Alikiba kuilaani rasmi bongo flava September

AdvocateFi

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
11,492
Reaction score
5,047
Yule Mwana Dar es Salaam, Kingkiba, Balozi wa wanyama, Msanii pekee aliyetoboa Kimataifa bila Collabo, Kiboko ya Wizkid, Fundi na Master wa game ya mziki wa Africa "Alikiba" ambaye kwa sasa ndiyo msanii anayeongoza Kulipwa fedha nyingi kwenye Show kuliko msanii yeyote Yule East Africa.

Mwezi September kwenda kushusha Laana 5 takatifu kupitia nyimbo mpya atakazoenda kuachia 2 zake binafsi na 3 alizoshirikishwa na wasanii wa ndani na nje ya nchi,

Wajuzi na watafiti wa duru za Burudani Africa Mashariki, Wanabashiri kuwa huenda ikawa ndiyo mwanzo na mwisho wa kufunga rasmi nyufa za mziki wa bongoflava ambazo zimekuwepo kwa miaka mingi, Ambapo kwa sasa wasanii wengi wamevamia game na kukop mziki wa Nigeria bila kuzingatia misingi ya mziki wetu wa asili, Mbaya zaidi na wengine kufika mbali kutumia kiki za kihafidhina na kununua tuzo ili kupush mziki wao unaosuasua.

Note:
Kila atakayesikia project hizo mpya za KingKiba, Hakuna hata mmoja atakayethubutu kumaliza luku yake kusikiliza nyimbo zenye unaijeria, kiki na promo za kipuuzi.

Stay tuned, #KAJIANDAE #AJE_REMIX #NISAMEHE #TUMESHINDIKANA #NIA_YAO
 
Povu vp mlisema 25 mwezi w 8. Kimyaaaaa
 
Una uhakika na hio story?? Umeiskia wap?? Alikiba na wizkid unawalinganisha vp??
 
Povu vp mlisema 25 mwezi w 8. Kimyaaaaa

Ni kweli Augustb 25 mfalme alikuwa aachie laana mpya, ingekuwa Exclusively kwa mara ya kwanza Mtvbase Africa ila ratiba zikaingiliana na session za kupromote tuzo za MTvmama, so ratiba tumeipeleka mbele had September mpaka baada ya mtv kumaliza mission yao ya mtvmama na kutangaza host city na nominations.
 
Ahahaaaaaah...
Sawa..!
Mpango wake wa kuisimamisha Dunia umeishia wapi tena..?
Maana ilikua aisimamishe jana..!
Taratibu asije akaisimamisha Dunia September Mosi,akaharibu shughuli ya kitaifa ya UKUTA..!!!
 
Ahahaaaaaah...
Sawa..!
Mpango wake wa kuisimamisha Dunia umeishia wapi tena..?
Maana ilikua aisimamishe jana..!
Taratibu asije akaisimamisha Dunia September Mosi,akaharibu shughuli ya kitaifa ya UKUTA..!!!

Hahaha Mkuu swali lako nimeshalijibu hapo juu, Ni baada ya UKUTA itakuwa.
 
Nimependa hapo unapomuita Komando KIPENSI mkali wa wizkid..!
Una moyo MGUMU zaidi ya RELI ya MJERUMANI mkuu..!
 
Povu limekutoka sana,si vibaya ukipata burudani.
 
KARIBU WCB.
 
Alisema alikiba "kuachia nyimbo nyingi ni kutojiamini", sasa sijui siku hizi hajiamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…