Alichokisema nabii Bashando baada ya huduma WRM iliyo chini ya nabii Suguye kufungiwa

Alichokisema nabii Bashando baada ya huduma WRM iliyo chini ya nabii Suguye kufungiwa

Basi imekuwa tofauti, sisi huku nyanda ya juu kusini tunaufuta uislamu. Kila mkutano wa injili tunaofanya kuna waislamu wanaokoka. Wiki iliyopita kuna shehe wa BAKWATA wilaya moja aliokoka maana tulimuombea na akatokwa mapepo na sasa anamtumikia Yesu aliye hai. Huko Masasi ni eneo lenye waislamu wengi na binafsi nieleweshe huyo/hao wakristu wanabadilisha dini au mnakutana nao vipi hadi abadili dini zaidi ya mbinu yenu ya kuoa wakristo?
"Huko Masasi ni eneo lenye waislamu wengi"
[emoji115][emoji115]
Umechanganya. Masasi kuna Wakristo wengi, Mtwara na Newala ndiko kwenye Waislamu wengi.
 
Nabii wengi ni waongo na wazinzi Sana, hongera kwa serikali kufungia makanisa Kama haya.
 
cult ni imani kama ilivyo dhehebu lako unalo abudu, serikali haitakiwi kuingilia imani ya mtu yeyote kama hamna kosa lolote linalovunja sheria za nchi.
Je mkuu emmarki kuwaingiza watu kwenye vifungo (bondage) kwa njia ya kukanyaga maji, mafuta au kwa njia ya nywele au kucha za watu SIO harakati za kuuinua ufalme wa Shetani? Natambua mambo kama niliyoyataja hapo juu huwezi kupeleka ushahidi wake mahakani LAKINI kama Serikali imeona kuna ushahidi wa kimazingira ni wajibu wake wa kikatiba kuchukua hatua stahiki (kuwalinda raia wake). Najua utaniambia hao watu wanajipeleka wenyewe kwenye hizo CULTS, LAKINI serikali ikae kimya mnapoongeza idadi ya watu (ZEZETA) mlioshika ufahamu wao katika kufanya maamuzi yenye tija kwa taifa.

Mkuu emmarki naomba uelewe kwamba mimi nimeokoka na kwa bahati mbaya nilishawahi kuwa "Victim" wa hizi CULTS hivyo naandika ninachokijua.

Ahsante
 
"Huko Masasi ni eneo lenye waislamu wengi"
[emoji115][emoji115]
Umechanganya. Masasi kuna Wakristo wengi, Mtwara na Newala ndiko kwenye Waislamu wengi.
Ni kweli inawezekana nimechanganya kwani sijawahi kufika wala kuishi huko zaidi ya kusikia Ukanda wa Pwani una waislamu wengi kuliko kanda nyingine.
 
Nitajie jina la huyo shehe wa wilaya na wilaya yake nimekuambia ni ngumu mno kwa mtu aliyeusoma uislamu kuja kuwa mkristo
Nikishakutajia then utafanya nini? Kwa hiyo hakuna waislamu wanaosilimu? Ninahubiri sasa maeneo mbalimbali zaidi ya miaka 6 sasa najua nisemalo bro. Tumesoma na nimewaona Masheikh walio okoka na tukaenda soma nao vyuo vya Kupanda makanisa vya TAG pia wengine wamesoma pale CBC Dodoma.
Pia, naomba unisaidie. Mnakutana wapi na Mkristo hadi abadili dini na kuwa muislamu zaidi ya kumuoa kama Ambavyo nimemuoa Aziza Abdallah akawa Mkristo tofauti na sisi tunaohubiri, tunawekea wagonjwa mikono na wakapona, tunawatoa mapepo masheikh n.k
 
