Alikiba kawakataza Kings Music kufanya interviews Wasafi Media?

Alikiba kawakataza Kings Music kufanya interviews Wasafi Media?

Squidward

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2014
Posts
7,828
Reaction score
9,546
Habari zenu wananzengo,

Guys hili bifu la mondi na kiba bado lipo pale pale, wale wanaosema hawa jamaa hawana mabifu basi wanajidanganya tu.. Jiulize ushawahi kuwaona vijana wa Kings music wakitambulisha ngoma zao mpya wasafi media? ila cha ajabu wasafi tv na radio wanapiga ngoma za hao kings kila siku hadi ngoma zao mpya zinachezwa bila hata official interviews/release kwa wasafi. Sawa una bifu na mondi hata uzao wako usijihusishe na chochote kinachohusiana na mondi hata kama kina faida kwao kibiashara? Kumbe bifu binafsi na biashara huwa vinakwenda pamoja? Alikiba badilika biashara haiendi hivyo hata kidogo waache vijana wako wawe huru kwenda popote as long as hawavunji/hawavunjiwi heshima kwako na kwa wengine. Big up kwa Wasafi Media, ile ni media ambayo ipo huru Tanzania haijalishi uwe na bifu na mmiliki wake au la wewe ngoma zako zitapewa airtime everyday labda wewe mwenyewe uwaambie waache kupiga. Compared to clouds, East Africa radio, efm, wote tunajua hizo media ukikorofishana na presenter au hata mfagia ofisi kwa mambo yenu binafsi basi Department zote haijalishi tv au radio watasitisha kucheza ngoma zako mara moja! VERY UNPROFESSIONAL. Entertainment media za kibongo zijifunze kwa wakenya wanafanyaje hizi kazi, wenzetu hawaendeshi media zao kwa mihemko.

maxresdefault.jpg
 
Binafsi mimi sio mshabiki sana wa nyimbo za hawa wawili ila kwa nilichojifunza kuhusu hii inayosemekana bifu,ni kwamba ilisaidia sana kumuinua Ali kiba hata kama tayari alishakuwa mkubwa,kingine inaonekana Ali ananufaika zaidi na hapendi hii kitu iishe
 
basi hii bifu iishie kwake tu na sio kwa vijana wake wasiohusika na chochote. asiende mbali Aangalie Kenya tu pale biashara ya muziki inakwendaje acheki na Nigeria kwa lile kundi la Mavins la kina donjazzy...
 
Huyu jamaa namkubali lakini huwa ana mambo ya kiboya sana.

Kila akiwa kwenye baadhi ya redio ana kazi ya kulalamikia eti wengine wananunua viewers. Wakati ye mwenyewe hajui kupromote kazi zake.

naamini huu uzi meneja wake atausoma na watajitafakari upya. Kiba ana mambo ya kizamani tena ya zama za mawe za kati. wabadilike kwa kweli waache utoto
 
basi hii bifu iishie kwake tu na sio kwa vijana wake wasiohusika na chochote. asiende mbali Aangalie Kenya tu pale biashara ya muziki inakwendaje acheki na Nigeria kwa lile kundi la Mavins la kina donjazzy...
Huko Marvin record umeenda mbali mkuu wale wanigeria biashara ya muziki wanaijua vilivyo ni kazi rahisi kwa kcee wa lebo ya five star music kuipa promo nyimbo ya Davido wa lebo ya DMW,au tiwa Savage kuipa promo nyimbo ya Wizkid,huku unafiki mwingi kwa wasanii na biashara hawaijui kabisa
 
kweli kabisa mkuu. Kwa Tanzania nathubutu kusema kwamba Wasafi media & record label pekee ndo wametuprove wrong kuwa bifu ni bifu na biashara ni biashara so havifuatani pamoja. Kwa jinsi navyomuona Diamond yupo tayari kuruhusu Kings music wapige shoo wasafi festival na kulipwa vizuri tu kama wasanii wengine ila Alikiba hiko kitu hataki sasa hiyo ni akili au matope? yule jamaa akili hana, akae chini na professionals wamfunze biashara inakwendaje.
 
Back
Top Bottom