurudisha fedha zilizowekezwa lakini kwa serikali haihitaji hayo, ndio maana sekta hizo za binafsi zinalipiwa lakini za serikali ni bure au kuchangia kiasi kidogo. Hivyo basi bwawa la Nyerere hahitajiki kurejesha fedha wala faida zaidi ya kuwa na uwezo wa kupata fedha kwa ajili ya gharama za uendeshaji. Kama ni deni, tunayo madeni katika sekta nyingi ambazo huduma zake hutolewa bure na serikali.

Halafu faida ya umeme inajulikana. Faida haipo katika uuzaji wa umeme tu, lakini nje ya box (indirect) utawezesha kupungua kwa bei za bidhaa za viwanda kwani viwanda vitakuwa na gharama ndogo za uzalishaji, gharama za maji hasa mijini ni kubwa nazo zinachangiwa na gharama kubwa za umeme, bei ya umeme ikishuka obvious na gharama za maji zitashuka, tuseme maeneo mengi yanayotumia umeme gharama za bidhaa na huduma zitapungua. Kwa hiyo faida ni kubwa kuliko inavyodhaniwa.

Naishauri serikali iendelee kujenga mitambo ya umeme kila sehemu ambayo kuna uwezekano, sio lazima miradi mikubwa hata hii ya megawat moja, kumi na kadhalika. Tuhimize wananchi kulinda mazingira na vyanzo vya maji. Tusitetee wauza majenereta na wapiga dili.
 
Ukiondoa awamu ya jiwe kuwa utawala wa hovyo pia nadhani ndio awamu yenye watu incompetent wengi
 
Kwa Hiyo umejaribu kuwaza pia Kwamba kama ungekuwa mradi wa Umeme wa Gesi ungekamilika basi wenyewe Gharama za mradi zingerudi Mapema zaidi Kulinganisha na huu wa Maji???

Ukweli utabaki Ukweli tu kuwa Prof. Katika hili alikosea kidogo, maana LENGO KUU KWA WANANCHI NI KUPATA UMEME KWA BEI NAFUU NA WALA SIYO KWENDA NA WAKATI ETI UMEME WA GESI HUKU WANANCHI WANAUMIA.
Hata hivyo Nchi zilizoendelea bado zinatumia Maji kama chanzo Kikuu Cha Umeme!!!

Naweza kukubaliana Naye Prof. sehemu moja tu Kwamba Vyanzo mbalimbali vya umeme viendelee kutengenezwa ili kama Wakati wa Matengenezo kusiwe na uhaba Au upungufu wowote wa Umeme nchini
Umeme wa maji bado unatumika lakini hakuna nchi kubwa iliyoendelra inayotumia maji kama chanzonkikuu cha umeme.
 
Huo ni mradi wa muda mrefu iweje day one Bei ya umeme iwe nafuu?Kama hajasoma masuala ya biashara si anyamaze.huyu muhongo ni bomu elimu yake haina msaada kwa watz
Watu wengi wanajadili wasichokijua.

Ukweli ni kuwa hakukuwa na haja ya kuanza mradi mwingine wa umeme wakati tayari umepoteza pesa nyingi kwenye mradi mwingine wa umeme, na miundombinu yake ipo underutilized.

Tumetumia pesa nyingi kujenga bomba la gas, zaidi ya dola bilioni 1, tukitarajia bomba hilo litatumika kusafirisha gas ya kuzalishia umeme. Bomba hilo mpaka sasa linatumika kama 10% tu, halafu unaenda tena kuanza mradi mwingine wa matrillion ya pesa ambao utazalisha umeme mdogo zaidi kuliko miundombinu ya kwanza. Wewe una akili kweli? Very poor reasoning and planning.
 
kwa hiyo bwawa likianza kutumika, umeme utapanda bei kufidia hiyo investment cost?
Investment inalenga

1.,Umeme wa uhakika

2.Umeme wa kuuza nje

3.Gharama za umeme za sasa ndio basis ya kuweka ukubwa na kujua lini litakuwa limelipa

4.Uhakika wa umeme unapeleka kuwa na same rates kwa miaka mingi sana....

Swali la Prof ni la kijinga kwa umri wake na elimu yake

wewe hapa hauwezi kujibu; kamuulize prof
Inaonekana hujui chochote kuhusiana na miradi ya umeme. Umeona watu wanajadili, na wewebu ukajitumbukiza kuweka chochote kilichokujia.

Kwa kuwa hufahamu, elimika na yafuatayo:

1) Tayari tumejenga bomba la kusafirishia gas ya kuzalishia umeme kwa dola zaidi ya bilioni 1

2) Bomba la gas kwa sasa linatumika kwa 10%

3) Umeme ambao ungezalishwa kwa gas ni megawat 3,500

4) Ili kupata megawat 3,500 kilichokuwa kinahitajika ni kununua mtambo tu wa kufua umeme.

Kutokana na ujinga:

1) Tumeacha bomba lililotugharimu zaidi ya dola bilioni 1 liendelee kutumika kwa 10%

2) Tumeanda kuanza mradi mpya wa umeme kwa gharama ya zaidi dola bilioni 5

3) Tumeacha mradi wa kuzalisha megawat 3,500 ambao ungekamilika kwa uwekezaji mdogo, tumeenda kwenye gharama kubwa ya ujenzi kwaajili ya kuzalisha umeme kidogo zaidi, megawati 2,000 tena kuzifikia ni kwa awamu.

Hivi sisi tuna akili?
 
Hoja dhaifu mno kutoka kwa Prof! Kwani kuna mradi gani ambao ukikamilika hatutowajibika kulipa gharama?

