Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,831
- 5,489
Siku za hivi karibuni kumetokea Msiba wa msanii wa kike wa Bongofleva Haitham. Na mazishi hayo yamefanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na watu mashuhuri na wasanii mbalimbali na mmoja wao akiwa msanii Ali Kiba.
Wakati wa mazishi kuna kitendo ambacho kimetokea ambacho kimepeleka Ali Kiba kutoa kauli ambayo sio nzuri au inayoonekana kudharirisha Dini ya Wakristo. Mimi binafsi kama Chief Lumanyika nimechukia sana na kupelekea kwenda kwenye Account yake ya instagram na kumu-unfollow hili nisiwe naona post zake.
View: https://youtu.be/C3rMRxBCXRU?si=giuRLLh1MAzofSfh
Kitendo hicho cha kukashifu Dini ya Wakristo kimetokea ambapo kwenye Video watu wanaonekana wapo kwenye mazishi na hatua za kuzika mwili wa marehemu ambapo Ali Kiba aliona kama anarekodiwa na watu, ambapo akaonekana kustaajabishwa na kutoa kauli ya "Nyie ni wakristo?", Akiwauliza vijana ambao ndio walikuwa wakimrekodi Ali Kiba hapo msibani.
Kutumia neno "Nyie ni wakristo", ni Disrespect na ni kitendo cha kumaanisha kuwa Dini ya wakristo ndio ya wafanya uovu, au ya watu wasiofaa, au ya watu wa ovyo. Kwamba Wakristo sio watu wa kuheshimu Mazishi. Cha kushangaza Tanzania ni nchi yenye Dini nyingi wakiwemo wapagani, lakini kitendo cha yeye kusema moja kwa moja kuwa nyie ni wakristo bila ya kujua hao watu anaowauliza ni Dini gani ni kutokuheshimu Dini ya kikristo. Kwa sababu Tukio hilo lingeweza kufanywa na mtu yeyote hata ambaye ni Muislamu ambaye ni wa Dini yake, budha au mpagani.
Kauli hii ya Ali Kiba pia imezua hoja mitandaoni kupelekea watu kuchukizwa na Kauli hii, na moja ya account ambayo nimeona watu wamechukua ni kwenye Instagram page ya Bongotrending Habari.
Hakuna sehemu yoyote kwenye Dini ya wakristo wanaposema tuwarekodi watu kwenye mazishi au wakiwa msibani. Hivyo hata ikitokea mkristo anarekodi mazishi, basi hiyo ni hulka yake binafsi na haina uhusiano wowote na Dini ya kikristo.
Ali Kiba anapaswa kuomba Radhi au Wakristo tuanze kuzisusia nyimbo zake kama jinsi wasanii wa Marekani na nchi nyingine wanavyofanyiwa wakizingua. Mimi staki kumuona tena, nimefuta hata nyimbo zake.