Alijidai fundi jikoni, akaaibika mbele ya wageni wake. Umewahi pika chakula kibaya?

Alijidai fundi jikoni, akaaibika mbele ya wageni wake. Umewahi pika chakula kibaya?

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Siku moja shangazi yetu alituambia kuwa atakuwa na wageni wa muhimu wanakuja kumtembelea nyumbani ivyo tuweke mazingira sawa kwenye kila kitu kusiwe na dosari kama mjuavyo nyumba ikiwa na watu wengine inakuwa na hekaheka inahitaji kurekebishwa mpangilio.

Basi tukafanya hivyo huku yeye akienda sokoni kununua vitu vya kuwakarimu wageni wake kwa ajili ya kuja kupika ili wageni wake waondoke wakiwa wameshiba na kurika sana.

Kikawaida shangazi hakuwa anaingia jikoni kupika mara kwa mara wapishi wa ile familia tulikuwa sisi watoto ndio tulikuwa tunapika kila siku na hata kue na tukio gani ila hiyo siku akasema ataika yeye tusije pika vitu vya ajabu akapata aibu.

Akatuka kazi ya kuandaa juisi na kachumbari pamoja na kukata matunda tu ila vingine vyote yeye akasimamia shoo, picha linaanza akaniita, hebu nisaidie kunitazamia hili pilau, naona mtu anavuja jasho kama katoka kukimbia.

Kufunua hivi, pilau lipo kama bokoboko na sehemu zingine lina kiini, mboga chumvi kama gari la Uvinza limepata ajali kwenye sufuria, wai wa maji nao uko kama makande kifupi kila alichogusa kilikuwa kibaya. Ndizi sijui hata nisemeje kama zimelowekwa, wakati huo wageni wako ndani wanasubiri chakula.

Akaingia chumbani akafunga mlango, nikawaita ndugu wengine tukajadili tufanye nini, tukaamua kupika wali wa maji kwa haraka na maharage yalikuwa yapo hayajaungwa tukayaunga tukawapa wageni, ila yeye akasingizia kaumwa tumbo la ghafla na akatoka tu kidogo kuwaanga wageni wake ila aibu aliipata.
 
Ndio mana mnaambiwa wafundisheni watoto wenu kupika wakiwa wadogo kuepusha aibu kama hizi
 
😹😹😹 Na huyo shangazi yako ndio mimi..!!
Kuna siku nilitoa kitu hiko mpaka mbwa waligoma kula aiseee..!! 😹
 
Back
Top Bottom