Nilitegemea maprof kama hawa ndio wangekuwa watetezi wa kuwekeza kwaajili ya vizazi vijavyo! Hawa wazee wameshikwa na ma lobbyists walambe 10% zao na vizazi vyao na si Watanzania kwa ujumla.
Hivi huu mradi sio pesa zetu za ndani tuna jengea!?
 
Alisema mtu mmoja '' Afrika anayeongea sana bila takwimu ndio anaonekana anajua zaidi''
 
Leo baadhi ya wabunge wamemshukia Profesa Muhongo na kudai ni heri darasa la saba Msukuma na Kibajaji kuliko PhD holder.

Naye Spika Ndugai akasema ni vema maprofesa wakawa wanajipanga vizuri kabla ya kuongea kuepukuka changamoto za akina Kibajaji kwani uprofesa ni muhimu kwenye kufundisha na utafiti lakini siyo siasani hasa Bungeni.

Imenibidi nifuatilie kujua huyu Muhongo anayeshambuliwa ameongea nini?

Kumbe Muhongo hajasema umeme wa maji mbaya bali inachukua muda mrefu sana kurejesha gharama ndio akahoji labda kama bei nafuu itaanza kutumika day one bila kujali pay back period.

Mantiki yake ni kuwa bei inaweza kuwa kubwa hadi mradi utaporudisha gharama zake, ambayo huwa ni miaka mingi mbele

CCM mko peke yenu bungeni hakuna wa kumsingizia.
we mwehu kuanzia lini serikali ikafanya biashara...kwani wewe umeme ukishuka gharama kwa miaka hata 50 ela kurudi utakufa..mwehu sana hizo gharama zinazorudi zaidi ndo zinasabbabisha umeme kuuzwa ghali..sijui mnawaza kutumia makalio
 
Wanaweza kuvizia hotuba au press conference ya Mbowe mitandaoni na kuijibu bila tashwishwi. [emoji1787]
 
we mwehu kuanzia lini serikali ikafanya biashara...kwani wewe umeme ukishuka gharama kwa miaka hata 50 ela kurudi utakufa..mwehu sana hizo gharama zinazorudi zaidi ndo zinasabbabisha umeme kuuzwa ghali..sijui mnawaza kutumia makalio
Wewe unatumia katikati ya makalio kuwaza!
 
Hoja dhaifu mno kutoka kwa Prof! Kwani kuna mradi gani ambao ukikamilika hatutowajibika kulipa gharama?

Nilitegemea maprof kama hawa ndio wangekuwa watetezi wa kuwekeza kwaajili ya vizazi vijavyo! Hawa wazee wameshikwa na ma lobbyists walambe 10% zao na vizazi vyao na si Watanzania kwa ujumla.
Kwani wewe Taga nani alikuzuia kusoma na kuwekeza kwa ajili ya vizazi vijavyo?
 
Kibajaji nae anajilinganisha na Muhongo,
Kweli hii ni hatari sana. Sijawahi ona, ukiangalia hata anachoongea ni porojo tu. Hakina hata research yoyote, hakina data, yaani ni vitu vya kufikirika tu.
Mtu ambaye alitakiwa aongee kwa data ni Prof. Muhongo. Kwa level yake hakutakiwa kuongea bila data. Kibajaji ata akiongea porojo anavumilika lakini sio mtu mwenye uprofesa!
 
Hawa maprof wamejitakia haya madhila kwa kuacha taaluma zao na kukimbilia siasa acha wachezee vitasa kwanza vya mangumbaru adi akili ziwakae sawasawa
Angetoa hoja hiyo mbele ya wasomi wenzake wangebisha kwa hoja tuu. Na sio kashfa hizo
 
Inaonekana hujui chochote kuhusiana na miradi ya umeme. Umeona watu wanajadili, na wewebu ukajitumbukiza kuweka chochote kilichokujia.

Kwa kuwa hufahamu, elimika na yafuatayo:

1) Tayari tumejenga bomba la kusafirishia gas ya kuzalishia umeme kwa dola zaidi ya bilioni 1

2) Bomba la gas kwa sasa linatumika kwa 10%

3) Umeme ambao ungezalishwa kwa gas ni megawat 3,500

4) Ili kupata megawat 3,500 kilichokuwa kinahitajika ni kununua mtambo tu wa kufua umeme.

Kutokana na ujinga:

1) Tumeacha bomba lililotugharimu zaidi ya dola bilioni 1 liendelee kutumika kwa 10%

2) Tumeanda kuanza mradi mpya wa umeme kwa gharama ya zaidi dola bilioni 5

3) Tumeacha mradi wa kuzalisha megawat 3,500 ambao ungekamilika kwa uwekezaji mdogo, tumeenda kwenye gharama kubwa ya ujenzi kwaajili ya kuzalisha umeme kidogo zaidi, megawati 2,000 tena kuzifikia ni kwa awamu.

Hivi sisi tuna akili?
Utakuwa uchambuzi umefanyika. Nionavyo mimi Ile gesi kule inanunuliwa kutoka kwa wachimbaji wenye vitalu/visima vya gesi sio bure. Hata usafirishaji unalipiwa. Soko kubwa lla gesi ni kuuza nje ya nchi kwa bahati nzuri Kenya watainunua na serikali itapata fedha kwenye kodi/mrahaba. Na hili la kujenga bomba kwenda Mombasa mtabeza? Na wenzetu Wakenya ni wajanja na wana mbinu za kibiashara, mnaweza kuwapelekea hiyo gesi na wao wakaiuza nje. Hata hivyo Vinyerezi vitaendelea kujengwa.
 
Back
Top Bottom