Alikuwa mtu au nilikutana na jini au ubongo wangu ndo ulikuwa una-hallucinate: Mwanamke mzuri kapendeza, na hanijui aliniomba 2000 ili akale

Alikuwa mtu au nilikutana na jini au ubongo wangu ndo ulikuwa una-hallucinate: Mwanamke mzuri kapendeza, na hanijui aliniomba 2000 ili akale

Usiku nikaingiwa na mawazo kwamba bora ningemuomba namba nimtumie kwa simu then nile kimasikhara lkn upande mwingine wa akili unanambia ningekula jini.


Hapa ndipo watu wengi huwa tunafeli, mtakuja kitongoza na kulala na watoto wa ndugu zenu bila kujua.
 
Chief asante kwa somo. Ningekua nna roho mbaya conscience isingeniuma kiasi hiki kama nlivyoelezea hapo juu.

Lakini tusikimbie ukweli, dunia imebadilika sana chief. Kuna quote inasema "Set boundaries with people because when you are too kind it's easy to get misused".

Sio kwamba niliamua kuwa negative lakin niliamua kutokana na mazingira na past experience nlizopitia. Rafiki yangu alishawahi kumpa lift mrembo mmoja ile kufika kumshusha sehemu akaanza kumpigia kele eti ana-mbaka. Baada ya hapo wakatokea watu wakamlazimisha jamaa amlipe fidia huyo dem, yule jamaa alilipa laki tano hivi hivi na bado scandal ikafika kwa mke wake.

Mimi ningempa pale sijui nini kingetokea, lakini kuliko kumpa nikawa kwenye hatari ni bora nisimpe na nisiwe kwenye hatari. Kuna magroup mengi ya kusaidia zaidi yake, kama nilikua wrong basi nitacover kwa wengine.
Sikukatalii tahadhari lakin naona uko too risk conscious hadi unaweza kupoteza utu wa kawaida, ukaidhuru afya ya roho na nafs!
Nataman usipoteze utam wa kusaidia unaloweza though cautiously.

Nikupe kisa changu binafs
Ni jion, natokea kijijin kwetu msiban narud mjini km 52 hiv.
..njian nikakutana na mama ana mtoto mchanga ameshakosa hiace za kwenda mjini nikasimamishwa.
..nikatoa tu lift mana nilkuwa na ndugu yangu tu.
.. njian nikala mzinga kupinduka mara 4. Gari nyanga nyanga.
Mi mzima (Ashukuriwe sana aliyebuni mkanda). Ila gari likawa light off.
..Ila huyo mama na zaid mtoto wanalalamika maumivu sana.
..Nikakod gari haraka hadi zahanat ya karib, na mmewe akaja usiku.
..Ndg yang aliumia sana kichwan kushonwa kwa kupasuliwa na mlango.
.. nikalipia gharama na kuwasafirisha wote hadi kwao wilaya jiran baada ya kuonekana hakuna issue kubwa kiafya.
Nikajikuta kama laki 240 zimeenda.
Na nilitoa lift penye nauli ya 2500.
..BAADA YA WIKI YULE MAMA AKANIPIGIA SIMU KUWA ANAHITAJI LAKI 3 MAANA HAZALISHI ANASIKILIZIA AFYA YAKE.
..Je nisitoe lift katika maisha yangu tena?!
Anyway, LIFE IS A PRISM, EVERYBODY SEES IT FROM HIS/HER ANGLE.
 
Mimi juzi nimetoka msibani (kanisani) tegeta huko mdada akanifata akaniambia dada samahani Naomba 1000 ya nauli nami nikamjibu sina (alipendeza na Tunguo twake twa mitego)baada ya jibu langu akaniambia Naomba 1000 chochote nitakupa,nikamuuliza mimi mwanamke mwenzako utanipa nini??akaniamgalia nami nikamkazi jicho huyo pole pole akaondoka(huyu alikuwa kazini mchana kweupe)
 
Mimi juzi nimetoka msibani (kanisani) tegeta huko mdada akanifata akaniambia dada samahani Naomba 1000 ya nauli nami nikamjibu sina (alipendeza na Tunguo twake twa mitego)baada ya jibu langu akaniambia Naomba 1000 chochote nitakupa,nikamuuliza mimi mwanamke mwenzako utanipa nini??akaniamgalia nami nikamkazi jicho huyo pole pole akaondoka(huyu alikuwa kazini mchana kweupe)
Duuh, alitaka akupe mkasi
 
Siku hizi hayo yamekuwa ni mambo ya kawaida sana.

