Alichohoji Profesa Muhongo ni kama bei ya umeme itakuwa nafuu kuanzia siku ya kwanza au baada ya kurudisha gharama za uwekezaji?

Kazi kweli kweli mtazamo wako ni sawa na wa Kibajaji!

Ahaa haa
Labda kama unataka siasa, Sensitivities hazijawaji sema bei itabadirika if capital imekuwa recouped. Bali inaangalia ups and downs of demand. Anyways, ngoja niishie hapa.
 

Migambo wanaruka na kukanyagana. Majizi ya kura yako yenyewe yanazinguana tu huko kwenye bunge kibogoyo.
 
Nimshukuru Mungu kwa kutenda miujiza ya kukugeuza wewe kutoka kwenye kuunga mkono hadi sasa unaongea kama mwananchi wa kawaida mwenye akili timamu.

Mpaka muda huu siamini kama ACCOUNT yake huyu jamaa johnthebaptist haija dukuliwa.
 
anayepanga bei ni Serikali sitarajii aweke bei kubwa kwani alishafanya analysis ya mradi.

Labda wajinga ndio unaweza kuwaambia hili, kama bei ya mafuta ya kula na sukari tu imewashinda kushusha, ndio itakuwa hiyo ya umeme wa 10t ya mkopo?
 
Labda wajinga ndio unaweza kuwaambia hili, kama bei ya mafuta ya kula na sukari tu imewashinda kushusha, ndio itakuwa hiyo ya umeme wa 10t ya mkopo?
bei ya sukari ulitaka ishuke hadi sh ngapi?
 

Kama kwenye mafuta ya kula na sukari bei imeshindikana kuwa nafuu na hakuna mkopo, ndio itakuwa kwenye umeme ambapo 10t zinakopwa? Wajinga ndio waliwao. Huu utapeli pia umetumika sana kwenye manunuzi ya ndege kuwa ni zetu, leo nenda angalia nauli za ndege za ATCL, linganisha na ilivyokuwa fastjet kisha ulete mrejesho.
 
Nimshukuru Mungu kwa kutenda miujiza ya kukugeuza wewe kutoka kwenye kuunga mkono hadi sasa unaongea kama mwananchi wa kawaida mwenye akili timamu.
Upepo tu habadiliki huyo
 
"The Power of hunger" mpaka prof anatumika kwa kujitoa ufahamu. Ni mkumbushe aliyo sema Mh DR(ad honorem) Lusinde kuhusu faida zitokanazo na Bwawa la Umeme la Mwl Nyerere.

Hoteli za kitalii zitajengwa kwenye fukwe za Bwawa. Utalii Selous utashindana na Kaskazini
Kilimo cha umwagiliaji
Samaki Sato wa kumwaga
Umeme nafuu, Richmond, Aggreco, ITPL na nduguze watasubiria sana kwenye foleni kusubiri zamu zao tena.
Mamba na Viboko watajidai zaidi ni endelee prof teni teni na nduguze?
 
bei ya sukari ulitaka ishuke hadi sh ngapi?

Ilikuwa shilingi ngapi kabla ya serikali kuingilia mambo ya sukari? Na hivi majuzi kabla serikali kujiingiza kwenye mafuta bei ilikuwa kiasi gani,na sasa ni kiasi gani?

Halafu wakati tulipokuwa tukitumia umeme wa maji, mbona bado umeme wa maji haukuwa rahisi? Katika nchi za Afrika mashariki sisi hatukuwa na umeme wa bei rahisi. Kwahiyo Mkitaka kudanganya watu, inabidi muwe na kumbukumbu ya ukweli huo.
 
Hii promo ya umeme wa maji sasa, ilipigwa na chama hicho hicho miaka 6 nyuma kwenye umeme wa gas. Sisi wengine tunajua hilo genge liitwalo ccm ni kundi hatari la matapeli, wanaopigania 10% zao.
 
