Alikuwa mtu au nilikutana na jini au ubongo wangu ndo ulikuwa una-hallucinate: Mwanamke mzuri kapendeza, na hanijui aliniomba 2000 ili akale

Maneno yanaweza kuwa ya uongo, kuna muda inabidi uongeze uchunguzi wako. Labda angeniomba 50,000 au 30,000. Lkn 2000 kwa ule urembo kweli. Yaan ningekua na picha mngeshangaa. Plus yale marashi inaonekana alikua hajatokea mbali sana sababu yalikua makali bado na mazuri
Kwhy angekuomba 30K, ungempa. Ila 2k ni jini?
 
Hahahahahaaaa. Ati msambwanda ulokosa mwenyewe....

Yan nikisema napata mixed feelings ndo maana yake hio. Ule mzigo aisee ulikua next level kiukweli. Af mrefu wa kati kiasi
Ulifeli wapi? Au alikua anakutisha?
 
Ni muendelezo wa story zile zile za demu mwenye marashi na kwato za punda
 
Huyo demu alijua kwa Jinsi ulivyomkubali. Akikuomba 2K. Utampa hata 10K au hata zaidi.

Bahati mbaya kwake, ukawa unawaza majini.
 
Maneno yanaweza kuwa ya uongo, kuna muda inabidi uongeze uchunguzi wako. Labda angeniomba 50,000 au 30,000. Lkn 2000 kwa ule urembo kweli. Yaan ningekua na picha mngeshangaa. Plus yale marashi inaonekana alikua hajatokea mbali sana sababu yalikua makali bado na mazuri
Mavazi yasikushangaze mzee yanafunika kilichopo tumboni tu, laiti matumbo yangekua na vioo ungeelewa
 
Ulifeli wapi? Au alikua anakutisha?
Yale mazingira nlokutana nae aliniogopesha tu, sijui hata fear ilitokea wp. Kipindi nipo nyuma yake nli-appreciate mzigo lkn muda wa maongezi kila kitu kikapotea kabisa akilini
 
Au ulikua unaogopa watu wanaokuzunguka? Yeye alikua amekuelewa hakua jini wala nini
 
Habarini mabibi na mabwana...

Nimekaa na hiki kisa natafakari mara mia mia lkn sipati jibu, naishia kupata mixed feelings tu.

Ilikua hivi, Jumamosi iliopota nilitoka zangu kwenda mazoezini mida ya saa kumi na mbili. Niko zangu nakimbia kwenye barabara ya rami, mida hio ilikua bado tupu kiasi na kwa mbele nikamuona mdada fulani hivi kavaa yale madela yanayong'aa ng'aa hivi, huwa yanakua na rangi ya njano imechanganywa na nyeusi kwa mbali. Na inaonekana alikua amelishikilia kwa mbele sababu kwa nyuma huo mzigo aiseee ulikua umejichora shape namba nane kapisa ile ya kuprint. Wowowoo imejazia balaa.

Sasa mimi nikawa bize zangu kuongeza speed nikiwa nyuma yake, yeye alikua anatembea. Ile nmefika karibu nae kama mita 3 hv akasimama akageuka nyuma kama ananisubiria. Nikashangaa kiasi lkn nilivofika usawa nae akanisimamisha, yale marashi yalikua sio ya dunia hii aisee.

Ile kunisimamisha nikamuangalia sura, mwanamke ni mzuri ana rangi ya maji ya kunde hivi. Akanisalimia nikajibu. Ila kilichofuata ndicho kikanishangaza na ndo kinachofanya nifikiria hadi sasa. Yule mwanamke alinambia "Samahani kaka, nna njaa kweli naomba unisaidie elf 2 kama unayo" Jamani sio typing error, aliniomba elf 2, (2000).

Mimi nikabaki nashangaa kama nusu dakika huku nafikiri nini hiki. Yaan ukiangalia kuanzia shape lake,, malashi yalokua yananukia pale, sura yake, lile dela lake lilivo zuri (nadhan mnayafaham haya madela, kama ya special hivi yellow na black). Akilini nikapiga hesabu haraka na kwa wale wenzangu na mimi tuliosomea Cuba na baadae Israeli nadhan mnajua sometimes hii huwa ni mitego tu aidha ya kishirikina ua kiintellijensia.

Kiukweli nikamwambia yule dada, "hapa sina hela kabisa, si unaona nimevaa nguo za mazoezi hivo sijabeba pesa" Yule mdada akajibu kwa upole kabisa "Sawa kaka angu".

Hela nilikua nayo lakini nikaogopa aidha ingekuwa ni uchawi au mambo mengine yenye madhara kwangu sababu haiwezekani mwanamke mzuri vile aniombe 2000 na kwa kukazia kabisa "ana njaa sana"

Usiku nikaingiwa na mawazo kwamba bora ningemuomba namba nimtumie kwa simu then nile kimasikhara lkn upande mwingine wa akili unanambia ningekula jini.

