DOKEZO Alihukumiwa Miaka 30 jela kwa ubakaji miezi mitano iliyopita, leo tupo naye mtaani, hili limekaaje?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Rufaa hiyo.
Haya mambo yanasababisha watu kujichukulia sheria mkononi.
Mambo km haya ya kiwaki ndo yanasababisha watu kufanya mauaji..!!

Hapana, Kila Kesi inaamuliwa kulingana na Ushahidi uliopo katika Kesi husika.

Kumbuka: Siku hizi kuna visa vingi Sana vya uhasama katika Jamii, zipo baadhi ya Kesi ni kweli kabisa kwamba Watu wamekuwa wakibambikiwa Kesi kutokana na kuwepo kwa chuki binafsi kati ya mtu na mtu, uhasama ni mkubwa sana katika Jamii Siku hizi.
Hata wewe unaweza kuja kusingiziwa au Kubambikiwa tuhuma mbaya za ubakaji, Mauaji au hata kupewa Kesi ya robbery.

Usifikiri kwamba Watu wote kabisa waliopo jela kweli ni Wahalifu, wengine ni wahanga wa vitendo vya Kubambikiwa Kesi za uwongo.
 
Sahihi
 
Siku hz naona kama kesi ya ubakaji au kumpa mimba mwanafunz sio ngumu kihivyo,wengi naona wapo mtaan tu pamoja na kukutwa na hatia
 
Wanasemaga "No one is above the Law"...
Ila kiuhalisia, "The Law is like spider web, a weak will stuck but strong one will pass through"...

Si ajabu ukirejea utapewa kesi ya madai.
Usivunjike moyo, endea kupambania haki ya mwanao
 
Atakuwa katoka kwa rufaa. Kesi nyingi za ubakaji ngazi ya chini huhukumiwa kutokana na mihemko na waendesha mashataka wengi huwa wanakuwa sio weredi huwa wanaacha loopholes nyingi zinazofanya kesi ikienda mahakama za juu inatenguliwa. Na mahakimu huwa wanakuwa wamefungwa mikono juu ya hilo hivyo hta kma wataona loopholes huwa wanachukua hatua ya kukufunga miaka 30 jela. Ili utokee huko mbele
 
Mimi kama mwalimu Kuna mwanafunzi alishawahi kusimamia mbele ya walimu wenzangu ofisini na kudai kuwa nilimtongoza akanikataa nikaanza kuwa namuadhibu kwa uonevu ,ukweli nikuwa mtoto huyo toka aanze kidato Cha kwanza Hadi Cha nne siku nioiyomuadhibu ilikuwa ni siku ya kwanza
Hapana, Kila Kesi inaamuliwa kulingana na Ushahidi uliopo katika Kesi husika.

Kumbuka: Siku hizi kuna visa vingi Sana vya uhasama katika Jamii, zipo baadhi ya Kesi ni kweli kabisa kwamba Watu wamekuwa wakibambikiwa Kesi kutokana na kuwepo kwa chuki binafsi kati ya mtu na mtu, uhasama ni mkubwa sana katika Jamii Siku hizi.
Hata wewe unaweza kuja kusingiziwa au Kubambikiwa tuhuma mbaya za ubakaji, Mauaji au hata kupewa Kesi ya robbery.

Usifikiri kwamba Watu wote kabisa waliopo jela kweli ni Wahalifu, wengine ni wahanga wa vitendo vya Kubambikiwa Kesi za uwongo.
 
Mtoto wako kama kweli alibakwa ndiyo kabakwa huwezi toa maumivu yake kwa kudai haki ya mtuhumiwa kufungwa. Haki ipo mbinguni duniani ni Sheria.

Wala usiumie moyo Shukuru Mungu tulia kisasi ni cha Mungu. Ukiweka kisasi maana yake humuamini Mungu. Muache Mungu akupiganie haki yako. Fanya mambo mengine wanadamu hutawaweza Yesu alipambana nao akaishiwa kuzungukwa na kusulibiwa wewe ni nani!!???
 
H
Kuna Kijana mmoja tulimtuhumu kumbaka Mwanangu wa miaka minne tukapeleka malalamiko kwenye vyombo husika vya Kiserikali, Jamhuri ikafungua kesi ya ubakaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.

Tumeenda Mahakamani mimi na Mke wangu kwa zaidi ya Mwaka mmoja na nusu, ambapo tulikuwa tukiacha shughuli za kutupatia kipato na kwenda Mahakamani ili tuone haki ya mtoto wetu kama itapatikana.

Mungu sio Athumani tukiwa tunaelekea kukata tamaa kutokana na shauri kusikilizwa kwa muda mrefu, hukumu ilitolewa jambo ambalo lilitupa faraja kutokana na gharama za nauli na muda mwingi tulivyokuwa tumetumia kwenda Mahakamani.

