Alichokisema nabii Bashando baada ya huduma WRM iliyo chini ya nabii Suguye kufungiwa

Alichokisema nabii Bashando baada ya huduma WRM iliyo chini ya nabii Suguye kufungiwa

cult ni imani kama ilivyo dhehebu lako unalo abudu, serikali haitakiwi kuingilia imani ya mtu yeyote kama hamna kosa lolote linalovunja sheria za nchi.

Cult sio dhehebu, ni imani kwa mwasisi wa dini sio Mungu. Akina kibwetere, Akina Jim Jones akaaua maelfu ya watu, akina David koreshi na juzi hapa Tanzania mungu Zumaridi.
 
Mambo ya aibu yanatokea kanisani mpaka serikali imeingilia Kati. Huku Zumaridi anajiita mungu huku Suguye na kucha zake. Mambo ya ajabu Sana,
 
Serikali iongeze kibano dhidi ya hawa wajasiriamali wa Injili, waabudu mashetani, occultic prophets wanaojificha nyuma ya neno ufunuo. Wakiacha wakaota mizizi kama Nigeria au South Africa taifa litakuwa kwenye hali mbaya sana. Hakuna jina lingine alilopewa mwanadamu limpasalo kuokolewa kwalo zaidi ya jina la Yesu. Kutumia visaidizi kama chumvi, maji au mafuta ni ushirikana kama ushirikana mwingine tu.
 
Waache kutafuta huruma mitandaoni. Wafanye kama manabii wengine walivyofanya. Nabii Eliya alivyoona anaonewa na dola alifunga anga mvua isinyeshe. Sasa zamu ya Suguye kusimama kama Nabii
We utakuwa mpumbavu hakika,unadhani isiponyesha mvua hao watu wa serikali watakufa njaa?

Hizi sijui ni roho za kichawi hizi?!Watu wafe njaa kwa sababu ya suguye?
Hivi hujui hata wachawi wanafunga mvua isinyeshe wakipata watu wajinga kama wewe?!

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna kufunguliwa, njaa hadi iwatie adabu, kwanza uaskofu umepewa na nani ww? Mnapeana majina kila aina kutafuta fedha, mara Nabii, mara askofu, mara mtume, serikali imefanya uamuzi mzuri sana, sisi tunasimama na serikali

Kwani kuna sehemu maalumu ama utaratibu maalumu wa kupewa hayo majina?naomba unielekeze hiyo sehemu.
 
Alichokisema Nabii #Bashando "Mimi ni miongoni mwa watu ambao sikuuelewa kabisa ufunuo wa nywele na kucha wa Nabii Suguye, na niliukosoa hadharani, ila pamoja na kutokuuelewa haunipi sababu ya kushangilia huduma ya WRM kufungwa.

Hapa kuna jambo ambalo watu wengi hatuelewi.

Ni kwamba kuna tofauti kubwa kati ya Suguye na WRM, ambapo Suguye ni mwenyekiti wa taasisi ya WORD OF RECONCILIATION MINISTRY (WRM) na mtu ambaye Mungu anamtumia katika huduma ya kinabii, na WORD OF RECONCILIATION MINISTRY ni kanisa ambalo watu wanakusanyika kumwabudu Mungu.

Hivyo basi kufunga kanisa la WRM siyo kumkomoa Nabii Suguye bali ni kuwakomoa watu elfu nne waliyoamua kuabudu ndani ya kanisa la WRM.

Ndiyo maana Suguye alisafiri kwenda Marekani lakini WRM ikaendelea na shughuli zake hapa Tanzania. Kilio changu kikubwa mimi kama mwenyekiti wa UMOJA WA HUDUMA ZA KITUME NA KINABII TANZANIA (UHKKT), ni watu elfu nne kunyimwa haki yao ya kikatiba ya kuabudu.

Lakini pia ni kuipunguzia serikali mapato ya fedha za kigeni ambazo watu kutoka mataifa mbalimbali walikuwa wanakuja Tanzania kwa ajili ya kufuata maombi katika huduma ya WRM.

