Alichosimulia Edgar Mwakabela "Sativa" kuhusu waliomteka na kumpiga Risasi ya Kichwa

Alichosimulia Edgar Mwakabela "Sativa" kuhusu waliomteka na kumpiga Risasi ya Kichwa

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
KUTEKWA, KUPOTEA, KUTESWA, KUPATIKANA KWA SATIVA

1719657668612.jpeg

Edga Mwakabela (Sativa225)

Maelezo yote yametoka katika kinywa cha Edgar Edson Mwakabela (Sativa255) ambaye alitekwa jumapili 23.06.2024 Darces Salaam na kupatikana 27.06.2024 Katavi.

Shughuli inaanza siku ya Jumapili, 23.06.2024, maeneo ya Ubungo. Edgar Edson Mwakabela aliagana na kaka yake Patrick, na akaanza safari ya kurudi Kimara.

Walitoka wote Coco Beach. Baada ya muda, Patrick alimuuliza kama amefika salama, hakujibiwa ujumbe wake, na simu za SATIVA baada ya hapo hazikupatikana tena.

SATIVA alikuwa anatafuta chumba, wakakubaliana na dalali kwamba hiyo sehemu ambayo anataka kuhamia, mpangaji katika nyumba hiyo anatoka mwezi wa (10) Oktoba.

Baada ya muda mfupi, dalali akarudi kumpigia simu SATIVA akimueleza kwamba jamaa katika nyumba ile ametoka hivyo anaweza kufanya malipo yake muda huo.

Wakati huo, SATIVA alikuwa amewaaga rafiki zake aliokuwa nao, akawa amechukua usafiri wa bodaboda, alipopigiwa simu na dalali, akabadilisha bodaboda yule.

Wakati akishuka na kutafuta bodaboda nyingine kueleka alipo huyo dalali, akawekwa mtu kati na watu watatu. Wakamfunga pingu na kumtupa katika gari waliyokuja nayo.

Watekaji hao walimpokonya simu zake zote tatu. Simu mbili walizima. Simu moja ikabaki hewani kwa muda mfupi, baadae simu zote za SATIVA zikawa hazipatikani.

Wakaondoka naye hadi kituo cha Polisi Oysterbay, Mkoa wa Kipolisi - Kinondoni. Hapo wakamfikisha nyuma ya kituo cha Polisi Oysterbay, wanapaita 'karakana"

SATIVA akiwa karakana hapo majira ya saa 2 usiku, waliendelea kumuuliza, kosa lako ni lipi? Umewakosea jambo gani wakubwa hadi kuagiza ukamatwe na kuteswa?

Inavyoonekana, watekaji hao walikuwa na maelekezo ya kumteka SATIVA tu lakini hawakujua kwanini wametumwa kumteka. SATIVA aliwaambia hajui kitu yoyote.

Lakini katika maswali yao ya msingi waliendelea kumuuliza, rafiki zako ni akina Martin Maranja Masese na Boniface Jacob? Mnakutana wapi kupanga mambo yenu?

Akiwa hapo karakana ya magari ya kituo cha polisi Oysterbay, alifika mtu mmoja akiwa ndani ya gari aina ya VX V8 akashuka akiwa amevaa jezi ya timu ya Simba SC.

Mtu huyo chini alivaa pensi ya rangi ya kaki. Kwa muonekano wa nje alikuwa ni mtu wa mazoezi, mrefu wa wastani na siyo mweupe sana. Huo ni wajihi wake wa nje.

Mtu huyo aliposhuka kwenye gari akiwa pekee yake, wale waliokuwa pale walimpigia saluti, akamfuata moja kwa moja SATIVA pahali alipokuwa amefungwa pingu mikononi.

Akamuuliza, unaitwa nani? Katika mitandao ya kijamii unatumia jina gani? SATIVA akampa majibu. Baada ya hapo akawavuta pembeni wale watu waliokuwa na SATIVA pale.

Akatoa maelekezo kuwa kuna watu watakuja kumchukua SATIVA, afungwe katika Karakana ya Oysterbay. Akarudi katika gari aliyokuja nayo, ikawashwa, akasepa.

Usiku huo, SATIVA akafungwa pingu katika moja ya nguzo zilizopo katika hiyo karakana ya Polisi - Oysterbay. Wakiendelea kumuuliza SATIVA amekosa nini kikubwa hicho?

Wao walishangaa kiongozi mkubwa kufika hadi hapo Karakana ya Polisi - Oysterbay na kumuhoji SATIVA, jambo ambalo kwao siyo kawaida. Wakajiuliza, kosa lake nini?