Hukumu iliyotolewa ni kwamba mtuhumiwa alitiwa hatiani kuhusika na kosa alilokuwa anatuhumiwa nalo. Hukumu hiyo kwetu ilileta nuru, faraja na kutufuta machozi tukiamini haki imetendeka baada ya awali kuhisi kuna mazingira ya danadana ambayo yalifanya haki kucheleweshwa.

Mshtakiwa baada ya kutiwa hatiani alihukumiwa kwenda jela miaka 30, ambapo hadi sasa ni takribani miezi mitano imepita.

Katika hali ya kusikitisha nuru imetoweka baada ya kuanza kumuona mtuhumiwa mtaani akiishi kama raia huru, ni kwa mara kadhaa tumemuona mtuhumiwa huyo huku jamaa zake wakifurahia kutoka gerezani.

Mimi sio mtaalamu zaidi wa Sheria lakini napata ugumu kuelewa kama Mtu aliyehukumiwa anaweza kurejea mtaani bila kushinda rufaa au kutolewa kwa kuzingatia taratibu nyingine za kisheria ikiwemo msamaha wa Rais.

Nimeshindwa kuweka taarifa zote kwakina ikiwemo namba ya kesi yenyewe na jina la mtuhumiwa ili kuepuka uwezekano wa walioshiriki mchezo huo kinyume kutopata fursa ya kumrejesha mtuhumiwa gerezani kupoteza ushahidi lakini nikihakikishiwa usalama na haki kutendeka naweza kutoa ushirikiano.

Kutokana na kile nilichokieleza naomba kama kuna wataalamu wanisadie kuelewa ni kwa namna gani mtuhumiwa anaweza kuwa uraiani tofauti na taratibu nilizoeleza, lakini vipi natamani kufahamu aina ya wafungwa ambao unufaika na msamaha wa Rais.

Kwa mwenendo huo napata mashaka kama watuhumiwa tunaoambiwa wamehukumiwa kama wapo ndani inavyotakiwa uenda wengine wapo nje tena kinyume na Sheria, KWAKWELI NIMEOGOPA!
hebu tueleze ilikuwaje mlimtuhumu huyo kijana?
 
Siku hz naona kama kesi ya ubakaji au kumpa mimba mwanafunz sio ngumu kihivyo,wengi naona wapo mtaan tu pamoja na kukutwa na hatia
Wanasemaga "No one is above the Law"...
Ila kiuhalisia, "The Law is like spider web, a weak will stuck but strong one will pass through"...

Si ajabu ukirejea utapewa kesi ya madai.
Usivunjike moyo, endea kupambania haki ya mwanao
Yawezekana kabisa huyo Mtu ameshinda katika Kesi ya Rufaa.
Upo uwezekano mkubwa sana kwenye suala hili.
Mathalani, hata yule Mtu aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua kikatili mke wake na kisha kumchoma moto, upo uwezekano mkubwa sana huyo Mtu kuweza kushinda katika Kesi ya Rufaa endapo kama ataamua Kukata Rufaa Mahakama ya Rufani kwa sababu Ushahidi uliotumika katika kumtia hatiani una Utata mkubwa sana. Akikat Rufaa huyo Mtu uwezekano wa kushinda Rufaa yake upo mkubwa sana kwa zaidi ya 80%.

Kutokana na kuwepo kwa UTATA huu mkubwa sana katika Ripoti Mbili za Kitaalamu za Utabibu kuhusu Afya ya akili UA Mtuhumiwa, basi upo uwezekano mkubwa sana wa Mtu huyo kuachiwa huru endapo kama atakata Rufaa katika Mahakama ya Rufani. Jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufani watakuwa na kazi nyepesi Sana katika kutoa Uamuzi wa Kesi hii.

Huyo Daktari na huyo Jaji tayari wametengeneza na kusafisha njia ya ushindi kwa huyo Mfungwa.

Ripoti hizo zote Mbili za Uchunguzi wa Afya ya Akili ya huyo mtuhumiwa ambazo zimewasilishwa Mahakamani, zote kabisa ni BATILI hadi wakati huu.
Jaji huyo wakati wa Kuendesha Kesi hiyo, alipaswa kutoa AMRI ili huyo Mtuhumiwa achunguzwe Afya yake ya Akili chini ya Jopo lingine la Madaktari wengine mara tu ulipotokea utata huo wa Ushahidi wa Ripoti ya Daktari, lakini siyo kutumia ripoti yoyote ile ya Tabibu ambayo tayari imewasilishwa mbele yake.
Hoja ya Msingi hapa ni:-
Kama Daktari anakana kuitambua Ripoti iliyowasilishwa awali hapo Mahakamani na kudai kwamba siyo Ripoti Halali, Je, kuna UHAKIKA gani kwamba hiyo Ripoti ambayo aliyowasilisha yeye mwenyewe kwa mara ya Pili kuwa ni Halali????????

