Alichokisema Ismail Jussa baada ya Tume kutoa Rasimu ya Katiba...


Jee serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya kumaliza kutema asali na kubugia pilipili yatajiri yapi mbona unakuwa mbaguzi wa fikra? Ya mtwara hayahusiani na dini, haya ya ukanda na ukabila ni mada mpya, tumalize la udini halafu nitakujibu.

 
Madai ya Waislam ktk katiba ya Tanganyika-
Mahakama Qadhi
Ijumaa iwe Mapumziko
Madaraka sawa kati ta Wakiristo na Waislam
Rais wa Tanganyika iwe kwa zam kati ya wakiristo na waislam.
Katiba itambuwe kuwepo kwa Mungu.
.......
.....,,,,


Ahsante sana ami yangu Boribo kwa kuainisha hayo. Lakin kubwa zaidi la kuongeza hapo ni lile la MoU ya kanisa na Serikali ya JMTz na suala la Gas kule Mtwara.

Nafikiri ingekuwa busara kwao kwa sasa kuanza kufikiria changamoto hizo kwanza katika uanzishwaji wa Taifa lao badala ya kukesha kutwa kucha kufikiri Serikali ya SMZ.

Cc: Nguruvi3, Mag3, yericho Nyerere, Mkirua, Mwakanakijiji, Nicholas
 
Jee serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya kumaliza kutema asali na kubugia pilipili yatajiri yapi mbona unakuwa mbaguzi wa fikra? Ya mtwara hayahusiani na dini, haya ya ukanda na ukabila ni mada mpya, tumalize la udini halafu nitakujibu.


madai ya waislam huko Tanganyika ni haya.
By Boribo
Madai ya Waislam ktk katiba ya Tanganyika-
Mahakama Qadhi
Ijumaa iwe Mapumziko
Madaraka sawa kati ta Wakiristo na Waislam
Rais wa Tanganyika iwe kwa zam kati ya wakiristo na waislam.
Katiba itambuwe kuwepo kwa Mungu.

Na zaidi kuachwa wawe huru katika kuunda umoja wao na sio BAKWATA. Sijazungumzia Mou Ya kanisa na Serikali ya JMTz.

Je mmejipanga vipi na changamoto hizi.

Haya ndio kwa sasa mlitakiwa kukaa na kufikiri na sio kuifikiria Znz kwani waswahili wanasema Ondoa boriti katika jicho lako kabla kulitazama la mwenzako.
Pole sana
 
Swali zuri tumejipanga vipi....Kwakuwa tuna akili timamu, na kwakuwa tunajuwa kuwa Katiba ya JMT ndiyo sheria mama, Tutatumia kifungu cha 31 cha rasimu kwani ikishapitishwa itakuwa ni katiba ya JMT

Mawazo mgando kama ya hawa kina Boribo wala hayawezi kutukosesha usingizi kwani hao hao pamoja na wewe mnadai hamuitaki BAKWATA kisa "imeanzishwa na serikali
" lakini mnataka mahakama ya kadhi tena inayoanzishwa naserikali hiyo hiyo!! sijuwi mnatumia nini kufikiri anyway!! mnapaswa kusikitikia. Na kama hujakiona hicho kifungu cha 31 soma hapa chini upate kuelimika.

Uhuru wa
imani ya dini

31.-(1) Kila mtu anao uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi
katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini,
imani yake au kutokuwa na imani na dini.
(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa
ni huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ili mradi asivunje sheria za nchi.
(3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya
shughuli za mamlaka ya Serikali.
(4) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini ya
taratibu zilizowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya
kidemokrasia kwa ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii na
wa kitaifa na vitasimamiwa kwa utaratibu ulioainishwa kwenye sheria za
nchi.
(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru
wa kutangaza dini kwa kukashifu imani na dini nyingine, kujenga chuki au
kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini.
(6) Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyote
itakayowagawa wananchi, kuleta uhasama au kuharibu amani miongoni
mwa wananchi.
(7) Neno "dini" kama lilivyotumika katika Ibara hii litatafsiriwa
kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno
mengine yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa
kwa maana hiyo.


