Alichokosea Dr. Msolla kuhusu mashabiki Yanga kuchangia usajili

Alichokosea Dr. Msolla kuhusu mashabiki Yanga kuchangia usajili

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Dr. Msolla kwa nia njema kabisa alisema kuwa wadau wa Yanga wachangie fedha ya kusajili wachezaji 2 wa kigeni.

Kwa kauli hii dk Msolla Amevuruga saikolojia ya wachezaji, amevuruga saikolojia ya Wana Yanga na amewapa nafasi upande wa pili kutibua vichwa vya wachezaji na mashabiki wa Yanga kuwa hakuna hela.

Haieleweki kama haya ni mawazo yake binafsi, ni mawazo jumuishi ya uongozi wa Yanga au Ni GSM wametaka wadau pia wachangie au Kuna mgogoro wa usajili Kati ya GSM na uongozi wa club.

Kama hao wachezaji 2 hawamo kwenye mipango na Budget ya GSM je, mishahara ya hao wachezaji itategea pia bakuli au Ni vipi?

Kauli hii ya Mwenyekiti imewafanya wachezaji kuvurugukiwa, maana wanazo kumbukumbuku ya misimu iliyopita ya kuchangiwa na wadau.

Maswali yote haya yamesababishwa na Dr Msolla kwani sio lazima wachezaji wawe 10.
 
Hakika Mwenyekiti Wetu HAKUPIMA VYEMA KAULI Yake ile,ikiwa aliipima basi KLABU Ina ficha HALI HALISI ILIYOPO....daaah tunaoumia Ni Sisi wanachama.....
 
Kuna thread humu nimeiona kwamba majina yameshaenda FIFA na CAF, wachezaji 9 wa kigeni akiwemo Morrison, hapo si anakuwa amebaki mmoja pekee?

Hii imekuwaje tena?
Huyu Morrison Imekuwa Ni siasa kwa viongozi wetu.....Unajua inachekesha Sana;TFF wametuambia Morrison Mchezaji Huru....Sasa Inashangaza kwa Uongozi wetu kusema YUKO katika Usajili😁😁.

Ili uwe Kiongozi Wa Hivi Vilabu Vyetu Ni Lazima UWE MTU WA BENDERA FUATA UPEPO TU Mana ukiamua kusimama kiuongozi,Kesho tu HAUTOKUWEPO....😂😂
 
Poleni sana.

Kwanini msisajiri wachezaji kutokana na uwezo wenu ?
Nani anawashinikiza kwamba ni lazima muwe na wachezaji wa kigeni kumi ?

Mjitafakari.
 
Walinzi wa Usiku tafahamiane kabisa hapa.
Maana ndio binadamu pekee tunaoishi usiku tukiwa macho.
Ikitokea kiama kinakuja usiku ni sisi pekee tutakao kwenda mbinguni.
Wengine watakuwa wanalala fofofo
😁😁😁Aaagh Ndg yngu weee,Tuko vibandani tunakimbiza mbu kwa kuwa JF hapa tunawalinda maboss wetu wahindi Ukorokoroni Kaka,Mikocheni Moja Hiyo!!
 
Yanga hovyooo. Unapeleka jina la Morrison CAF na FIFA ili iweje? TFF imeshamkata mkia na YANGA hamlipi chochote, sasa mnamng'ang'ania kivipi? Au ni Mwanamke mweupe na ninyi ni wasukuma?!?
 
Huyu mwenyekiti muda wake wa kuongoza Yanga unakaribia mwisho.
 
Yanga hovyooo. Unapeleka jina la Morrison CAF na FIFA ili iweje? TFF imeshamkata mkia na YANGA hamlipi chochote, sasa mnamng'ang'ania kivipi? Au ni Mwanamke mweupe na ninyi ni wasukuma?!?
Hapo Sasa😁😁😁

Siasa za viongozi kucheza na HISIA za Mashabiki wengi WANAOPENDA KUSIKIA HARUFU ya nyama Kikaangoni ilihali mume Hyo Robo Unga Pia Kakopa....
 
Msolla na ndugu yake mkwassa popote wanapokuwepo lazima pafeli
 
Afu utakuta shabiki wa utopolo amekomaa,,mo weka billion 20 ulizo ahidi kuweka kwenye account ya simba
 
Yaaaan soka letu ni zaidi ya ukuda kama bakuli linaanza pitishwa mapema ivi bado shabiki hajanunua jezi mpya ,bado hajaenda na kusafiri uwanjani kukutana na dispointment ....nahisi swala la morison ni amsha amsha za simba na yanga tu .....ila katika hili la bakuli kazingua
 
Yanga hovyooo. Unapeleka jina la Morrison CAF na FIFA ili iweje? TFF imeshamkata mkia na YANGA hamlipi chochote, sasa mnamng'ang'ania kivipi? Au ni Mwanamke mweupe na ninyi ni wasukuma?!?
Kwani Msolla bado anamlipa mshahara Morrison hadi Sasa Kama mchezaji wa Yanga? Kama ameacha kumlipa anakuwaje mchezaji wa Yanga? Au kanuni zinasermaje?
 
Kuna thread humu nimeiona kwamba majina yameshaenda FIFA na CAF, wachezaji 9 wa kigeni akiwemo Morrison, hapo si anakuwa amebaki mmoja pekee?

Hii imekuwaje tena?
Hivi unajaza vipi mkataba TMS bila kuambatanisha na mkataba. Je, wao wawili wameambatanisha na mkataba upi wakati TFF wameukataa mkataba?
 
Back
Top Bottom