Alikiba unapaswa kuomba RADHI Wakristo

Alikiba unapaswa kuomba RADHI Wakristo

Kuna Dini fulani watu wake wengi wana chuki na Dini nyingine, hawakai bila kutaja Dini ya wenzao, wabaguzi sana.
 
Ila mwamba una complicate sana mambo asee. Acha kupeleka Kila kitu kwenye negative mkuu.

Maisha sio magumu kihivi mkuu

By the way unahisi kwa bandiko lako hili unaweza convince watu kususia nyimbo za Ali just like that? Huwajui wabongo wewe
Dini ni kitu sensitive sana, ndio maana, kama Dini ni kitu cha kawaida ebu pitisha Nguruwe msikitini alafu wakikuuliza wajibu hivyo kuwa Wanapenda ku complicate mambo ndio utajua hujui... Mimi siko hapa kuwaambia watu kususia nyimbo bali tumechukizwa na kauli yake hiyo ya kuonyesha kuwa Wakristo ni watu wa ajabu
 
Siku za hivi karibuni kumetokea Msiba wa msanii wa kike wa Bongofleva Haitham. Na mazishi hayo yamefanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na watu mashuhuri na wasanii mbalimbali na mmoja wao akiwa msanii Ali Kiba.

Wakati wa mazishi kuna kitendo ambacho kimetokea ambacho kimepeleka Ali Kiba kutoa kauli ambayo sio nzuri au inayoonekana kudharirisha Dini ya Wakristo. Mimi binafsi kama Chief Lumanyika nimechukia sana na kupelekea kwenda kwenye Account yake ya instagram na kumu-unfollow hili nisiwe naona post zake.

View: https://youtu.be/C3rMRxBCXRU?si=giuRLLh1MAzofSfh
Kitendo hicho cha kukashifu Dini ya Wakristo kimetokea ambapo kwenye Video watu wanaonekana wapo kwenye mazishi na hatua za kuzika mwili wa marehemu ambapo Ali Kiba aliona kama anarekodiwa na watu, ambapo akaonekana kustaajabishwa na kutoa kauli ya "Nyie ni wakristo?", Akiwauliza vijana ambao ndio walikuwa wakimrekodi Ali Kiba hapo msibani.

Kutumia neno "Nyie ni wakristo", ni Disrespect na ni kitendo cha kumaanisha kuwa Dini ya wakristo ndio ya wafanya uovu, au ya watu wasiofaa, au ya watu wa ovyo. Kwamba Wakristo sio watu wa kuheshimu Mazishi. Cha kushangaza Tanzania ni nchi yenye Dini nyingi wakiwemo wapagani, lakini kitendo cha yeye kusema moja kwa moja kuwa nyie ni wakristo bila ya kujua hao watu anaowauliza ni Dini gani ni kutokuheshimu Dini ya kikristo. Kwa sababu Tukio hilo lingeweza kufanywa na mtu yeyote hata ambaye ni Muislamu ambaye ni wa Dini yake, budha au mpagani.

Kauli hii ya Ali Kiba pia imezua hoja mitandaoni kupelekea watu kuchukizwa na Kauli hii, na moja ya account ambayo nimeona watu wamechukua ni kwenye Instagram page ya Bongotrending Habari.

Hakuna sehemu yoyote kwenye Dini ya wakristo wanaposema tuwarekodi watu kwenye mazishi au wakiwa msibani. Hivyo hata ikitokea mkristo anarekodi mazishi, basi hiyo ni hulka yake binafsi na haina uhusiano wowote na Dini ya kikristo.

Ali Kiba anapaswa kuomba Radhi au Wakristo tuanze kuzisusia nyimbo zake kama jinsi wasanii wa Marekani na nchi nyingine wanavyofanyiwa wakizingua. Mimi staki kumuona tena, nimefuta hata nyimbo zake.

Ukristo sio dini mpuuzi wewe
 
Ni kweli wakristo tunapenda kirekodi misiba wala hajakosea kiufupi tunazingua
Hakuna mkristo ambaye anayerekodi msibani... ukristo hausemi turekodi msibani, mkristo yoyote anayerekodi msibani hiyo ni hulka yake binafsi... Hata hivyo Dini zingine pia wanarekodi msibani... Hata YouTube zipo video nyingi tu za misiba ya waislamu wanarekodi, na hao utasema ni wakristo...
 
Mtoto wa kiume acha kuweka vinyongo sijui ume-mfollow sasa inasaidia nn?

Kama umechukua acha kusambaza chuki pia utajua maana zaidi kama alikuwa na nia mbaya au laah?
Kumu-unfollow imenisadia mimi binafsi, kwa sababu maamuzi ni yangu ya kipi nione na kipi nisikione... Siwezi kutizama mambo ya mtu anayekashfu Dini yangu
 
Dini ni kitu sensitive sana, ndio maana, kama Dini ni kitu cha kawaida ebu pitisha Nguruwe msikitini alafu wakikuuliza wajibu hivyo kuwa Wanapenda ku complicate mambo ndio utajua hujui... Mimi siko hapa kuwaambia watu kususia nyimbo bali tumechukizwa na kauli yake hiyo ya kuonyesha kuwa Wakristo ni watu wa ajabu
Mbona mfano haupo kwani huyo jamaa alikuja kanisani kwenu kusema hivyo?

Unapelekaje nguruwe msikitini?
 
Hukionagi kama kichokoraa fulani kinajishaua hakina hata lolote anadharau na huku anamtegemea Mo yaani tz hakuna wakunitisha wote ni maskini tu sema wapo kidaraja huyo sio superstar huyo ni mwehu na mchukiaga sana . Kina sura kama kenge mbuzi hata ukiamua kumpika haivi haliki kwa kachumbari au nini .

Mke wake kasepa kanatunzwa ni kamario kazee
Wivu tu unakusumbua.
 
Kumu-unfollow imenisadia mimi binafsi, kwa sababu maamuzi ni yangu ya kipi nione na kipi nisikione... Siwezi kutizama mambo ya mtu anayekashfu Dini yangu
Sasa maamuzi yako ni mazuri ila ujinga ni kutaka watu nao wamchukie..
.Wewe ni muumini wa dini wala sio mmiliki wa dini pia jaribu kufuatilia ufafanuzi kwa nn kasema hivyo.
 
Mleta mada wala huelewi ulichokiwakilisha hapa,unaendeshwa na chuki tu,umesema Kiba kauliza "Nyie ni wakristo?" Hilo ni swali kauliza na sio hoja,wewe umejuaje kua hilo swali kaliuliza kisa kupigwa picha? Kumbe angeuliza "nyie wapagani?" Au "Nyie waislamu?" Wewe ndio ungeona sawa?
 
Sasa maamuzi yako ni mazuri ila ujinga ni kutaka watu nao wamchukie..
.Wewe ni muumini wa dini wala sio mmiliki wa dini pia jaribu kufuatilia ufafanuzi kwa nn kasema hivyo.
Hizo ni falsafa zako... Kuleta habari humu ni kuonyesha kwa namna gani msanii kubwa ambae unawafuasi wengi wa Dini tofauti tofauti hutakiwi kutoa kauli za kudharau dini za wengine.

Uzito wa Dini unategemea na Imani yako, sasa sio kwa kila mtu Dini ni nyepesi kama wewe unavyoichukulia... Ndio maana hata yule aliyechana Quran alipostiwa na vyombo vya habari, mbona hukutoka na kukataza wasiposti kuaminisha watu ujinga wa kumchukia huyo bwana
 
Back
Top Bottom