Alikufa tar 24/7 na alizaliwa tar 24/7 na zote zikiwa ni Ijumaa

Alikufa tar 24/7 na alizaliwa tar 24/7 na zote zikiwa ni Ijumaa

Wakuu habari zenu,

Kuna swala limenishangaza kidogo! Kuna mdogo wangu amefariki juzi Ijumaa ya tar 24/7/2015 kwa ugonjwa wa kansa ya utumbo mpana. Siku mbili nyuma kabla hajafa alikuwa anaongea vitu vya ajabu ajabu na akili inakuwa sawa, ila siku ile ambayo alikuwa anakata roho alikuwa anaongea kiarabu si kiarabu yaani alikuwa anaongea lugha isiyoeleweka na kabla ya kukata roho aliniambia nipige magoti na akanishika kichwani huku akitaja jina langu. Na pia alifanya hivyo kwa watu wote tuliokuwa tunamuhudumia kwa ukaribu sana.

Ila kilichonishangaza zaidi ni kitendo cha kufa tarehe aliyozaliwa na zote zikiwa ni siku ya ijumaa! Alizaliwa 24/7/92 na amekufa 24/7/2015 zote zikiwa ni ijumaa.

Swali langu ni kwamba hii inaweza kuwa na maana yoyote?

Peke yake Mungu ndiye ajuaye majibu ya maswali yako
 
[QUOTE=mshana jr;Hebu Google mysteries of 9/11 mimi hapa nitakupunja

mi nimegoogle ila naona shambulio LA marekani tu hata sijaelewa uhusiano ngoja nkusubiri tu Mshana
 
Pole sana BI/Bwana Tahira la Mirembe. Kusema kweli haya mambo huwa yanaacha maswali mengi kwa watu wa karibu. Sasa ubaya wa suala hili hata tukilijadili halitatupa suluhu ya kumrejesha mtu aliyekwisha kufa, cha msingi hapo mtoa mada ni kujitakasa ili siku ukifa uende katika uzima wa milele.
UKipenda kutafakari sana mambo ya waliokufa kwamba wamekufa kwa halali au la utajinajisi na baadae utamkosea Mungu. Biblia inasema yaliyowekwa wazi ni ya kwetu lakini yaliyofichika ni ya Mungu mwenyewe.
Mche Mungu tengeneza maisha yako ili umilele wako uwe mzuri
Barikiwa sana
 
amina mtumishi kwa maneno ywnye hwkima ba busaia ya lali qqa juu
 
Back
Top Bottom