Vipi wadau wenzangu, mlishawahi kutana na hii scandal?
Hiyo inaitwa "over expectation" mazee!

Mtu unamhukumu kwa wajihi wake na haiba yake, dah!

Cha kushangaza elfu mbili unaona siyo hela inayoweza kumsaidia mtu kupata mlo!

Alikueleza shida yake iliyokuwa na kipaumbele kikubwa kwa wakati huo direct, hakupenda kukutolea mlolongo wa matatizo yake mengine, alikuwa mwanamke mstaarabu na alihitaji kusaidiwa.

Hata hivyo sijapata sababu ya msingi iloyokupelekea kujishuku shuku na kujishitukia!

Kwani mjini umeingia lini kuanza kuishi mkuu?
 
Dunia imebadilika sana mkuu. Unatoa hio 2k unashangaa mkono unaotoka kupokea una vidole vitatu, hio trauma yake utapona lini sijui.
 
Ila pamoja na story una roho mbaya wala si roho ngumu.
Pia kuna mambo ya kufikirika ya kishirikina yamekuganda kama ukoko wa uji wa mhogo.
Jiulize kwanini nadharia hasi 2 na hafifu ndo ulizipa ushindi kuzid nadharia chanya maelfu?
Na kama una elimu dunia, imekukomboa kwa mbali sana.
Wema ni wema tu.
Ubaya ni ubaya tu.
KUna raha sana katika kuwa suluhisho(positive impact).
Hekma inasema, In case of doubt, the benefit goes the right(positive) wing.
Bahat mbaya ulichagua left.
Fikiria nadharia hizi pia.
....binadam si watu wazuri(je uwe katili kwao?)
....mchumba hasomeshwi (je usimsaidie umpendae katika kusoma kwake?)
....usimhurumie kichaa (je una hakika ubaya wake ndo ulimlipa vile?)
Nakadhalika 72.
Kifupi tu ndugu kutoa au kusaidia umnufaisha zaidi mtoaji, maana hustawi ndan ya moyo kuliko mpewaji anayenufaika tu materially!
 
Yaan hapa ndipo pananiuma, What if sikua sahihi, na kweli alikua ana njaa. Roho inaniuma sana nikifikiria hivo. Lakini wengiine ni chuma ulete chief. Hio hela inaenda kufanyiwa utaalamu huko unakua mtafutaji wa watu tu
Yaliyopita so ndweli, ganga yajayo Mkuu.
 
Yaan hapa ndipo pananiuma, What if sikua sahihi, na kweli alikua ana njaa. Roho inaniuma sana nikifikiria hivo. Lakini wengiine ni chuma ulete chief. Hio hela inaenda kufanyiwa utaalamu huko unakua mtafutaji wa watu tu
Ukikadiria hyo perfume inacost sh ngap afu awe anataka buku 2....?nakupongeza kwa kuruka huo mtego..hilo ni jini
 
Habarini mabibi na mabwana...

Nimekaa na hiki kisa natafakari mara mia mia lkn sipati jibu, naishia kupata mixed feelings tu.

Ilikua hivi, Jumamosi iliopota nilitoka zangu kwenda mazoezini mida ya saa kumi na mbili. Niko zangu nakimbia kwenye barabara ya rami, mida hio ilikua bado tupu kiasi na kwa mbele nikamuona mdada fulani hivi kavaa yale madela yanayong'aa ng'aa hivi, huwa yanakua na rangi ya njano imechanganywa na nyeusi kwa mbali. Na inaonekana alikua amelishikilia kwa mbele sababu kwa nyuma huo mzigo aiseee ulikua umejichora shape namba nane kapisa ile ya kuprint. Wowowoo imejazia balaa.

Sasa mimi nikawa bize zangu kuongeza speed nikiwa nyuma yake, yeye alikua anatembea. Ile nmefika karibu nae kama mita 3 hv akasimama akageuka nyuma kama ananisubiria. Nikashangaa kiasi lkn nilivofika usawa nae akanisimamisha, yale marashi yalikua sio ya dunia hii aisee.

Ile kunisimamisha nikamuangalia sura, mwanamke ni mzuri ana rangi ya maji ya kunde hivi. Akanisalimia nikajibu. Ila kilichofuata ndicho kikanishangaza na ndo kinachofanya nifikiria hadi sasa. Yule mwanamke alinambia "Samahani kaka, nna njaa kweli naomba unisaidie elf 2 kama unayo" Jamani sio typing error, aliniomba elf 2, (2000).

Mimi nikabaki nashangaa kama nusu dakika huku nafikiri nini hiki. Yaan ukiangalia kuanzia shape lake,, malashi yalokua yananukia pale, sura yake, lile dela lake lilivo zuri (nadhan mnayafaham haya madela, kama ya special hivi yellow na black). Akilini nikapiga hesabu haraka na kwa wale wenzangu na mimi tuliosomea Cuba na baadae Israeli nadhan mnajua sometimes hii huwa ni mitego tu aidha ya kishirikina ua kiintellijensia.

