Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ubaguzi huo,si ndio huo mnaoleta nyinyi kwa wa Tanganyika,hamuwataki Zanzibar.
Swali zuri tumejipanga vipi....Kwakuwa tuna akili timamu, na kwakuwa tunajuwa kuwa Katiba ya JMT ndiyo sheria mama, Tutatumia kifungu cha 31 cha rasimu kwani ikishapitishwa itakuwa ni katiba ya JMT
Mawazo mgando kama ya hawa kina Boribo wala hayawezi kutukosesha usingizi kwani hao hao pamoja na wewe mnadai hamuitaki BAKWATA kisa "imeanzishwa na serikali" lakini mnataka mahakama ya kadhi tena inayoanzishwa naserikali hiyo hiyo!! sijuwi mnatumia nini kufikiri anyway!! mnapaswa kusikitikia. Na kama hujakiona hicho kifungu cha 31 soma hapa chini upate kuelimika.
Uhuru wa
imani ya dini
31.-(1) Kila mtu anao uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi
katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini,
imani yake au kutokuwa na imani na dini.
(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa
ni huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ili mradi asivunje sheria za nchi.
(3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya
shughuli za mamlaka ya Serikali.
(4) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini ya
taratibu zilizowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya
kidemokrasia kwa ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii na
wa kitaifa na vitasimamiwa kwa utaratibu ulioainishwa kwenye sheria za
nchi.
(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru
wa kutangaza dini kwa kukashifu imani na dini nyingine, kujenga chuki au
kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini.
(6) Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyote
itakayowagawa wananchi, kuleta uhasama au kuharibu amani miongoni
mwa wananchi.
(7) Neno dini kama lilivyotumika katika Ibara hii litatafsiriwa
kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno
mengine yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa
kwa maana hiyo.
Hakuna anayeifikiria zanzibar kama unavyojidanganya bali kiukweli tunawasikitikia kwa kutema asali na kumeza pilipili. Kwamba waswalili wanasema toa boriti nikusaidie tu sio waswahili bali hayo ni maneno ya Bwana Wetu Yesu Kristo Mwana wa Mungu hivyo koma kuyaita maneno ya waswahili.
Hata ya kuchinja yalianza hivyo hivyo. Vipi katiba yenu inasemaje nani mwenye haki ya kuchinja katika public?
Siku zote mnapenda kutoa majibu rahisi kwa masuala magumu.
Kazi kwenu. vipi nako mtwara? au ndio nguvu kutoka nje zinazosukuma hayo?
Kumbuka hata mbuyu ulianza kama mchicha. yetu macho.