Wajinga waliwao

Endeleeni kuwatolea sadaka,nunueni maji mafuta yao,mzidi kuwatajirisha

Huku nyie mkiishi kama manyangau na misukule

Ova
 
Nikishakutajia then utafanya nini? Kwa hiyo hakuna waislamu wanaosilimu? Ninahubiri sasa maeneo mbalimbali zaidi ya miaka 6 sasa najua nisemalo bro. Tumesoma na nimewaona Masheikh walio okoka na tukaenda soma nao vyuo vya Kupanda makanisa vya TAG pia wengine wamesoma pale CBC Dodoma.
Pia, naomba unisaidie. Mnakutana wapi na Mkristo hadi abadili dini na kuwa muislamu zaidi ya kumuoa kama Ambavyo nimemuoa Aziza Abdallah akawa Mkristo tofauti na sisi tunaohubiri, tunawekea wagonjwa mikono na wakapona, tunawatoa mapepo masheikh n.k
Hebu nikutajie watu maarufu waliosilimu tukianza na bongo 1 james tupatupa 2 batilda burian 3 barnaba 4 rose ndauka 5 mchungaji mwaipopo,,,nawewe nitajie 5 maarufu waliotoka uislamu kuwa wakristo
 
"Huko Masasi ni eneo lenye waislamu wengi"
[emoji115][emoji115]
Umechanganya. Masasi kuna Wakristo wengi, Mtwara na Newala ndiko kwenye Waislamu wengi.
Huyo haelewi chochote kilè na kwa taarifa yake ajue kulikuwa na vijiji hata hawakuwa wanaujua uislamu ni nini ila leo misikiti imejengwa na wanasilimu kila kukicha
 
Serikali iachane na kuingilia mambo ya dini kabisa kama amani ya nchi haivunjwi na wenye imani hizo.
 
Chama cha mitume na manabii [emoji23][emoji23], mbona mnatoka kwenye lengo lenu la injili
 
Mkuu emmarki pokea salam za Upendo.
Niliposikia habari kumhusu Subuye na huduma yake kufungiwa na serikali ilinifanya kufanya utafiti kidogo kuhusu huyu ndugu. Taarifa nilizozipata kuhusu Subuye tangu akiwa mwana kwaya wa kanisa kule mwananyamala, alivyohamia kwenye biashara ya Hardware na hatimaye kuanzisha huduma yake iliyokua haraka kama uyoga zimenipatia maswali mengi kuliko majibu na baadhi ya niliambiwa ni aibu kwa mwili wa kristo hata kuyataja hapa.
Naomba kwa kuanzia niulize maswali yafuatayo:-
1. Unadhani Serikali imekosea kwa hatua ilizozichukua? Nikuhakikishie hayo ambayo hujaambiwa ni mazito na aibu kwa mwili wa kristo
2. Unadhani kwanini Subuye hajajiunga na jumuiya yeyote ya Kipentecoste? Hata angekuwa amejiunga je ninyi mna mnauwezo kumchukulia hatua za nidhamu mwanachama wenu?
3. Kwanini mmejeuza kuwa fashion uanzishwaji wa huduma za kifamilia (Wenye huduma na mali za huduma ni Mr & Mrs tu na sio Baraza la wadhamini).
4. Je hauoni wakati umefika wa kupiga marufuku uanzishwaji wa huduma mpya za kifamilia na kuhimiza zilizipo ziungane ili kuwa na huduma chache (Institutional ministries) ili kuepusha ya Subuye na CULT MINISTRIES zinazoota kama uyoga
5. Je huu utitiri wa huduma unaongeza kweli kwenye Nchi idadi ya watu wenye hofu ya Mungu?

Naomba Serikali isiishie kwa Subuye inyoshe mkono wake kwa kuzifungia huduma (CULT) zilizosalia.

Ahsante
Fafanua kidogo hapo kwenye cult ministries
 
Sihami RC mimi, endeleeni kupeleka kucha na nywele
 
Ila hizi Misnistries hizi jamani,kuna moja nimeona jamaa wanamwagiwa maji ya upako kwa kutumia Pump ya kumwagilia dawa mimea,nyingine jamaa anawakanyaga waumini migongoni ili wapate upako,kuna moja niliona unachapwa fimbo ili sijui ndio upate roho mtakatifu hata sikuilewa ile.Kuna mahali hawa watumishi wanakuwa kama wamepagawa na hela,wanaanza kuanzisha mambo yao ya kutunga ambayo hata hayapo,tusisahau uzembe wa kuziachia hizi ministries ulisababisha mmoja akawachoma waumini kanisa zima kule Uganda.Lord have mercy...
 
Back
Top Bottom