Alichokifanya Gerson Msigwa, New York alipaswa akifanye Siku Zote Ikulu. Zuhura Yunus Asiwe Bubu!

Wanabodi,
leo nilikuwa naangalia TBC Ardhio.
  1. Nikashuhudia Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akirudia kazi yake ya zamani ya utangazaji wa TV Reporting akiripotia TBC live mubashara moja kwa moja kutokea jijini New York, nchini Marekani kutuarifu maandalizi ya uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour, utakaofanyika usiku huu mida ya Saa 1:30 Kwa saa za Marekani ambapo ni saa 8:30 za usiku wa manane kwa saa za Tanzania.
  2. Msigwa ambaye sasa ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali, amejikumbusha enzi zake za utangazaji, kwa kumhoji Msemaji Mkuu wa Serikali mstaafu Dr. Hassan Abasi ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo na Utamaduni na ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya filamu ya Royal Tour,
  3. Dr. Hassan Abbas amesema uzinduzi utahudhuriwa na wageni mashuhuri 400 akiwemo Mayor wa Jiji la New York.
  4. Kitendo cha Msemaji Mkuu wa Serikali kumhoji Msemaji Mkuu wa Serikali mstaafu ni mahojiano ya kupendeza Sana.
  5. Kiukweli kipaji cha TV Reporting na composeture yake, hiki ni moja ya vipaji vikubwa sana ambavyo TBC ilivipotezea serikalini. Ndani ya TBC anayemkaribia Msigwa ni Khalid Gangana.
  6. Hongera Sana Gerson Msigwa kurudia kazi yako ya utangazaji!. Hiki ulichokifanya leo jijini New York, nchini Marekani, ndicho ulipaswa ukifanye Ikulu yetu, siku zote ilipokuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu.
  7. Kazi ya Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, sio tuu ni kuandika Press Release, bali pia kuiripoti direct from Ikulu kwa piece to camera kama ulivyo fanya leo.
  8. Ulipaswa kuturipotia shughuli muhimu za rais ikitokea Ikulu, na kuiripoti moja kwa moja into the news.
  9. Pia ulipaswa kuitisha Press Conference na kufanya Press Briefing kwetu sisi waandishi kama walivyofanya Balozi Choks, Balozi Nkurlu na Balozi Kalaghe, na kama wafanyavyo ma Press Sec wa wenzetu Duniani.
  10. Naamini Zuhura Yunus hata kuwa Bubu, ikitokea rais ana shughuli muhimu, asiishie kutusambazia just a press release bali sasa sambazeni multi media release yenye press release, photo gallery, audio footage, TV footage, social media footage na Peace to Camera.
All and all, hongereni sana for all that you are doing, Leo sisi huku Bongo ni hakuna kulala mpaka hiyo saa 8:30 usiku wa manane.
Tunawasubiria tushuhudie.
Paskali.
Mabandiko mengine kuhusu Royal Tour
Pascal Mayalla hongera kwa kuwaongezea nondo dada Zuhura Yunus (ingawa naye yupo biased sana).
 
Leo ni hakuna kulala, 2 hours to go!. Haya mambo ya kutembeza na Joni Mtembezi, two hours from now... sijui!. Ikitokea hamjaona update yangu, mjue mwenzenu nimezimika!.
P
Saa hizi ni dakika chache kabla ya uzinduzi, TBC sioni dalili ya kutuletea live!.

Kwa bahati mbaya vijana wengi na watu wa mjini hawaangalii TBC baada ya kugeuka tarumbeta la ccm. Kwa hiyo siyo habari itakayovutia wengi. Sana sana muilete huku huku kwenye social media wangalau watu wajue kilichoko kwenye hiyo Royal tour.
 
