DOKEZO Alihukumiwa Miaka 30 jela kwa ubakaji miezi mitano iliyopita, leo tupo naye mtaani, hili limekaaje?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tu
Hachana naye ...........wewe fanya mambo yako.........ila mshitakie mungu.......kama kuna yeyote aliyekanyaga haki yako nakuthibitishia atoboi...........yaani hata usisononeke kabisaaa ipo saa ya ushindi kwa mungu ............
Tuzingatie na kiswahili tunapoandika pia.
Hachana
Atoboi
 
Kuna Kijana mmoja tulimtuhumu kumbaka Mwanangu wa miaka minne tukapeleka malalamiko kwenye vyombo husika vya Kiserikali, Jamhuri ikafungua kesi ya ubakaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.

Tumeenda Mahakamani mimi na Mke wangu kwa zaidi ya Mwaka mmoja na nusu, ambapo tulikuwa tukiacha shughuli za kutupatia kipato na kwenda Mahakamani ili tuone haki ya mtoto wetu kama itapatikana.

Mungu sio Athumani tukiwa tunaelekea kukata tamaa kutokana na shauri kusikilizwa kwa muda mrefu, hukumu ilitolewa jambo ambalo lilitupa faraja kutokana na gharama za nauli na muda mwingi tulivyokuwa tumetumia kwenda Mahakamani.

Hukumu iliyotolewa ni kwamba mtuhumiwa alitiwa hatiani kuhusika na kosa alilokuwa anatuhumiwa nalo. Hukumu hiyo kwetu ilileta nuru, faraja na kutufuta machozi tukiamini haki imetendeka baada ya awali kuhisi kuna mazingira ya danadana ambayo yalifanya haki kucheleweshwa.

Mshtakiwa baada ya kutiwa hatiani alihukumiwa kwenda jela miaka 30, ambapo hadi sasa ni takribani miezi mitano imepita.

Katika hali ya kusikitisha nuru imetoweka baada ya kuanza kumuona mtuhumiwa mtaani akiishi kama raia huru, ni kwa mara kadhaa tumemuona mtuhumiwa huyo huku jamaa zake wakifurahia kutoka gerezani.

Mimi sio mtaalamu zaidi wa Sheria lakini napata ugumu kuelewa kama Mtu aliyehukumiwa anaweza kurejea mtaani bila kushinda rufaa au kutolewa kwa kuzingatia taratibu nyingine za kisheria ikiwemo msamaha wa Rais.

Nimeshindwa kuweka taarifa zote kwakina ikiwemo namba ya kesi yenyewe na jina la mtuhumiwa ili kuepuka uwezekano wa walioshiriki mchezo huo kinyume kutopata fursa ya kumrejesha mtuhumiwa gerezani kupoteza ushahidi lakini nikihakikishiwa usalama na haki kutendeka naweza kutoa ushirikiano.

Kutokana na kile nilichokieleza naomba kama kuna wataalamu wanisadie kuelewa ni kwa namna gani mtuhumiwa anaweza kuwa uraiani tofauti na taratibu nilizoeleza, lakini vipi natamani kufahamu aina ya wafungwa ambao unufaika na msamaha wa Rais.

Kwa mwenendo huo napata mashaka kama watuhumiwa tunaoambiwa wamehukumiwa kama wapo ndani inavyotakiwa uenda wengine wapo nje tena kinyume na Sheria, KWAKWELI NIMEOGOPA!
Mkuu ni mahakama gani alihukumiwa ili nikusaidie kitu
 
Daah pole sana kaka mtoto wa miaka mi4 kubakwa na mtu mzma alafu kiboya tu anatamba mtaani
 
Tutamkumbuka MAGUFULI!!
 
Nenda huko mahakamani kahoji,Huenda alikata rufani,na rufani kama kashindwa hawaitwi Tena mashahidi,Hakimu au jaji hupitia maelezo ya pande mbili na kuyafangia mapitio na kuyatolea maamuzi.Hivyo Huenda jamaa alishinda huko mkuu.
Ukishindwa rufani,huwezi tena kuanzisha kesi upya?
 
Kuna Kijana mmoja tulimtuhumu kumbaka Mwanangu wa miaka minne tukapeleka malalamiko kwenye vyombo husika vya Kiserikali, Jamhuri ikafungua kesi ya ubakaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.

Tumeenda Mahakamani mimi na Mke wangu kwa zaidi ya Mwaka mmoja na nusu, ambapo tulikuwa tukiacha shughuli za kutupatia kipato na kwenda Mahakamani ili tuone haki ya mtoto wetu kama itapatikana.