Nirudi kwenye swala la ufunuo wa kucha na nywele, inawezekana Nabii Suguye akawa alionyeshwa na Mungu au lah.. Lakini hata kama ufunuo ule ulikuwa haujaeleweka au una makosa ndani yake, siyo jukumu la serikali kuingilia kati huo ufunuo maana serikali haina dini, na katiba imetoa uhuru wa watu kuabudu bila serikali kuingilia..

Serikali inaweza kuingilia kati ibada ambayo itajumuisha jinai ndani yake... Kwa mfano ningesikia Nabii Suguye amekamatwa kwa sababu ametuhumiwa kuuza madawa ya kulevya, kubaka, kuiba, kuua, au kuvunja sheria za nchi kwa namna yeyote ile, hapo nisingefungua mdomo wangu kuongea, ningesubiria kuona mahakama ikitenda haki..

Ndiyo maana siku ya kwanza tu nilipopewa taarifa kuwa huduma ya WRM imefungwa nilipiga simu kwa Msajili na kumuuliza kuna jinai gani imegunduliwa katika huduma ya WRM? Na nilipopewa jibu nikamtafuta Nabii Suguye na uongozi wake bila mafanikio hadi hapa juzi nilipofanikiwa kuonana na Nabii Suguye uso kwa uso ndipo nikasikiliza kwa upande wake na kubaini baadhi ya makosa ndipo nikaamua kusimama na Nabii Nicolous Paul Suguye .

Kama tatizo ni ufunuo wa kucha na nywele naamini BARAZA LA MAKANISA YA KIPENTEKOSTE TANZANIA (CPCT) lipo na lina mamlaka ya kumuita kiongozi yeyote wa imani ya kipentekoste na kumuhoji na kutafuta busara ya kuondoa sintofahamu iliyojitokeza kwenye jamii..

Lakini kwa kuwa huduma ya Suguye siyo mwanachama wa CPCT bado CPCT wangeweza kuutumia UMOJA WA HUDUMA ZA KITUME NA KINABII TANZANIA kumuita Suguye na kukutana nae kwa kikao cha kuondoa sintofahamu iliyojitokeza, maana kucha na nywele ni swala la kiimani ambalo lingeweza kutatuliwa na baraza na chama cha imani husika.

Tukija kuruhusu mambo haya yaingiliwe na serikali kwanza tutakuwa tunafungua mlango wa serikali kuendesha ibada zetu na huko mbeleni tutashindwa hata kulitaja jina la Yesu Kristo na kuanza kusifia watawala na sera zao, na jambo la pili ni kupunguza nguvu kwenye baraza na umoja wa huduma...

Ushauri wangu kwa mitume na manabii wote wa Tanzania, msiyadharau haya mabaraza wala vyama ambavyo vina dhamana kisheria ya kutafsiri imani mbele ya serikali, ni vizuri kabisa kuomba uanachama na kujiunga ili serikali inapowatafuta iwakute huko ndani, lakini pia muwe na nguvu ya kushiriki uchaguzi wa kuchagua viongozi ambao hawatakuwa na udhehebu wa kutumia vibaya nafasi zao kuchongea watu wa imani ambazo hawajazielewa..

Najua kwenye utumishi kuna makosa mengi sana na katika makosa hayo inabidi kupata viongozi wanaoweza kulea na kuonya kwa upendo kwa kusudi la kurekebisha na siyo kukomoa kwa maslahi ya kidini na kidhehebu...

Ile dhana ya kusema unajitenga peke yako ili uweze kufanya huduma kiutulivu, hautaki chama wala baraza siyo njema sana, jitahidini kushirikiana na baraza na chama kwa maslahi ya mwili wa Kristo....

Namalizia kwa kusema, kama serikali imeweza kumtikisa mtumishi mkubwa kama Suguye, vipi mimi na wewe ambao ndiyo tunaanza huduma? Ninavyosimama na Suguye simuoni yeye kama Suguye ila ninaona hatari kwa watumishi wadogo mnaoanza huduma na hamna hata usajili, tukilinyamazia hili kwa kweli huko mbele mambo yatakuja kuwa magumu kama ilivyo nchi ya Rwanda.