Mimi binafsi nilikuwa napata lunch katika mgahawa mmoja (open venue), mara akapita dada mmoja na akaja kukaa kando ya kiti nilichokaa mimi, nikadhani naye kaja kuagiza chakula, mara kwa sauti ya upole akanisalimia; "habari yako kaka", safi tu dadaa, nikamjibu huku nikijua ni salamu ya kawaida kwakuwa kanikuta pale, kumbe ilikuwa ndio gia namba moja ya kuniingia, "Samahani kaka naomba unipatie japo elfu na mimi nipate chakula" aliniomba kwa sauti ya huruma sana, pale chakula kilikuwa kinaanzia sh 2,000/=. Nilishikwa na huruma nikamwambia aagize chakula, akaagiza.

Nashukuru Mungu siku hiyo mfukoni sikuwa haba, basi nilipomaliza kula nikamwachia sh 2,000/= mimi nikasepa, kipindi naondoka alinishukuru sana.

Alikuwa mwanamke mzuri kiasi kwamba huwezi kutaraji kwamba angekuwa na shida hiyo ya kukosa sh 1000/-, lakini ndio maisha, nikakumbuka kipindi fulani mimi nilikosa nauli tu sh 500/- na ilinibidi kutembea karibu km 20 hivyo sikumshangaa sana yule dada.

Tofauti yangu mimi na wewe ni; mimi sikumtamani huyo dada kutokana na shida yake nilimsaidia tu ili kutimiza kauli ya wahenga; tenda wema usingoje shukurani, saidia tu huwezi jua nawe utasaidiwa na nani!!.
Hongera sana ndugu,mimi kuna siku nipo kwa mama ntilie napata chai akaja kaka ni mlemavu wa miguu(mguu mmoja)akaketi karibu yangu akanisalimia na kuomba anunuliwe chai basi nikamwambia agiza akaagiza yaan bili yake ni mara tatu ya nilichokula mimi na mimi nikajua atakula chapati2 na chai dah!uzuri siku hiyo nilikuwa na kijipesa mfukoni(ni bora kumpa pesa kuliko kumwambia agiza)
 
agiza akaagiza yaan bili yake ni mara tatu ya nilichokula mimi na mimi nikajua atakula chapati2 na chai dah!uzuri siku hiyo nilikuwa na kijipesa mfukoni(ni bora kumpa pesa kuliko kumwambia agiza)
Hahahahahahahaaa, usingekua na hela ungeosha vyombo wakat kala mwingine
 
Hongera sana ndugu,mimi kuna siku nipo kwa mama ntilie napata chai akaja kaka ni mlemavu wa miguu(mguu mmoja)akaketi karibu yangu akanisalimia na kuomba anunuliwe chai basi nikamwambia agiza akaagiza yaan bili yake ni mara tatu ya nilichokula mimi na mimi nikajua atakula chapati2 na chai dah!uzuri siku hiyo nilikuwa na kijipesa mfukoni(ni bora kumpa pesa kuliko kumwambia agiza)


Upo sahihi mkuu, nashukuru nimejifunza; ni bora kumpa pesa kuliko kumwambia aagize, kumwambia aagize ni jambo la hatari.🙏🏻🙏🏻
 
Yaan hapa ndipo pananiuma, What if sikua sahihi, na kweli alikua ana njaa. Roho inaniuma sana nikifikiria hivo. Lakini wengiine ni chuma ulete chief. Hio hela inaenda kufanyiwa utaalamu huko unakua mtafutaji wa watu tu
NIamini mimi ulikuwa sahihi sana hata kama watu milioni moja wakikupinga,, Narudia tena ulikuwa sahihi sana.. Mimi ilinitokea 5yrs Ago.
A day to remember in my entire life na sina kumbu kumbu ni watu wangapi nishawaambia mpaka wa leo hii..
Sitasahau kamwe Maishani mwangu.
 
