Alikiba: Samahani mashabiki wangu kwa kuchelewesha video ya chekecha

Alikiba: Samahani mashabiki wangu kwa kuchelewesha video ya chekecha

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Staa wa muziki Alikiba amesema kuwa video shooting ya wimbo wake ‘Chekecha' ambayo imepangwa kufanyika Afrika Kusini, imechelewa kutokana na vurugu dhidi ya raia wa kigeni (Xenophobia) zilizoibuka hivi karibuni nchini humo.

"Tayari tulikuwa tumeplan kila kitu unajua kunakuwa kuna zile dancing, choreographer wangu alikuwa ameshacreate kila kitu amewatumia dancers wa South Africa, lakini kilichotufelisha ni hii Xenophobia iliyokuwa imetokea," alisema Alikiba kupitia Ubaoni ya E-Fm. "Vile vile unajua vifaa kule wanakuwa wanaazima kwahiyo imekuwa ni sheria ambayo imepitishwa hairuhusiwi kufanya hivyo mpaka patulie."

Hata hivyo Alikiba amesema mipango yote inaenda vizuri na siku si nyingi atasafiri kuelekea Afrika Kusini kwaajili ya kulipa deni la video alilonalo kwa mashabiki wake.

"Kwahiyo tumefanya tena opportunity nyingine tumepata tayari namshukuru Mungu tumeshapanga kila kitu." Kwa kuonesha kuwa anawajali na kuwaheshimu mashabiki, King Kiba hakusita kuwaomba msamaha kwa kuchelewa kufanya video ya ‘Chekecha', wimbo ambao una karibia kufikisha miezi mitatu toka ulipoachiwa mwishoni mwa February.

"Mimi nataka kuchukua nafasi hii kukuomba samahani, mafans wangu wote na wapenzi wa muziki, najitahidi sana lakini sisi tunapanga yetu na Mungu anapanga yake."

Chanzo: Bongo 5

====

Namshauri Alikiba hii video afanyie hapa nchini sioni sababu ya kwenda south mazingira tuliyonayo yanatosha kabisa kuipendesha video ya wimbo huu!
 
Sawa mfalme ngoja kwanza hii mwana tuipe kura iwe video bora ya mwaka
 
Huyo kobe anataka mashindano na farasi atafia njiani, nenda kafanye video kwa r kelly wewe usipende kuiga kwani south peke yake ndio inapofanywa video, mbona weusi wanafanya video hadi zanzibar na bado kali, unafeli wee ali kibakaa
 
Binadamu hawana jema kweli kweli.
 
Huyo kobe anataka mashindano na farasi atafia njiani, nenda kafanye video kwa r kelly wewe usipende kuiga kwani south peke yake ndio inapofanywa video, mbona weusi wanafanya video hadi zanzibar na bado kali, unafeli wee ali kibakaa
dadamond mwaka huu hana lake tuzo za bet
 
Ukitaka kuwajua wachawi wa dotcom, wee ingia jf
 
Huyo kobe anataka mashindano na farasi atafia njiani, nenda kafanye video kwa r kelly wewe usipende kuiga kwani south peke yake ndio inapofanywa video, mbona weusi wanafanya video hadi zanzibar na bado kali, unafeli wee ali kibakaa

Mbona Diamond alimuiga CPWAA kufanya video SA hamkuongea.??
 
Mbona Diamond alimuiga CPWAA kufanya video SA hamkuongea.??

Kuna watu wanashangaza aisee kwahyo wanataka dadamondi tu atolee SA mbona akina davido lina hadi kina chege ommy dimpozi wanatolea video. Mkuki kwa nguruwe huo unaitwa. Walisema hana hela ya kutolea video sasa wame change eti anashindana na kuiga.
 
Mimi wala hujanikosea King Kiba.Maana sina mamlaka ya kuhoji kwanini unachelewesha video na wala sijawahi kufanya hivyo.
Naisubiri kwa hamu, all the best.
 
Mimi wala hujanikosea King Kiba.Maana sina mamlaka ya kuhoji kwanini unachelewesha video na wala sijawahi kufanya hivyo.
Naisubiri kwa hamu, all the best.

Hivi hawa wasanii wetu (siyo kiba peke yake) wanapotoa hizi video zao wao kama wao wanarudishaje hizo gharama wanazoingia na kupata faida? manake naonaga kama vile tunazipata bure bure tu, we don't pay anything zaidi ya hizi MB za kuidownloadia
 
Nijuavyo mimi gharama zinarudi pale video itakapobamba msanii anapata mialiko kibao ya show.Na kama itakubalika zaidi na thamani ya msanii husika hupanda.
Kama alikua anachaji 3ml basi inaweza panda hadi 10-15 ml n.k
 
Staa wa muziki Alikiba amesema kuwa video shooting ya wimbo wake ‘Chekecha’ ambayo imepangwa kufanyika Afrika Kusini, imechelewa kutokana na vurugu dhidi ya raia wa kigeni (Xenophobia) zilizoibuka hivi karibuni nchini humo.

“Tayari tulikuwa tumeplan kila kitu unajua kunakuwa kuna zile dancing, choreographer wangu alikuwa ameshacreate kila kitu amewatumia dancers wa South Africa, lakini kilichotufelisha ni hii Xenophobia iliyokuwa imetokea,” alisema Alikiba kupitia Ubaoni ya E-Fm. “Vile vile unajua vifaa kule wanakuwa wanaazima kwahiyo imekuwa ni sheria ambayo imepitishwa hairuhusiwi kufanya hivyo mpaka patulie.”

Hata hivyo Alikiba amesema mipango yote inaenda vizuri na siku si nyingi atasafiri kuelekea Afrika Kusini kwaajili ya kulipa deni la video alilonalo kwa mashabiki wake.

“Kwahiyo tumefanya tena opportunity nyingine tumepata tayari namshukuru Mungu tumeshapanga kila kitu.” Kwa kuonesha kuwa anawajali na kuwaheshimu mashabiki, King Kiba hakusita kuwaomba msamaha kwa kuchelewa kufanya video ya ‘Chekecha’, wimbo ambao una karibia kufikisha miezi mitatu toka ulipoachiwa mwishoni mwa February.

“Mimi nataka kuchukua nafasi hii kukuomba samahani, mafans wangu wote na wapenzi wa muziki, najitahidi sana lakini sisi tunapanga yetu na Mungu anapanga yake.”

Chanzo: Bongo 5

====

Namshauri Alikiba hii video afanyie hapa nchini sioni sababu ya kwenda south mazingira tuliyonayo yanatosha kabisa kuipendesha video ya wimbo huu!

Kama ndio ivyo director godfather c alikuja bongo wiki nzima kwa nn hakushoot ? Yy aseme anasubiri apate show azichange ndio afanye video mwisho wa siku video inanzia choon. Puuuu.
 
Nijuavyo mimi gharama zinarudi pale video itakapobamba msanii anapata mialiko kibao ya show.Na kama itakubalika zaidi na thamani ya msanii husika hupanda.
Kama alikua anachaji 3ml basi inaweza panda hadi 10-15 ml n.k

Okay nimekuelewa, mi nilidhani kuna hela anapata directly kutokana na mauzo ya video yake, kumbe video ni ya kumtangaza ili apate mialiko ya show, now I know!!

That's means isipobamba imekula kwake, gharama alizoingia kuitengeneza atakuwa kama katoa sadaka vile
 
Back
Top Bottom