Mungu sio Athumani tukiwa tunaelekea kukata tamaa kutokana na shauri kusikilizwa kwa muda mrefu, hukumu ilitolewa jambo ambalo lilitupa faraja kutokana na gharama za nauli na muda mwingi tulivyokuwa tumetumia kwenda Mahakamani.

Hukumu iliyotolewa ni kwamba mtuhumiwa alitiwa hatiani kuhusika na kosa alilokuwa anatuhumiwa nalo. Hukumu hiyo kwetu ilileta nuru, faraja na kutufuta machozi tukiamini haki imetendeka baada ya awali kuhisi kuna mazingira ya danadana ambayo yalifanya haki kucheleweshwa.

Mshtakiwa baada ya kutiwa hatiani alihukumiwa kwenda jela miaka 30, ambapo hadi sasa ni takribani miezi mitano imepita.

Katika hali ya kusikitisha nuru imetoweka baada ya kuanza kumuona mtuhumiwa mtaani akiishi kama raia huru, ni kwa mara kadhaa tumemuona mtuhumiwa huyo huku jamaa zake wakifurahia kutoka gerezani.

Mimi sio mtaalamu zaidi wa Sheria lakini napata ugumu kuelewa kama Mtu aliyehukumiwa anaweza kurejea mtaani bila kushinda rufaa au kutolewa kwa kuzingatia taratibu nyingine za kisheria ikiwemo msamaha wa Rais.

Nimeshindwa kuweka taarifa zote kwakina ikiwemo namba ya kesi yenyewe na jina la mtuhumiwa ili kuepuka uwezekano wa walioshiriki mchezo huo kinyume kutopata fursa ya kumrejesha mtuhumiwa gerezani kupoteza ushahidi lakini nikihakikishiwa usalama na haki kutendeka naweza kutoa ushirikiano.

Kutokana na kile nilichokieleza naomba kama kuna wataalamu wanisadie kuelewa ni kwa namna gani mtuhumiwa anaweza kuwa uraiani tofauti na taratibu nilizoeleza, lakini vipi natamani kufahamu aina ya wafungwa ambao unufaika na msamaha wa Rais.

Kwa mwenendo huo napata mashaka kama watuhumiwa tunaoambiwa wamehukumiwa kama wapo ndani inavyotakiwa uenda wengine wapo nje tena kinyume na Sheria, KWAKWELI NIMEOGOPA!
Ndioo ukome sio kila tuhuma n za kweli mkuu lazima zithinitishwe na mahakama na kujiridhisha wakati anapigwa 30 ukashangilia MWENZIO KAJA na rufaaaa katokaa

Na akitoka sio lazima uambiwe unaweza kutana nae bar.....
 
Mi SHEMEJI Yangu walimtuhumu nilikuwa Nje miaka ya nyumaaaaa

Yule falaa akajipanga kweli niliporudi tukaichungulia kesi nikamwona MWANASHERIA MMOJA tukakata rufaaa

Alikaa ndani miezi 4. Nafika nkanza KWENDA bar za jirani yao watu wanashangilia YAAN jamaa na pesa zake kashindwa kutoka

Mouuzi MMOJA akaja na jamaa wawili akasambaza beer mbaya akaanza kutangaza yule pumbavu atoki amepigwa miaka 4

Aisee HAPO napambana kukutania na NDUGU WA kila aina.......tukakata rufaa hahaha jamaa katika akaenda nyumban akaoga

Alipomaliza tukakusanyana kama NDUGU 20. Bar WAKAINGIA 10 wakagiza pombe za kutosha na mbavu na miguu ya mbuzi ya kutosha

Wakashuka wengine nkabaki na jamaa

NYama zimeivaa wanaume tukaingiza timu hamad tunaingiza wale wahuni WALIOKUWA wakimzungumzia WANAINGIA haha wakaona kile kikosi awakukaa nusu saa wakaondoka

Mpaka kesho awakurudi tenaaaaa

SO mkuu sio kila anaehukumiwa anakosa wengine wanakosa tu wanasheria waziri kuwasaidia
 
Inawezekana alikata rufaa na pengine republic pia ilijichanganya sehemu flani.. basi akatoka.
Nb.
Kisheria mtu anaweza kuua Kila mtu anaona na Bado jezi akashinda akiwa na mwanasheria anayejua vichochoro
Kabisa mkuuuuu

Na kingineee unaona YULEE dk WA muhimbili aliepeleka ripoti mbili kesi ya muuwaji

Moja ANASEMA jamaa chizi akasikia jamaa wamempeleka SEHEMU nyingine kakurwa mzima akaitwa KUTETEA ripoti yake kuonyesha ya pili

So sio anaetuhumiwa KUBAKWA n kweli mbakaji

Imagine huyu dk angekutana na kesi kama hii HATA kama hajabakwa si ANAPOKEA mpunga wanakunyoosha mahakama
 
Mwenye mtoto mwenyewe huna uhakika kama mtoto wako alibakwa ndiyo maana unasema mulimtuhumu. Sasa unataka mtu apigwe mvua 30 kwa tuhuma tu bila ya ushahidi wenye kueleweka?
 
