Mwafrika, kila mwenye macho na masikio, ameyaona na kuyasikia madudu ya NEC kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kwa kifupi maroroso ni mengi tuu, lakini kwa vile Dr. Alisaini kuzikubali zile rules of the game, kama ana malalamiko yoyote, angeanzia kuyapeleka kwa refa (NEC) ndipo akaja na vyombo vya habari na hatimaye ayakabidhi kwa umma.
NEC inajua inachokifanya,( kuna posti niliposti kule nyuma kuhusu matokeo ya mwisho, nilitukanwa sana, nikashauri tusubiri nami bado nasubiri) na itaendelea na inachokifanya, Kesho saa 11 jioni, watatangaza matokeo ya mwisho na baada ya hapo hakuna hata mahakama yenye uwezo wa kufanya chochote. Jumamosi Saa 4:00 Uwanja wa Taifa, JK ataapishwa, kitakachofuata ni kusubiri 2015!.
Kila mpenda demokrasia wa kweli, lazima anaumizwa na kinachoendelea, naamini hata wana CCM wa ukweli, hawaipendi hali hii ya kupewa ushindi wa mezani, lakini Dr, anapaswa kuyapeleka malalamiko yake kunakohusika kwanza, ndipo na aumwage mtama kwenye kuku wengi.
Kwenye kulijadili hili, naombeni ushabiki tuuweke pembeni, tutangulize maslahi ya taifa.