Kiukweli kipaji cha TV Reporting na composeture yake, hiki ni moja ya vipaji vikubwa sana ambavyo TBC ilivipotezea serikalini
basi kwa kweli hicho kipaji cha composeture kitakuwa kipaji adimu na adhimu

inabidi huyo Halidi Gangana aliyebaki nae wampeleke nje akasomee weledi wa composeture kama ataweza kumudu masomo ya composeture
 
Tofauti walito nayo kubwa hao na Zuhura Yunus ni moja tuu, kuzungumza ukweli.
Msigwa na Dr Hassan walizoea kuishi kwa uongo, kusema kwa uongo, propaganda hata pasipostahili na sifa za kupitiliza tofauti na Zuhura anaye simamia weledi wa taaluma.
Ona eti Dr Hassan anasema uzinduzi huu unaangaliwa na watu Billioni 1 duniani kote! Uongo bila aibu!
 
Wanabodi,
leo nilikuwa naangalia TBC Ardhio.

  1. Nikashuhudia Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akirudia kazi yake ya zamani ya utangazaji wa TV Reporting akiripotia TBC live mubashara moja kwa moja kutokea jijini New York, nchini Marekani kutuarifu maandalizi ya uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour, utakaofanyika usiku huu mida ya Saa 1:30 Kwa saa za Marekani ambapo ni saa 8:30 za usiku wa manane kwa saa za Tanzania.
  2. Msigwa ambaye sasa ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali, amejikumbusha enzi zake za utangazaji, kwa kumhoji Msemaji Mkuu wa Serikali mstaafu Dr. Hassan Abasi ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo na Utamaduni na ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya filamu ya Royal Tour,
  3. Dr. Hassan Abbas amesema uzinduzi utahudhuriwa na wageni mashuhuri 400 akiwemo Mayor wa Jiji la New York.
  4. Kitendo cha Msemaji Mkuu wa Serikali kumhoji Msemaji Mkuu wa Serikali mstaafu ni mahojiano ya kupendeza Sana.
  5. Kiukweli kipaji cha TV Reporting na composeture yake, hiki ni moja ya vipaji vikubwa sana ambavyo TBC ilivipotezea serikalini. Ndani ya TBC anayemkaribia Msigwa ni Khalid Gangana.
  6. Hongera Sana Gerson Msigwa kurudia kazi yako ya utangazaji!. Hiki ulichokifanya leo jijini New York, nchini Marekani, ndicho ulipaswa ukifanye Ikulu yetu, siku zote ilipokuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu.
  7. Kazi ya Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, sio tuu ni kuandika Press Release, bali pia kuiripoti direct from Ikulu kwa piece to camera kama ulivyo fanya leo.
  8. Ulipaswa kuturipotia shughuli muhimu za rais ikitokea Ikulu, na kuiripoti moja kwa moja into the news.
  9. Pia ulipaswa kuitisha Press Conference na kufanya Press Briefing kwetu sisi waandishi kama walivyofanya Balozi Choks, Balozi Nkurlu na Balozi Kalaghe, na kama wafanyavyo ma Press Sec wa wenzetu Duniani.
  10. Naamini Zuhura Yunus hata kuwa Bubu, ikitokea rais ana shughuli muhimu, asiishie kutusambazia just a press release bali sasa sambazeni multi media release yenye press release, photo gallery, audio footage, TV footage, social media footage na Peace to Camera.
All and all, hongereni sana for all that you are doing, Leo sisi huku Bongo ni hakuna kulala mpaka hiyo saa 8:30 usiku wa manane.
Tunawasubiria tushuhudie.
Paskali.
Mabandiko mengine kuhusu Royal Tour

Kiswahili Cha neno kustaafu kinachezewa sana hivi ukiteuliwa cheo Fulani baadaye akapewa mwingine wewe wa awali unakuwa umestaafu?
 
Paskali, professional na siasa haviendani, yaani hata msigwa ni bahati tu kufanya hivyo akiwa hapo America ila akiwa hapa ikulu ni ngumu sana.

Kwa dadaenu zuhura pia ni vigumu kufanya hicho unachotaka, bahati mbaya upo nje ya field ila ukibahatika kuingia and in one week tu ahahahaa, sijui kama utaandika uliyokutana nayo huko.

Kila ofisi ina utaratibu wake ila hatuhufahamu kwa sababu tupo kwa nje.
 
Back
Top Bottom