Aliko Dangote ajutia kutoinunua Arsenal iliyokuwa inathamani ya dola bilioni 2, sasa ni dola bilioni 4

Aliko Dangote ajutia kutoinunua Arsenal iliyokuwa inathamani ya dola bilioni 2, sasa ni dola bilioni 4

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mfanyabiashara tajiri zaidi barani Afrika, Aliko Dangote, amekiri kuwa anajutia kutokununua klabu ya Arsenal ambaye ni shabiki mkubwa wa Klabu hiyo kipindi ambacho thamani yake sokoni ilikuwa ni dola bilioni 2 tofauti na sasa ni $4 bilioni.
1727187709700.png
Dangote alifichua kuwa alikuwa na nafasi kubwa ya kununua klabu hiyo kwa dola bilioni 2 (£1.5 bilioni). Hata hivyo, haikuwezekana kufanya hivyo kwani alikuwa anakamilisha mradi wake mkubwa wa kiwanda cha mafuta cha Dangote wakati huo, ambacho kwa sasa kinazalisha dizeli nchini Nigeria.

Dangote amedai kuwa kama angelinunua Klabu hiyo basi asingeweza kukamilisha mradi wake huo ambao uwekezaji uliogharimu dola bilioni 19, uliozinduliwa Mei 2023, na wenye uwezo wa kuzalisha mapipa 650,000 kwa siku. Kwa hiyo, ilikuwa ni lazima kumaliza mradi wake au kwenda kununua Arsenal.
 
Kibiashara yuko sawa, lakini kijamii hayuko sawa. Ni Ujinga kununua timu ulaya badala kukuza timu za hapa kwetu.
Aanuwezo wa kifedha aanzishe club yake, iwe na nguvu na maarufu kama Arsenal. Mbona waarabu wana wanunua kina Ronaldo, naye afanye hivyo akuze mpira wa miguu Nigeria na Afrika.
 
Back
Top Bottom