Usione ni warembo! Wapo ambao wana shida sana.
Pengine alivaa hivyo ili akapate wa kumpa hiyo ya kula.
MImi ningempa tu wala nisingemwomba cho chote,mimi siamini katika mambo ya chuma ulete.
Lakini upande mwingine kama nafsi inakataa kwa sababu umemhisi kwa hivyo ullivyodhania siyo kosa!
 
Habarini mabibi na mabwana...

Nimekaa na hiki kisa natafakari mara mia mia lkn sipati jibu, naishia kupata mixed feelings tu.

Ilikua hivi, Jumamosi iliopota nilitoka zangu kwenda mazoezini mida ya saa kumi na mbili. Niko zangu nakimbia kwenye barabara ya rami, mida hio ilikua bado tupu kiasi na kwa mbele nikamuona mdada fulani hivi kavaa yale madela yanayong'aa ng'aa hivi, huwa yanakua na rangi ya njano imechanganywa na nyeusi kwa mbali. Na inaonekana alikua amelishikilia kwa mbele sababu kwa nyuma huo mzigo aiseee ulikua umejichora shape namba nane kapisa ile ya kuprint. Wowowoo imejazia balaa.

Sasa mimi nikawa bize zangu kuongeza speed nikiwa nyuma yake, yeye alikua anatembea. Ile nmefika karibu nae kama mita 3 hv akasimama akageuka nyuma kama ananisubiria. Nikashangaa kiasi lkn nilivofika usawa nae akanisimamisha, yale marashi yalikua sio ya dunia hii aisee.

Ile kunisimamisha nikamuangalia sura, mwanamke ni mzuri ana rangi ya maji ya kunde hivi. Akanisalimia nikajibu. Ila kilichofuata ndicho kikanishangaza na ndo kinachofanya nifikiria hadi sasa. Yule mwanamke alinambia "Samahani kaka, nna njaa kweli naomba unisaidie elf 2 kama unayo" Jamani sio typing error, aliniomba elf 2, (2000).

Mimi nikabaki nashangaa kama nusu dakika huku nafikiri nini hiki. Yaan ukiangalia kuanzia shape lake,, malashi yalokua yananukia pale, sura yake, lile dela lake lilivo zuri (nadhan mnayafaham haya madela, kama ya special hivi yellow na black). Akilini nikapiga hesabu haraka na kwa wale wenzangu na mimi tuliosomea Cuba na baadae Israeli nadhan mnajua sometimes hii huwa ni mitego tu aidha ya kishirikina ua kiintellijensia.

Kiukweli nikamwambia yule dada, "hapa sina hela kabisa, si unaona nimevaa nguo za mazoezi hivo sijabeba pesa" Yule mdada akajibu kwa upole kabisa "Sawa kaka angu".

Hela nilikua nayo lakini nikaogopa aidha ingekuwa ni uchawi au mambo mengine yenye madhara kwangu sababu haiwezekani mwanamke mzuri vile aniombe 2000 na kwa kukazia kabisa "ana njaa sana"

Usiku nikaingiwa na mawazo kwamba bora ningemuomba namba nimtumie kwa simu then nile kimasikhara lkn upande mwingine wa akili unanambia ningekula jini.

Vipi wadau wenzangu, mlishawahi kutana na hii scandal?
= lami

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Omba omba wenye matako hao, siku hizi Wauza Uchi wamembuni mbunu Mpya ya kutia huruma, Sema UTI ungepewa tu ni wewe mwenyewe ulifeli padogo tu.
 
Back
Top Bottom