Alijifanya kidume, nimemlaza lock up

Alijifanya kidume, nimemlaza lock up

Usitake kutuaminisha,
Ulikua na mahusiano na kichaa akupige bila sababu.

Hapo mdomo bila shaka umeponza KICHWA.
 
Haya mambo ya wapendanao huwa sitii neno sana. Unashupaza shingo kuongea kesho unawakuta watu pamoja na wanajifunika shuka Moja.

Ila huyo mwenzetu kapitiliza, hizi Karne watu hawapigani mateke, makofi na ngumi. Mkishindwana mnaagana kiroho safi Kila mtu anaendelea na mambo yake.
Hafu baada ya muda atakuja na Uzi wa kumuomba msamaha
 
Alijifanya kidume, anajua kupigana. Kanipiga kofi na teke la mbavu bila sababu za msingi, nikasema hunijui wewe kama na mapenzi yaishe tu. Nikaenda kumchukulia RB, polisi wamemkamata wamemlaza lock up.

Sasa hivi eti ndio akili zinamkaa sawa anajifanya kunitumia wajumbe wamuombee msamaha.
Lock umeona ni sehemu hatari sanaaaaaa?
 
Yani wewe ni kamwanamke kafupi alafu kabishi..huwa hampendi kushindwa na itakuwa ulijaribu kupigana ndo mana ukapigwa namna hiyo..sasa sijui mwamba ulimbinya mbupu maana sio kwa kumaind huko..japo na yeye amezingua sana angalieni..litaanguka jitu sikumoja sisi yetu macho.
 
Nikaenda kumchukulia RB, polisi wamemkamata wamemlaza lock up.
Sio maisha hayo kabisa, Na hupaswi kujisia kwa ulichofanya, Na hakika hakuna mtu mwenye akili Timamu atakusifia kwa huo uoamuzi wa hovyo uliochukua.
==
Msome neno kwa neno mjumbe hapa chini👇 Perry jitafakari na chukua hatua stahiki. Tambua maisha ni mafupi hatupaswi kuishi kwa visasi namna hiyo.
Nilioyaona kule ndani ya hizo siku tano naweza kusema hivi kama mpenzi wako muwe mmegombana hata kufikia kupigana na hali yoyote ile akifikia kukupeleka ndani nakushauri uachane nae. Mie kwa uzoefu wangu wa kule hata mtu anifanyie visa gani siwezi kumpeleka ndani nitakaa nae nitamwonya

Kule ni sawa na mtu kukupeleka Jehanamu. Sasa kama mpenzi wako au mkeo anakupeleka Jehanamu huyo hafai kabisa
 
Alijifanya kidume, anajua kupigana. Kanipiga kofi na teke la mbavu bila sababu za msingi, nikasema hunijui wewe kama na mapenzi yaishe tu. Nikaenda kumchukulia RB, polisi wamemkamata wamemlaza lock up.

Sasa hivi eti ndio akili zinamkaa sawa anajifanya kunitumia wajumbe wamuombee msamaha.
Bora mamaako angekua ng'ombe tukanywa maziwa yale ulionyonyeshwa bure..unamueka mtoto wa mwenzio lock up alafu unaleta huku jukwaani..
 
Wanajifunika shuka moja huku wakiwa wanakusema mkuu. Mapenzi Ni mchezo wa hovyo sana
Nilikuwa namsikia kamanda mmoja redioni akisema kesi za namna hio ni nyingi ila huwa hawaamuliagi mtu na mpenziwe wakitibuana huwa wanasikiliza tu na kuwatimua🤣🤣🤣
 
Ndani ni kubaya kweli. Nilijiona mimi ni baunsa ila nikaingia nikakutana na mtu mfupi zaidi yangu na ana mwili zaidi yangu. Hata hivyo mambo mengi ya rumande yanakuzwa washkaji walikuwa peace.

Anyway, hakuna namna utampiga mwanamke kisha akakupeleka rumande halafu nikakuonea huruma.
Naimani ulimpa iphone 13 ndio akakupeleka ndani kama response
 
Nimewahi kukaa ndani nikiwa Chuo baada ya kumtukana abiria kwenye daladala kumbe alikuwa polisi mpelelezi wale wasiovaa sare.

Jamaa aliniweka Kawe Polisi kama kunikomoa kwa siku tano. Nilioyaona kule ndani ya hizo siku tano naweza kusema hivi kama mpenzi wako muwe mmegombana hata kufikia kupigana na hali yoyote ile akifikia kukupeleka ndani nakushauri uachane nae. Mie kwa uzoefu wangu wa kule hata mtu anifanyie visa gani siwezi kumpeleka ndani nitakaa nae nitamwonya

Kule ni sawa na mtu kukupeleka Jehanamu. Sasa kama mpenzi wako au mkeo anakupeleka Jehanamu huyo hafai kabisa

Siku naoa nilimwambia mke wangu siku ukinipeleka ndani ujue ndio mwisho wa ndoa yetu na nikitoka ni bora uwe umeshatangulia kwenu mapema sana
jehanamu kivipi mkuu hebu fafanua🤣
 
Hufai kuwa mke na wala yule sio kichaa kama alikutongoza na ukamuelewa maana yake anaakili timamu kuna sehem umezingua arafu unarahisisha RB haito kusaidia kitu at the end of the day atatoka tu
Huyu mwanamke mshamba tu. Anajisifia ujinga namna hii
 
Back
Top Bottom