Nimeona comment za watumishi wanaoanza huduma wakicheka na kufurahi kwa kilichoipata huduma ya WRM nikakumbuka usemi ambao Yesu alisema, "HERI MNAOCHEKA SASA KWA MAANA MTALIA NA KUSAGA MENO....

Mimi Mhashamu Baba Askofu Bashando nasimama na Nabii Nicholaus Suguye 🙏
View attachment 2469637
Sasa tunashindana na Nigeria kuwa na matapeli wanaojiita manabii. Ningekuwa rais wangekimbia nchi. Angalia Rwanda, hawana upuuzi huu wa manabii wa urongo
 
Hawa ni wachumia tumbo. Ukristo unachezewa sababu ndio dini pekee ukiwa na biblia unaweza kufanya chochote kwa jina la Ukristo!

Serikali haipaswi kuingilia lakini hata hilo baraza lao ni waganga njaa na wenye matendo binafsi yanayowafanya wasiweze kukemeana! Bora mchungaji mdhambi kuliko anayetumia maandiko kupotosha imani.

Kutafuta ugali kwa jina la muumba hapana! Bashando ambaye siku hizi ni chawa wa nabii kama yule wa Arusha ni dhahiri hamtetei Kristo. Hukumu mbinguni ipo ndugu zangu!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
KAMA swala ni kumuabudu Mungu mwenyezi, Mungu mkuu, Mungu wa kweli, Jehovah, Yesu Kristo aliye hai hata nyumba ya ibada ifungiwe kanisa litaishi milele

MATHAYO 16:18
"Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda."

YOHANA 4:23
"Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu."
Tatizo mnafikiri kila kinachoitwa Kanisa ni Kanisa.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Biashara mpya imezuka ya kuuza maji na mafuta. Mwenye kanisa (Kristo Yesu) akawaonya wafuasi wake miaka hiyo kama anavyoonya leo. "na manabii wengi wa uongo watatokea... nao WATAWADANGANYA WENGI" Angalia, usiwe miongoni wa wajinga wanaodanganywa.
 
Hawa manabii kwa kweli naomba Mungu anisamehe ulaji Sanaa upo mbele.
Uzuri wake hawa manabii huwa hawagongi hodi nyumbani kwa mtu kuwaita waje kusali na kutoa sadaka.Ni watu wenyewe kutaka ku-fasttrack hata mambo ya Rohoni ndiyo yanayowakosti wahanga.na wataendelea kupigwa."Ukiijua kweli itakuweka huru na utakuwa huru kweli kweli"
 
Sio rahisi kama unavyofikiria
Huo ndio ukweli acha kujifariji hivi nikuulize kati ya waislamu na wakristo nani wanaongoza kusilimu? Kwahuku wilaya ya masasi kila ukiokawa ukoo wa wakristo tupu kuna waislamu na vile vijiji ambavyo kulikuwa na ukristo tupu saivi kuna waislamu kibao wanawake na wanaume wanasilimu balaa sana
 
Huo ndio ukweli acha kujifariji hivi nikuulize kati ya waislamu na wakristo nani wanaongoza kusilimu? Kwahuku wilaya ya masasi kila ukiokawa ukoo wa wakristo tupu kuna waislamu na vile vijiji ambavyo kulikuwa na ukristo tupu saivi kuna waislamu kibao wanawake na wanaume wanasilimu balaa sana
Basi imekuwa tofauti, sisi huku nyanda ya juu kusini tunaufuta uislamu. Kila mkutano wa injili tunaofanya kuna waislamu wanaokoka. Wiki iliyopita kuna shehe wa BAKWATA wilaya moja aliokoka maana tulimuombea na akatokwa mapepo na sasa anamtumikia Yesu aliye hai. Huko Masasi ni eneo lenye waislamu wengi na binafsi nieleweshe huyo/hao wakristu wanabadilisha dini au mnakutana nao vipi hadi abadili dini zaidi ya mbinu yenu ya kuoa wakristo?
 
Back
Top Bottom