Majina yote weka hapa. Ukweli uko pale pale. Hakuna mtu anataka kutokuwa mwoga kwa au mnafiki kwa kuleta fujo ambazo hazina tija. Twende mbele na turudi, si njia njema.
Tujadili hoja.
Wote (au wengi) tumesikia alichosema.
Ameomba kura zisitishwe kutangazwa.
Mimi ningeongeza kuwa, matokeo yajumlishwe upya kwa kutumia namba za mwanzo zilizopatikana katika kila kituo na kusainiwa na mawakala wa vyama vyote.
Kama kweli ccm mmeshinda, kwa nini msikubali kura zijumlishwe upya (sio kuhesabiwa upya)?
hoja ipi hiyo? ya wewe kujiita kuwa ni mwanachadema wakati unajua kabisa ukweli sio huo?
Acha crap zako bana, ukileta bange hapa, utazipata tu maana haya nyani haangaliwi usoni.
Unafiki wako peleka huko huko Lumumba walikokutuma.
Mwafrika, kila mwenye macho na masikio, ameyaona na kuyasikia madudu ya NEC kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kwa kifupi maroroso ni mengi tuu, lakini kwa vile Dr. Alisaini kuzikubali zile rules of the game, kama ana malalamiko yoyote, angeanzia kuyapeleka kwa refa (NEC) ndipo akaja na vyombo vya habari na hatimaye ayakabidhi kwa umma.
NEC inajua inachokifanya,( kuna posti niliposti kule nyuma kuhusu matokeo ya mwisho, nilitukanwa sana, nikashauri tusubiri nami bado nasubiri) na itaendelea na inachokifanya, Kesho saa 11 jioni, watatangaza matokeo ya mwisho na baada ya hapo hakuna hata mahakama yenye uwezo wa kufanya chochote. Jumamosi Saa 4:00 Uwanja wa Taifa, JK ataapishwa, kitakachofuata ni kusubiri 2015!.
Kila mpenda demokrasia wa kweli, lazima anaumizwa na kinachoendelea, naamini hata wana CCM wa ukweli, hawaipendi hali hii ya kupewa ushindi wa mezani, lakini Dr, anapaswa kuyapeleka malalamiko yake kunakohusika kwanza, ndipo na aumwage mtama kwenye kuku wengi.
Kwenye kulijadili hili, naombeni ushabiki tuuweke pembeni, tutangulize maslahi ya taifa.
Nimewapata wote hapo nitawajibu kwa pamoja.
Labda kama mtaniona sijui kama mmoja wenu alivyosema au ni namna ya kudai haki, vyovyote vile. Lakini, haikuwa busara hata kidogo kwa mtu wa kiwango chake kuongea kitu alichooongea. Hata kama unagombea roho yako isitoke, huwezi lazimisha roho za wengine pia zitoke!. Ni kiwango cha chini kabisa cha busara kwa mtu kama Dr. Slaa kuongea namna ile. Mnaonipinga hapo juu, je mmeweza elewa kwanini Slaa hajaongelea kuhusu Ubunge wakati kwenye Ubunge ndiyo kuna malalamiko zaidi kuliko Urais? NImemsikia BBC jioni akisisitizia matokeo ya Urais tu, kwanini isiwe Ubunge na Udiwani? Sikutarajia, hamna mtu alitarajia. Nilichodhani mimi, angetuambia sisi wafuasi, tusubiri matokeo kwanza na baada ya hapo twende mahakamani.
Hapa ndipo tumefika watu wanasema TOGETHER we stand, Divided it is time to GO.
Hivi kisheria wakipokea malalmiko mahakama wanweza kusitisha zoezi linaloendelea kabla ya wahuni kujitangaziwa usshindi wa kutengenezwa?. Kama hilo lipo naona lichangamkiwe ili walau tuwe tumejaribu na NEC ionekane kughairi amri ya mahakama!
Just trying.
Mwafrika, kila mwenye macho na masikio, ameyaona na kuyasikia madudu ya NEC kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kwa kifupi maroroso ni mengi tuu, lakini kwa vile Dr. Alisaini kuzikubali zile rules of the game, kama ana malalamiko yoyote, angeanzia kuyapeleka kwa refa (NEC) ndipo akaja na vyombo vya habari na hatimaye ayakabidhi kwa umma.
NEC inajua inachokifanya,( kuna posti niliposti kule nyuma kuhusu matokeo ya mwisho, nilitukanwa sana, nikashauri tusubiri nami bado nasubiri) na itaendelea na inachokifanya, Kesho saa 11 jioni, watatangaza matokeo ya mwisho na baada ya hapo hakuna hata mahakama yenye uwezo wa kufanya chochote. Jumamosi Saa 4:00 Uwanja wa Taifa, JK ataapishwa, kitakachofuata ni kusubiri 2015!.
Kila mpenda demokrasia wa kweli, lazima anaumizwa na kinachoendelea, naamini hata wana CCM wa ukweli, hawaipendi hali hii ya kupewa ushindi wa mezani, lakini Dr, anapaswa kuyapeleka malalamiko yake kunakohusika kwanza, ndipo na aumwage mtama kwenye kuku wengi.
Kwenye kulijadili hili, naombeni ushabiki tuuweke pembeni, tutangulize maslahi ya taifa.
mkunduuu..................................nimefuatilia kwa makini sana uchaguzi wa mwaka huu. Nimevutiwa sana kwa jinsi shamra shamra na msisimko mkubwa sana. Hakika tanzania tumekomaa kisiasa na tunaelekea kwema.
Tatizo langu linakuja pale mmoja wa wagombea, hapa namaanisha dr. Slaa kuanza kwa maksudi kabisa kutaka kuanzisha fujo zisizo na maana. Kwa jinsi alivyozipanga points zake kwa kusema kura za urais zisimamishwe na si kura za ubunge nadhani kila mmoja anafahamu kuwa alikuwa anakwepa kuudhi washirika wake walioshinda ubunge. Kwa maana hii tunatambua kuwa janja yake kubwa ni kutaka serikali ya kitaifa iundwe. Mimi nakubaliana na hiyo point, ila approach aliyotumia kwa kweli inanipa wasi wasi kama kweli ana busara na ni mtu aliyekomaa kisiasa.
Kama kiongozi mkubwa si busara kuanza kuchochea ghasia. Hicho kitendo kimenikera sana na sikutarajia kwa kiongozi niliyempa points nyingi sana kabla.
Tusimame kama watanzania. Kama kuna shida na matokeo, tusubiri kwanza then twende mahakamani.
Mag3, Sophist, fishyfish wote mna haki ya kusema, aidha niwe coward, mwoga au vyovyote vile mtavyoita, hata siku moja kushindwa na kudai haki violently is never is solution. Ninachokifahamu ni kukaribisha De campo na wenzake na kuishia kutoaminiana baada ya kiongozi wetu kupelekwa pale. Kuna namna tele za kudai haki, na si kuhamasisha watu waingie mitaani. Hata hivyo, ninavyojua kwa nchi hii hakuna mtu atakuwa tayari kuwa chambo. Tuna muda na kama tumeweza kuchukua viti 51 kama wapizani, kwanini tusiweze kuchukua nchi muda ukifika?!
kwa hiyo nyie ndugu niliowataja hapo juu, mawazo ni mazuri kwa kuandika hapa hapa ili kuyajadili na si mazuri kivitendo mtaani. Bahati nzuri hayo mnayoyasema na kuchochea hamjawahi yapata ila kwa kuona kwenye TV. Ni mbaya sana.