Hakuna anayeifikiria zanzibar kama unavyojidanganya bali kiukweli tunawasikitikia kwa kutema asali na kumeza pilipili. Kwamba waswalili wanasema toa boriti nikusaidie tu sio waswahili bali hayo ni maneno ya Bwana Wetu Yesu Kristo Mwana wa Mungu hivyo koma kuyaita maneno ya waswahili.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja nikusaidie kuwapelekea Notifications waje wakusulubu maana ulivyowacopy wanaweza wasijuwe kuna hoja nyepesi huku ukabaki unajisifu wamekukimbia... Nguruvi3, Mag3, Yericko Nyerere, Mkirua, Mzee Mwanakijiji, Nicholas
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli uyasemayo mimi huwa nashangaa badala kujadili kuhusu tanganyika na ujio wake wengi wao wanaisema vibaya z'bar hivi z'bar ina kitu gani mpaka kuwakosesha usingizi
 
Kwani Muungano na particularly uwepo wa visiwa vya unguja na pemba una impact gani kwa sasa kwenye kupunguza hayo matatizo? Huoni kuwa ni kuongeza tatizo (UAMSHO, UPEMBA, UUNGUJA, HIZBU NK,NK,)Na sasa concentration itakuwa sehemu moja?? Ni kuvuja kwa pakacha....
 
Jidanganye!
 

Wakiuvunja kinakuuma nini wewe? kama hawautaki utawalazimisha? hivi mbona mnapenda chokochoko ninyi?
 
Sasa suala la elimu watasoma kwao sasa! Huo ndo utamu! Sijui wana vyuo gani huko kwao! Na serikali yao itagaramia wa zanzibar kwenye elimu!

mkuu mbona vyuo zanzibar vipo vya kutosha!
 
Ukiona mtu haijui nchi ya Tanganyika,ni kosa lake kutojuwa jiografia,ikiwa akasoma ni lazima ajuwe kuna nchi Ya Tanganyika na wa Tanganyika ni wakazi wake.
 
Ubaguzi huo,si ndio huo mnaoleta nyinyi kwa wa Tanganyika,hamuwataki Zanzibar.
 
wangekuwa wanajiweza wasingejazana Tanganyika.
 
Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika, full stop. Historia yake ni kama ya kisiwa cha Gore huko senegal, mbona hadi sasa ni sehemu ya Senegal???
 
NI UTATA TU NAPENDA KUULIZA
Hivi Wazanzibari waliopata ajira kwenye mambo yaliyokuwa ya muungano awali watapoteza nafasi hizo kama mambo hayo si ya muungano tena? maana watanganyika tulikuwa hatupati ajira kule zanzibar.
 
Zanzibar ikijitenga itaendelea kuinyima usingizi Tanganyika kwa kutumia Udini, wataivuruga tuuu. majuto mjukuu
 
Wakiuvunja kinakuuma nini wewe? kama hawautaki utawalazimisha? hivi mbona mnapenda chokochoko ninyi?

Umeelewa nilichokisema au uelewa wako uko kwanye hiyo sentensi pekee? na kama chokochoko kama unavoziita, waulize wazanzibar wanaotaka madaraka kamili. nilichokieleza ni kwa nini kuwepo mwanya mwingine wa kuunda tume hapo baadaye kwa yale saba yaliyobaki?

Wamepata hayo 15 (kama rasimu itapitishwa) lakini kuna dalili za wazi kwamba wataendelea kudai yaliyobaki. wakishaonja hawataacha kuonja. hiyondiyo ilikuwa hoja yangu.
 
Mie naona Zanzibar ijiondoe kabisa kila mtu ajitegemee. Muungano wa nini?
 
20. ibara 113 out clause kuhusu uwepo wa muungano utaamuliwa kwa kura ya maoni
Hii ibara inaashiria kulikuwa na opt in clause ambayo ilitokana na kura ya maoni, kama hili halikufanyika waheshimiwa TUME si mufanye hilo kwanza? Ama mtueleze hili lilifanyika lini kwa upande wa wananchi either de facto ama de juro
Ninavyoelewa mimi hili la kura maoni kuulizwa wananchi kama wanautuaka huu muungano hawajaulizwa hapo mwanzo na wala hivi sasa, hivyo kuwepo ibara hii ni udanganyifu wa kisheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…