Hao Mawakili wa Utetezi wa huyo Mfungwa wanapaswa wakate Rufaa katika Mahakama ya Rufani, uwezekano wa Rufaa hiyo kushinda ni mkubwa sana hususani kutokana na hiyo Hoja nzito ya kuwepo kwa Mkanganyiko/Utata mkubwa sana katika Ushahidi uliowasilishwa Mahakamani ambao umetumika katika kumtia hatiani Mshitakiwa huyo.
Huyo Mshitakiwa/ Mfungwa atatoka jela.

All in all, This Case is not proved beyond the reasonable doubt!
 
Uchungu wenu huwezi mtu mwingine kuelewa, naomba Mungu afanye faraja na kumpa mtoto mwanzo mpya, kiroho na kimwili, maana historia hii huumiza maisha yaliyobakia.

Fuatilia mahakamani, ufahamu kilichojiri. Na msemee kwa Mwenyezi Mungu, ukitoa yooote ya rohoni kwake, hanaga kona kona, kwenye kutupigania.

Kikubwa, aponye nafsi ya BINTI
 
Kuna Kijana mmoja tulimtuhumu kumbaka Mwanangu wa miaka minne tukapeleka malalamiko kwenye vyombo husika vya Kiserikali, Jamhuri ikafungua kesi ya ubakaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.

Tumeenda Mahakamani mimi na Mke wangu kwa zaidi ya Mwaka mmoja na nusu, ambapo tulikuwa tukiacha shughuli za kutupatia kipato na kwenda Mahakamani ili tuone haki ya mtoto wetu kama itapatikana.

Mungu sio Athumani tukiwa tunaelekea kukata tamaa kutokana na shauri kusikilizwa kwa muda mrefu, hukumu ilitolewa jambo ambalo lilitupa faraja kutokana na gharama za nauli na muda mwingi tulivyokuwa tumetumia kwenda Mahakamani.

Hukumu iliyotolewa ni kwamba mtuhumiwa alitiwa hatiani kuhusika na kosa alilokuwa anatuhumiwa nalo. Hukumu hiyo kwetu ilileta nuru, faraja na kutufuta machozi tukiamini haki imetendeka baada ya awali kuhisi kuna mazingira ya danadana ambayo yalifanya haki kucheleweshwa.

Mshtakiwa baada ya kutiwa hatiani alihukumiwa kwenda jela miaka 30, ambapo hadi sasa ni takribani miezi mitano imepita.

Katika hali ya kusikitisha nuru imetoweka baada ya kuanza kumuona mtuhumiwa mtaani akiishi kama raia huru, ni kwa mara kadhaa tumemuona mtuhumiwa huyo huku jamaa zake wakifurahia kutoka gerezani.

Mimi sio mtaalamu zaidi wa Sheria lakini napata ugumu kuelewa kama Mtu aliyehukumiwa anaweza kurejea mtaani bila kushinda rufaa au kutolewa kwa kuzingatia taratibu nyingine za kisheria ikiwemo msamaha wa Rais.

Nimeshindwa kuweka taarifa zote kwakina ikiwemo namba ya kesi yenyewe na jina la mtuhumiwa ili kuepuka uwezekano wa walioshiriki mchezo huo kinyume kutopata fursa ya kumrejesha mtuhumiwa gerezani kupoteza ushahidi lakini nikihakikishiwa usalama na haki kutendeka naweza kutoa ushirikiano.

Kutokana na kile nilichokieleza naomba kama kuna wataalamu wanisadie kuelewa ni kwa namna gani mtuhumiwa anaweza kuwa uraiani tofauti na taratibu nilizoeleza, lakini vipi natamani kufahamu aina ya wafungwa ambao unufaika na msamaha wa Rais.

Kwa mwenendo huo napata mashaka kama watuhumiwa tunaoambiwa wamehukumiwa kama wapo ndani inavyotakiwa uenda wengine wapo nje tena kinyume na Sheria, KWAKWELI NIMEOGOPA!
Mcheki Waziri Dorothy Gwajima atakusaidia. Namba yake 0765 345777
 
Mambo ya rufaa, nikiwa mle ndani nilishudia wafungwa wakiachiwa,kesi ya kulawiti,noti bandia,kumpa mimba mwanafunzi,kingne noti ikitembea utatoka tu.
 
Kama unauhakika hakukata rufaa jaribu kwenda gereza husika alofungwa jaribu kuulizia inawezekana ametoloka piaa
Atoroke gerezan halaf aishi mtaani kwa uhuru kbs ivi unawachukuliaje askari wajela jela ? 😀
 
Back
Top Bottom