Kiukweli nikamwambia yule dada, "hapa sina hela kabisa, si unaona nimevaa nguo za mazoezi hivo sijabeba pesa" Yule mdada akajibu kwa upole kabisa "Sawa kaka angu".

Hela nilikua nayo lakini nikaogopa aidha ingekuwa ni uchawi au mambo mengine yenye madhara kwangu sababu haiwezekani mwanamke mzuri vile aniombe 2000 na kwa kukazia kabisa "ana njaa sana"

Usiku nikaingiwa na mawazo kwamba bora ningemuomba namba nimtumie kwa simu then nile kimasikhara lkn upande mwingine wa akili unanambia ningekula jini.

Vipi wadau wenzangu, mlishawahi kutana na hii scandal?

Siku hizi hayo yamekuwa ni mambo ya kawaida sana.

Mimi binafsi nilikuwa napata lunch katika mgahawa mmoja (open venue), mara akapita dada mmoja na akaja kukaa kando ya kiti nilichokaa mimi, nikadhani naye kaja kuagiza chakula, mara kwa sauti ya upole akanisalimia; "habari yako kaka", safi tu dadaa, nikamjibu huku nikijua ni salamu ya kawaida kwakuwa kanikuta pale, kumbe ilikuwa ndio gia namba moja ya kuniingia, "Samahani kaka naomba unipatie japo elfu na mimi nipate chakula" aliniomba kwa sauti ya huruma sana, pale chakula kilikuwa kinaanzia sh 2,000/=. Nilishikwa na huruma nikamwambia aagize chakula, akaagiza.

Nashukuru Mungu siku hiyo mfukoni sikuwa haba, basi nilipomaliza kula nikamwachia sh 2,000/= mimi nikasepa, kipindi naondoka alinishukuru sana.

Alikuwa mwanamke mzuri kiasi kwamba huwezi kutaraji kwamba angekuwa na shida hiyo ya kukosa sh 1000/-, lakini ndio maisha, nikakumbuka kipindi fulani mimi nilikosa nauli tu sh 500/- na ilinibidi kutembea karibu km 20 hivyo sikumshangaa sana yule dada.

Tofauti yangu mimi na wewe ni; mimi sikumtamani huyo dada kutokana na shida yake nilimsaidia tu ili kutimiza kauli ya wahenga; tenda wema usingoje shukurani, saidia tu huwezi jua nawe utasaidiwa na nani!!.
 
Ila pamoja na story una roho mbaya wala si roho ngumu.
Pia kuna mambo ya kufikirika ya kishirikina yamekuganda kama ukoko wa uji wa mhogo.
Jiulize kwanini nadharia hasi 2 na hafifu ndo ulizipa ushindi kuzid nadharia chanya maelfu?
Na kama una elimu dunia, imekukomboa kwa mbali sana.
Wema ni wema tu.
Ubaya ni ubaya tu.
KUna raha sana katika kuwa suluhisho(positive impact).
Hekma inasema, In case of doubt, the benefit goes the right(positive) wing.
Bahat mbaya ulichagua left.
Fikiria nadharia hizi pia.
....binadam si watu wazuri(je uwe katili kwao?)
....mchumba hasomeshwi (je usimsaidie umpendae katika kusoma kwake?)
....usimhurumie kichaa (je una hakika ubaya wake ndo ulimlipa vile?)
Nakadhalika 72.
Kifupi tu ndugu kutoa au kusaidia umnufaisha zaidi mtoaji, maana hustawi ndan ya moyo kuliko mpewaji anayenufaika tu materially!
Chief asante kwa somo. Ningekua nna roho mbaya conscience isingeniuma kiasi hiki kama nlivyoelezea hapo juu.

Lakini tusikimbie ukweli, dunia imebadilika sana chief. Kuna quote inasema "Set boundaries with people because when you are too kind it's easy to get misused".

Sio kwamba niliamua kuwa negative lakin niliamua kutokana na mazingira na past experience nlizopitia. Rafiki yangu alishawahi kumpa lift mrembo mmoja ile kufika kumshusha sehemu akaanza kumpigia kele eti ana-mbaka. Baada ya hapo wakatokea watu wakamlazimisha jamaa amlipe fidia huyo dem, yule jamaa alilipa laki tano hivi hivi na bado scandal ikafika kwa mke wake.

Mimi ningempa pale sijui nini kingetokea, lakini kuliko kumpa nikawa kwenye hatari ni bora nisimpe na nisiwe kwenye hatari. Kuna magroup mengi ya kusaidia zaidi yake, kama nilikua wrong basi nitacover kwa wengine.
 
Back
Top Bottom