Mbona nyumba hii nzuri? Tembea uone....! Nyumba hii imeezekwa kwa bati, japo kwa kushindilia kwa mawe....! Nyumba hii imesimama imara, japo ni ndogo na ni dhahiri kuwa haitadumu kwa miaka mitatu...! Si ajabu ukikuta nyumba hiyo ni ya balozi au mwenyekiti wa kitongoji wa CCM....! Mabango yaliyobandikwa hapo yameprintiwa kutoka Canada kwa udhamini wa ikulu ya Jamhuri wa Muungano Tanzania...! Gharama ya bango moja inazidi gharama ya bati moja hadi hapo....! Fika katika ngome za CCM kama vile Ngorongoro, Longido, Monduli, Kiteto, Simanjiro.