Baada ya Miaka 4 ya purukushani na aliyewahi kuwa Mke wangu Leo nimeamua kwa hiari yangu kuweka silaha chini na focus yangu iwe kwenye kuboresha maisha yangu na kizazi changu, nimeamua kumtumia ujumbe hapo chini.
"Ulinambia wazi kwa kinywa chako kuwa nimeshindwa kulea watoto, hata ukasema ‘kila mtu anaona wewe umeshindwa kulea watoto’. Niliumia kimya kimya kwa kauli zako za kifedhuli, lakini kwa sababu watoto ni wa damu yangu, niliwacha kwako kwa matumaini kuwa utawalea kwa moyo wa upendo na kuwapa hayo maisha bora ambayo kwangu ulisema hayapo, shule za gharama n.k
Leo hii unanirudia kudai matunzo na mali zangu na hiyo bado siyo dharau ya kwanza.
Wakati tulipoachana ulisema huna haja ya chochote na unathamini mchango wangu. Ulikataa hata nyumba kwa hiari yako mwenyewe. Leo, baada ya miaka minne, unakuja na madai kama vile hayo maneno hayajawahi kusemwa katika kinywa chako. Sijashindwa, ila hisia zinaniambia naumiza watoto, watu wa karibu yako hawawezi kukushauri vitu vya msingi coz wanaona namna ninavyojitoa Kwa watoto wangu 'WANACHUKIZWA' wanatafuta namna ya kuumiza watoto, na mtu pekee anaeweza kuwasaidia hilo lengo ni wewe, UMEJAZWA UJINGA, umejaa kwenye mfumo wao.
Lakini sasa, sitaki tena kuishi kwa mashindano ya roho mbaya na kinyongo.
Chukua kila kitu. Sina haja ya mali ya kuandamana na kelele na unafiki. Nitajitahidi kwa hali na mali kutoa msaada kwa watoto wetu, si kwa sababu wewe unataka nifanye hivyo, bali kwa sababu ni wajibu wangu kama mzazi na sio vinginevyo.
Naanza upya, na moyo mweupe. Ulichokikataa kwa heshima, usije kukidai tena kwa tamaa. Ubarikiwe na dhamira yako."
Unasema ulikwenda wa Shehe na alikwambia huna haki katika ile nyumba ki'ilmu ya dini yetu ya Kiislam, umeamua kuwa mgalatia na kuishi bila kufata misingi ya dini, sawa
Njoo Tarehe 10 July 2025 Mahakamani uchukue unachohitaji