Kwamba kiongozi mkubwa ameacha shughuli zake usiku hadi kumfuata hapo, kosa lake ni nini? SATIVA akawaambia kwa kweli hata mimi sijui gani nimefanya hadi sasa.

Kwa maelezo ya SATIVA anasema watu hao watatu waliomkamata awali, hawamkupiga isipokuwa waliendelea kumuuliza makosa yake hadi kuagizwa kuletwa hapo.

Tangu alipofikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay saa mbili na dakika 25 usiku, akafungwa pingu katika hizo bomba za karakana, amefuatwa alfajiri ya kesho yake.

Ilipofika saa 12 alfajiri ilimfuata gari ambayo haina 'playe number' za Tanzania. SATIVA akachukuliwa na kuwekwa katika gari hiyo, na huko ndani akakutana na sura mpya.

Hapo, wale waliomkamata tangu siku ya 23.06.2024 wakawa wamemaliza wajibu wao, akakutana na watu watu waliopewa kazi maalum ya kumtesa na kumuua.

Kitu cha kushangaza zaidi, ndugu na rafiki zake SATIVA walifika hadi kituo cha polisi Oysterbay, wakaelezwa mtu wa aina hiyo hajawahi kufikishwa kituo hicho cha polisi.

Polisi walipewa taarifa ya kupotea kwa SATIVA, na ikafunguliwa jalada katika kituo cha polisi Gogoni - Kimara, na polisi wakatoa Report Book (RB) Na.

Bado ndugu na rafiki zake waliendelea kumtafuta vituo vya Polisi vyote vikubwa na hospitali hadi mochwari, bado SATIVA hakuonekana na polisi walisema hawajui.

SATIVA anasema wakaanza safari ndefu sana, gari ikiwa mwendo, akiwa amefungwa kitambaa usoni. Lakini katika maongezi yao walisema uelekeo wao ni Arusha.

Tangu amekamatwa jana yake, hiyo ni siku nyingine, SATIVA hakuwa amekula au kunywa kitu chochote. Walipofika Mkoa wa Arusha, SATIVA akaomba apewe maji.

Lakini, wakiwa ndani ya gari kabla ya kumshusha walibadilisha aina ya matamshi yao ili SATIVA asiwasome. Mfano ugali wao waliisema ugaliwa. Wali walisema waliwa.

Wakiwa Arusha, walimshusha, akapelekwa katika moja ya mahabusu katika Mkoa wa Arusha lakini hakufanikiwa kufahamu ni mahabusu ya kituo gani cha Polisi.

SATIVA anasema katika hiyo mahabusu amewekwa kwa siku mbili. Kwa mantiki hiyo ni 25/06/2024 na 26/06/2024. Siku hiyo pili wakamtoa ndani ya mahabusu hiyo.

Wakaondoka naye kama wanampeleka katika moja ya mipaka ya Tanzania na kenya. Wakaendelea kumuhoji huko, saa saba mchana wakarudi naye Arusha Mjini.

Wakaanza safari ndefu, anasema walipofika katika moja ya mapori ambayo hajui ni wapi, gari ile ilisimama, wakatoa panga kubwa na kuanza kumpiga bapa za panga nyingi.

Katika mazungumzo yao yote wakati wakimpiga SATIVA mabapa ya panga, walikuwa wakimuuliza kama anatumwa na Boniface Jacob na Martin Maranja Masese.

SATIVA aliendele kusema hawajui watu hao na hajawahi kukutana nao pahali popote. Wao waliendelea kumtesa wakisisitiza kwamba awataje hao watu wanaomtuma.

Mgongo wa SATIVA umevia damu nyingi sana. Mabapa ya panga pia alipigwa sana kwenye kichwa, mapaja na miguu. Akapata maumivu makali sana kwenye miguu na kichwa.

Walimpiga mabapa ya panga zao mengi kwa muda mrefu wakiendelea kumuhoji SATIVA nani ambaye anamtuma kukosoa serikali ya CCM na kutukana viongozi wa nchi.

Mahojiano yao na SATIVA yalijikita katika kufahamu kama Martin maranja Masese na Boniface Jacob ndiyo wanaomtuma kufanya shughuli za kukosoa serikali yao?

Baada ya mateso makali sana, kiongozi wa msafara akaamuru waende wakamalizane naye haraka muda huo. Hapo imefika majira ya nne usiku wakiwa porini sana.

Wakamfunga kitambaa, wakamrudisha kwenye gari na safari ikaanza. Wakijadiliana kwamba, Katavi kuna wanayama wakali na misitu minene, waelekee huko.

