Yawezekana kabisa huyo Mtu ameshinda katika Kesi ya Rufaa.
Upo uwezekano mkubwa sana kwenye suala hili.
Mathalani, hata yule Mtu aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua kikatili mke wake na kisha kumchoma moto, upo uwezekano mkubwa sana huyo Mtu kuweza kushinda katika Kesi ya Rufaa endapo kama ataamua Kukata Rufaa Mahakama ya Rufani kwa sababu Ushahidi uliotumika katika kumtia hatiani una Utata mkubwa sana. Akikat Rufaa huyo Mtu uwezekano wa kushinda Rufaa yake upo mkubwa sana kwa zaidi ya 80%.
Kutokana na kuwepo kwa UTATA huu mkubwa sana katika Ripoti Mbili za Kitaalamu za Utabibu kuhusu Afya ya akili UA Mtuhumiwa, basi upo uwezekano mkubwa sana wa Mtu huyo kuachiwa huru endapo kama atakata Rufaa katika Mahakama ya Rufani. Jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufani watakuwa na kazi nyepesi Sana katika kutoa Uamuzi wa Kesi hii.
Huyo Daktari na huyo Jaji tayari wametengeneza na kusafisha njia ya ushindi kwa huyo Mfungwa.
Ripoti hizo zote Mbili za Uchunguzi wa Afya ya Akili ya huyo mtuhumiwa ambazo zimewasilishwa Mahakamani, zote kabisa ni BATILI hadi wakati huu.
Jaji huyo wakati wa Kuendesha Kesi hiyo, alipaswa kutoa AMRI ili huyo Mtuhumiwa achunguzwe Afya yake ya Akili chini ya Jopo lingine la Madaktari wengine mara tu ulipotokea utata huo wa Ushahidi wa Ripoti ya Daktari, lakini siyo kutumia ripoti yoyote ile ya Tabibu ambayo tayari imewasilishwa mbele yake.
Hoja ya Msingi hapa ni:-
Kama Daktari anakana kuitambua Ripoti iliyowasilishwa awali hapo Mahakamani na kudai kwamba siyo Ripoti Halali, Je, kuna UHAKIKA gani kwamba hiyo Ripoti ambayo aliyowasilisha yeye mwenyewe kwa mara ya Pili kuwa ni Halali????????
Hao Mawakili wa Utetezi wa huyo Mfungwa wanapaswa wakate Rufaa katika Mahakama ya Rufani, uwezekano wa Rufaa hiyo kushinda ni mkubwa sana hususani kutokana na hiyo Hoja nzito ya kuwepo kwa Mkanganyiko/Utata mkubwa sana katika Ushahidi uliowasilishwa Mahakamani ambao umetumika katika kumtia hatiani Mshitakiwa huyo.
Huyo Mshitakiwa/ Mfungwa atatoka jela.
All in all, This Case is not proved beyond the reasonable doubt!