DR VRM
JF-Expert Member
- Sep 9, 2024
- 3,933
- 3,071
Kwa kweli ameshindwa kuwasilisha au kuwakilisha alichokikusudia na badala yake anaelekeza kwenye kamati ya Raisi inayojihusisha na uteuzi ,ambapo hapa Gwajima amepaona ndiopo penye ukakasi wa wakuu wa ulinzi kwa ujumla wao kusitishwa kuendelea na uchunguzi utekelezaji au ufuatiliaji endapo kuna harufu au uhakika wa wanayoyafuatilia kuwagusa wakuu wa nchi, au kashindwa kusema wakuu wa CCM.
Hatuba yote ya Gwajina imeshindwa kuwalaumu wakuu wa vyombo vya ulinzi kwa ujumla wao na haswa Police na Usalama wa Taifa.
Tunaona nchi za walizo endelea wakuu hawa wakiwemo Mawaziri hujiuzulu mara moja na ikiwa Gwajima kwa alivyo wagusa wakuu kuwa wana watoto wana familia na hili na lile, hivyo inabidi inabidi wamezee ,Wakuu wanaweza kumjibu Gwajima kuwa wao hawapo kwa ajili ya wananchi wote wapo kwa ajili ya matumbo yao.
Kwajima amegusia kuwa Raisi huwaondoa au hufukuza Gwajima amekosea (Raisi hajamfukuza mtu kazi anabadilisha).
Hapa hapatakiwi kubadilisha wala kufukuzwa kunahitajika yanapotokea matokeo(Tuseme utekaji) na hakuna alietuhumiwa na mwishowe kukamatwa ,wakuu wa vyombo vya ulinzi husika akiwemo Waziri ni lazima kuwajibika kwa kujiuzulu.
Tuchukuwe lile tukio la kuchukuliwa watu Mahakani na gari zinazosemekana za polisi na watu waliovalia mavazi ya kipolisi hawa wanawakilisha Jeshi la Ulinzi la Polisi mbaadae unasikia Mkuu wa polisi akisema hajachukuliwa mtu na polisi haina taarifa ya tukio hili,
Inawezekana wakuu hawa wa Polisi wanaishi katika wakati uliopita na kwa muda huu wapo wapo tu,
Maana kuna watu waliokuwepo na kurekodi tukio mbali ya vyombo vya habari hata watu wa kawaida siku hizi automatikc ni wahabarishi na pengine huwezi hata kujua kama wapo karibu yako.
Hapo Waziri au Mkuu wa Jeshi la polisi ilikuwa mara moja achukuwe hatua juu ya viongozi wa polisi walioko katika eneo na kwa yule kamanda alietoa tangazo la UWONGO kuutangazia umma wa watanzania kuwa Polisi hawana habari kwa kilichotokea ,
Tuseme kama si wao na walikuwepo kwenye eneo wangelijivua kwa kusema waliochukuwa raia ni Kikosi kutoka usalama wa Taifa ,ila kusema hawana habari na tukio limetokea na kuna polisi wa kudumu katika mageti ya mahakama, Waziri na Mkuu wa polisi .
Na hivi vyombo vyetu vinajua kuhoji mambo ya udaku tu lakini vinashindwa kuwahoji direct wakuu husika wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa masuali ya kutoa jasho na yahusuyo matokeo mazito ,japo jawabu tunalijua kuwa ...suala hilo lipo kwenye uchunguzi na uchunguzi ukikamilika tutakuja kuwajulisha.... ndio imetoka au imekula kwao.
Gwajima kabla ya kufika kwenye maeneo ya Raisi na teuzi kwanza angawakaba koo hawa viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa raia na baadae akapanda ngazi kwa Raisi. Huenda Raisi anawabadilisha watu kwa kusema Polisi haina habari yoyote.
View: https://youtu.be/WHnxlsWXiY0