MALISA
#UpdstesKisutu
WAKILI WA JAMHURI: Mheshimiwa tuna maombi mawili mbele ya Mahakama yako tukufu. La kwanza tunaomba Mahakama kumpa AMRI Boniface atoe Password yake ya mtandao wa X (Twitter) ili kukamilisha upelelezi.
WAKILI WA JAMHURI: Law enforcement Officers wanashikilia simu mbili za Boniface aina ya Samsung. RCO Msangi alipomtaka atoe Password alikataa, hivyo upelelezi ulikwama. Kwahiyo tunaomba mahakama kutoa AMRI ya kumlazimisha Boniface atoe password ili kukamilisha upelelezi.
WAKILI WA JAMHURI: Mhe.Hakimu tunaomba upande wa utetezi watujibu ili tuwasilishe maombi ya pili.
HAKIMU: Upande wa utetezi mnajibu moja moja au wamalizie zote?
WAKILI KIBATALA: Wawakilishe zote Mheshimiwa.
HAKIMU: Jamhuri endeleeni.
WAKILI WA JAMHURI: Ombi la pili, tunaomba Mtuhumiwa asipewe dhamana mpaka hali itakapokuwa nzuri, ili asitekwe au kuuliwa kwani alisema yupo kwenye danger. Natambua dhamana ni haki yake ila alimwambia RCO Msangi kuwa yupo kwenye risk ya kutekwa na kuuawa. Hivyo tunaomba asipewe dhamana kwa usalama wake.
HAKIMU: Upande wa utetezi mpo tayari?
WAKILI KIBATALA: Ndio Mheshimiwa Hakimu.
WAKILI KIBATALA: Sheria inasema (anataja vifungu) OCS ndiye anayeruhusiwa kutazama simu ya Mtuhumiwa na si RCO. Kwanini RCO Msangi alitaka simu ya Boniface wakati OCS alikuwepo?
Pia sheria inasema (anataja vifungu) anayepaswa kuleta maombi ya password Mahakamani ni Polisi sio Jamhuri. Mpaka sasa Polisi hawajaleta maombi yoyote mahakamani. Na hii inadhihirisha hawana shida na password ya Boniface. Sasa nyie Jamhuri mnataka password kwa sheria ipi?
WAKILI KIBATALA: Pia hii Application haina kifungu chochote cha sheria, haina individual Callander wala criminal case number. Mheshimiwa Hakimu; Hawa wanataka Mahakama yako itoe Amri wakati application yao haina hata case number? Watu watakushangaa Mheshimiwa. Pia affidavit yao inasema simu ni Samsung. Lakini ni Samsung gani, yenye IMEI number? Line gani za simu? Mheshimiwa Hakimu naomba utupilie mbali maombi ya Jamhuri.!
INAENDELEA......