Wasomi wetu wajifunze.wanaacha kutusaidia kwenye kufundisha na kufanya tafiti wao wanaenda kwenye siasa.sasa wewe imagine,Prof anaanza kubishiwa na akina kibajaji kweli.yaani amepoteza muda wake kuacumulate knowledge halafu anakuja kufedheheshwa hivi. Nakumbuka zamani alikuwaga na gia ya kuleta matokeo ya sekondari ya mbunge anayembishia,sasa hapa kibajaji hata hiyo shule hakwenda kabisa
 
Kwa jinsi itakavyokuwa hoja ya msingi hapa je umeme wa maji ni rahisi au siyo rahisi?
 
Kuna wanasiasa naona wanatumika kuwa kama mashionari..

Hiyo Phd ya Muhongo Mimi sina lakini nina mashaka nayo kwakweli..

Ipo hivi gharama za mwanzo za ujenzi wa mradi umeme wa maji siku zote Huwa juu kutokana na kuchukua eneo kubwa tofauti na mradi wa umeme wa gesi(Yani kwenye ujenzi)..

Lakini tukija kwenye gharama za uendeshaji zinakuwa ni kama sifuri Yani kwenye hesabu Huwa tunasema (the value can be neglected kutokana na faida kuwa kubwa kuliko gharama za uendeshaji) hapa ndipo tunapo pata faida yake, tukumbuke mvua hailipiwi ni bure kabisa na vilevile umeme wa maji ni moja ya vyanzo umeme ambavyo havichafui mazingira kwa kuongeza gesi ya ukaa(Carbondioxide) vilevile hudumu miaka mingi mfano tuangalie bwawa la mtera..

Sasa tukija kwenye umeme wa gesi.. bila hata kuambiwa wote tunajua gharama ya gesi ilivyo juu ukiona gesi unaungua ujue ni pesa tunaunguza.. na hapo tukumbuke kwenye mradi wa gesi tulishapigwa nchi yetu haita faida pakubwa kwenye uuzwaji wa hiyo gesi kuzalisha umeme..

Sasa hapo tujiulize hao wanaopinga huu mradi wapo kwa maslahi ya nani..??

Mi nadhani wataanzania pamoja na Hayati kuwa na mapungufu yake.. alitufungua akili lakini pia kila maamuzi aliyofanya yalikiwa ni kwaajili ya hii nchi yetu tuwe makini sana.
 
Ndugai and meko are the part of the problem,meko is very dead n gone,ndugai can not be the part of the solution,he is suffering from that disease of acquired stupidity...
 
Hii promo ya umeme wa maji sasa, ilipigwa na chama hicho hicho miaka 6 nyuma kwenye umeme wa gas. Sisi wengine tunajua hilo genge liitwalo ccm ni kundi hatari la matapeli, wanaopigania 10% zao.

Gas wa weke kwenye mitungi wakauze nje ya nchi serikali ipate kodi ya Dollari.
 
Yes maana anakuwa dalali wa wauza gas turbine na engine. Madalali kama hawa wa viwanja wanapandisha bei kwa kusingizia mkubwa fulani anakaa hapa....
 
Ndugai and meko are the part of the problem,meko is very dead n gone,ndugai can not be the part of the solution,he is suffering from that disease of acquired stupidity...
JPM hakuwa mtu wa kauli mbili mbili. He was putting his offer straight...take or leave it. Huyu Spika hasomeki. Haeleweki. Haaminiki. Ukiwa kigeugeu utaaminikaje?
 
JPM hakuwa mtu wa kauli mbili mbili. He was putting his offer straight...take or leave it. Huyu Spika hasomeki. Haeleweki. Haaminiki. Ukiwa kigeugeu utaaminikaje?

Aaah wap..!!I am not taking it,yule ndimi mbili kweli kweli,Mara ooh Maendeleo hayana vyama,na hapo hapo anasema kwamba mkichagua upinzan sitaleta Maendeleo hapa,au ananunua wabunge upinzan na kuwaleta ccm kisha anapeleka Maendeleo huko alikowatoa,Hana maana yule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…