Alimbaka kweli ?hii skendo kama imetokea manzese nyumba ipo karibu na barabara kubwa uyo kijana alikuwa anafanya kazi ya kusambaza vinywaji? Ktik duka lililopo ktk iyo nyumba? Kama ndio je ni mtot alibakwa au alikuwa anachezewa sehem zake za siri? Maana kuna kisa nilikisikia eneo ilo sasa sijui ndo hili suala ama la, kama ndio jamaa si alipewa dhamana akakimbia?
 
Inawezekana alikata rufaa na pengine republic pia ilijichanganya sehemu flani.. basi akatoka.
Nb.
Kisheria mtu anaweza kuua Kila mtu anaona na Bado jezi akashinda akiwa na mwanasheria anayejua vichochoro
Yaani bila mlalamikaji kujua!!,hadi mtuhumiwa aonekane mtaani,??,,kiufupi hapo yaonekana rushwa ilitembea si bure.
 
Yawezekana kabisa huyo Mtu ameshinda katika Kesi ya Rufaa.
Upo uwezekano mkubwa sana kwenye suala hili.
Mathalani, hata yule Mtu aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua kikatili mke wake na kisha kumchoma moto, upo uwezekano mkubwa sana huyo Mtu kuweza kushinda katika Kesi ya Rufaa endapo kama ataamua Kukata Rufaa Mahakama ya Rufani kwa sababu Ushahidi uliotumika katika kumtia hatiani una Utata mkubwa sana. Akikat Rufaa huyo Mtu uwezekano wa kushinda Rufaa yake upo mkubwa sana kwa zaidi ya 80%.

Kutokana na kuwepo kwa UTATA huu mkubwa sana katika Ripoti Mbili za Kitaalamu za Utabibu kuhusu Afya ya akili UA Mtuhumiwa, basi upo uwezekano mkubwa sana wa Mtu huyo kuachiwa huru endapo kama atakata Rufaa katika Mahakama ya Rufani. Jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufani watakuwa na kazi nyepesi Sana katika kutoa Uamuzi wa Kesi hii.

Huyo Daktari na huyo Jaji tayari wametengeneza na kusafisha njia ya ushindi kwa huyo Mfungwa.

Ripoti hizo zote Mbili za Uchunguzi wa Afya ya Akili ya huyo mtuhumiwa ambazo zimewasilishwa Mahakamani, zote kabisa ni BATILI hadi wakati huu.
Jaji huyo wakati wa Kuendesha Kesi hiyo, alipaswa kutoa AMRI ili huyo Mtuhumiwa achunguzwe Afya yake ya Akili chini ya Jopo lingine la Madaktari wengine mara tu ulipotokea utata huo wa Ushahidi wa Ripoti ya Daktari, lakini siyo kutumia ripoti yoyote ile ya Tabibu ambayo tayari imewasilishwa mbele yake.
Hoja ya Msingi hapa ni:-
Kama Daktari anakana kuitambua Ripoti iliyowasilishwa awali hapo Mahakamani na kudai kwamba siyo Ripoti Halali, Je, kuna UHAKIKA gani kwamba hiyo Ripoti ambayo aliyowasilisha yeye mwenyewe kwa mara ya Pili kuwa ni Halali????????

Hao Mawakili wa Utetezi wa huyo Mfungwa wanapaswa wakate Rufaa katika Mahakama ya Rufani, uwezekano wa Rufaa hiyo kushinda ni mkubwa sana hususani kutokana na hiyo Hoja nzito ya kuwepo kwa Mkanganyiko/Utata mkubwa sana katika Ushahidi uliowasilishwa Mahakamani ambao umetumika katika kumtia hatiani Mshitakiwa huyo.
Huyo Mshitakiwa/ Mfungwa atatoka jela.

All in all, This Case is not proved beyond the reasonable doubt!
Kesi ikifikia kwenye rufaa,na mshitakiwa kushinda,mshtaki,hawezi kufungua kesi upya?
 
Back
Top Bottom