Wakafika Katavi saa 10 kuelekea saa 11 alfajiri. Wakaingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi, pembezoni ya mto Ikuu ambao unatajwa kuwa na viboko na mamba wengi.

Wakaegesha gari na kuanza kuingia naye msituni. Kuelekea ulipo huo mto Ikuu. Huko mahojiano yakendelea wakati huo akipigwa mabapa ya panga kila pahali. Noma.

Kwa maelezo yake SATIVA anasema alipigwa pingu na kitambaa usoni. Na wakamueleza kwamba biashara yake itakuwa imeishia katika msitu wa hifadhi ya Taifa ya Katavi.

Kiongozi wa wauaji hao akatoa maelekezo kwa mmoja kati ya wauaji hao kwamba " mpige risasi huyo kibaka tumalizane naye twende zetu". Ikachapwa risasi kutoka kwa nyuma.

Risasi imepita kutoka kwenye upande wa kushoto wa kichwa, ikapita hadi kwenye shavu na kupasua taya mara mbili na kusaga taya. Damu zikamwagika nyingi akiwa chini.

Wakiwa hapo akasikia wakisema hapa kuna fisi wakali sana, ataliwa na fisi au mamba wakali kutoka katika mto huo au viboko wengi waliopo katika mto huo pembeni.0

Baada ya kama dakika mbili wakiwa hapo, akasikia wakiondoka, wakawasha gari. Akapoteza fahamu. Baadae akahisi mwili umepigwa baridi, akaanza kujivuta.

Akajivuta kwenda hadi ilipo barabara, na hapo ndipo akakutana na askari wa doria wa wanayamapori (TANAPA) na wakaanza kumuuliza maswali mengi ya ufahamu.

Sativa alipookotwa na hao watu wakiwepo askari wanyama pori Hifadhi ya Katavi, baada ya kumuhoji kidogo, akapelekwa kituo cha Afya Kibaoni njia ya kwenda Majimoto.

Na kuanzia hapo, hadithi nyingine yote mnaifahamu. Hivyo ndivyo rafiki yetu, Edgar Edson Mwakabela, SATIVA alivyotekwa na maharamia na kuteswa na kunusurika kifo.

NB; Kumbuka, hifadhi ya Taifa ya Katavi katika kundi la wanyama wakali kuna viboko 5,400. Simba 190. Fisi 750. Mbwa mwitu na Mamba sensa haijafanyika. Noma.

Martin Maranja Masese, MMM.

====

Pia soma:

- Kamanda wa Polisi Katavi: Edgar Mwakabela (Sativa255) anasema alichukuliwa Dar hadi Arusha na kisha kutupwa Katavi

- Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana

- Boniface Jacob: Sativa amemtambua ACP Faustine Mafwele miongoni mwa askari waliomhoji Oysterbay alipotekwa
 
Tuliokuwa tunaona mbali tulikua tunasema anayofanya Jiwe kuteka teka watu madhara yake watu watakuja kujionea ni jambo la kawaida tu.
Sasa bibi Tukinao wa Kizimkazi anaona watu wake wanayoyafanya. Yeye anajifanyaga mama huruma, mbona hatumuoni kutoa tamko mgonjwa ahudumiwe kwa gharama zake?

Tukiwaambia tatizo kubwa la nchi hii ni CCM mnatuona mapoyoyo. Walaakini wanaopenda CCM ndio mapoyoyo.
 
au kuna mkubwa aliweka mzigo mrefu alinunua tips zake mkeka ukabuma, dogo akamjibu uharo 😂
Dogo mweupe sana kichwani sioni hata sababu ya kuhangaika nae, itakua Kuna mtu ambae anajiona Mungu mtu dogo alimtukana, maana kama matusi kwa sativa ndo nyumbani, Yani matusi ya nguoni mpaka kwa mama za watu ye hawazi
 
Mmmh, huu mkasa unafikirisha kidogo ,umefungwa kitambaa usoni na bado unajua matukio yote yalitokea muda gani? Tunamwombea apone upesi.
Amefungwa Kutambaa Walipoanza Kumuondosha Oysterbay Umesoma Vizuri huo mkasa..

Kipindi anachukuliwa Alichukuliwa kama Mtuhumiwa kupelekwa Polisi..
Na alikuwa anapiga story vizuri na washkaji mpaka walipokuja wale wababe asbuhi kumchukua..

Na Ukimsikia anasema kuwa taarifa nyingi alikuwa akizipata kutongana na mazungumzo yao
 
Mtoto mdogo, sema yawezekana alitukana sana mtu. Unajua hasira na madaraka haviendani. Unakua unaonekana mchanga tu.
Sema Martin bwana. Jamaa kajiweka kwenye story.🤣🤣🤣🤣 Sasa martin au bon ni wakupambana kuwapata kweli. Si wanadeal nao tu. 😂😂😂😂. Siasa. Gadamn.


ILA VIJANA HASWA TWITTER.
HESHIMA KITU CHA BURE.
UNAWEZA FANYA MOVEMENT ZAKO ILA UWE NA BUSARA.
TRUST ME. HATA UGOME KAMA UNA OBJECTIVE UNA TOA DUKUDUKU LAKO KWA UFASAHA NA HESHIMA. HATA ADUI YAKO LAZMA AKUUNGE MKONO AU AKULINDE. ILA UNAMCHOCHEA, NA MATUSI, NA KEJELI. 19-35 NDUGU VIJANA MTAKUFA SAAAAAAAAAANA.
 
Katavi Mbuga ya wanyama wakali na hapo Mto Iku ndipo makutanyiko ya wanyama.
SATIVA (Sijui kama ndio jina lake halisi) akubali kwamba Mungu ameamua kubakiza maisha yake "spare his life" kwa namna ya ajabu sana. Nitachambua kidogo kwa uelewa wangu kidogo.

Wauwaji ni wazi walipompiga risasi walijua wamempiga kichwani kulenga ubongo na kama kawaida ya risasi ya kichwa lazima aanguke na apoteze fahamu hata kama ingepiga sikio tuu, hivyo kuwahadaa watekaji wake kama mamemuua.
Na lazima watekaji walikuwa na kiwewe na haraka ya kukutwa na askari wa wanyamapori waliopo hapo Iku maana ndipo kambi yao ilipo, kufuatia mlio wa bunduki hivyo waliondoka upesi eneo hilo wakijua wameua tayari na hasa ukizingatia ni usiku.
Hawakuwa na muda wa kumtizama walijua tayari kazi imekwisha na ndio kupona kwa huyu jamaa. Ni wazi walikuwa na nia ya kumuua sababu walichagua kumpiga kichwani kutoka nyuma, maana kikanuni ukitaka kumuua mtu akiwa amekupa mgongo unampiga kichwa kutoka nyuma, kulenga ubongo wote wa mbele, wa kati na wa nyuma. Ni ukitaka kumuua mtu amekugeukia (anakuangalia) unapiga eneo la moyo ukiwa mbele. Ni nadra kumuua mtu kwa bunduki ndogo kama bastola kutoka nyuma kulenga moyo, risasi maranyingi hujisokota kwenye uti wa mgongo au kuishia kwenye mapafu hivyo kushindwa kufikia vital organs za kumfanya afe maramoja. Hawa ni weledi watu wenye mafunzo maana bila shaka walimfunga pingu nyuma "Handcuffed" na walitaka asiwaone, kumvalisha kitambaa "Blindfolded" na kumpiga risasi ya kichwa wakilenga kumwaga ubongo afe maramoja "Instantly killing".

Kuna mtu nilimsikia anasema, wenda kulikuwa na kujifanya amekufa "Play dead" kuwahadaa watekaji. Sio kweli, bunduki inatabia ya kuvuruga fahamu kwa mlio, nguvu hofu na mstuko mkubwa anaoupata victim hasa kwenye ukaribu "close range", hivyo ilikuwa lazima apoteze fahamu na aanguke hata kama risasi haijamfanyia damage kubwa.
Huyu Bwana ameponea bahati tuu, ni mambo yanatokea marachache sana haya. Kupona risasi ya kichwa kwa muktadha kama huu ni nadra sana bila kujali umakini wa muuwaji wake alikuwa makini kiasi gani. Ni wazi Muuaji alikuwa confident kuwa ameshamuua, na hivi sasa anajiuliza imekuwaje huyu bwana yupo hai hapati pia majibu.

Inasikitisha sana watanzania tunafanyiana namna hii, wangeweza kutumia namna nyingine ya kumtisha huyu kijana mdogo wenda labda alikuwa aggressive sana kushambulia, ila bado walikuwa na option ya namna nyingine ya kumuonya na kumtisha.

Ni sisi tuu kwa karne hii ndio bado tuna mbinu za kizamani za kudeal na watu wetu namna hii, ni mbinu za kipuuzi hazina nafasi kwenye karne hii kwa watu wetu.

This is definitely barbaric, uncouthed and presumptuous way of dealing with our people.
 
Back
Top Bottom