Alikuwa wapi siku zote?

Ama kweli ibilisi wa mtu ni mtu!
Huyu mwamba anataka kuniharibia ila amechelewa kipindi Niko field hospital x yeye alikuwa intern hospital hiyo hiyo, nilitokea kumpenda sana hii ni baada ya yeye kuonesha dalili za kunipenda...
Unazingua sasa na wewe.. punguza wenge focus na maandalizi ya harusi. Wewe sio wakwanza kuolewa. Grow up
 
Ama kweli ibilisi wa mtu ni mtu!
Huyu mwamba anataka kuniharibia ila amechelewa kipindi Niko field hospital x yeye alikuwa intern hospital hiyo hiyo, nilitokea kumpenda sana hii ni baada ya yeye kuonesha dalili za kunipenda...
hongera kwa ustahimilivu na ujasiri, pole kwa changamoto na setbacks ulizozipitia awali...

skiza,
be bold and focused na kilicho mbele yako..

usibabaike, usipoteze muda wala kutoa kipaumbele kwa anaetatiza ndoto za maisha yako, na asie na nia njema na mafanikio yako...

daima mtangulize Mungu katika kila hatua, unapoelekea kuyafikia makusudi na matarajio yako ya maisha, akuepushe kushadadia jambo ambalo linaweza kumkwaza mwenzi wako...

nakutakia 13th njema..

Neema na Baraka za Mungu ziambatane na kuandamana nanyi nyote, sasa, daima na milele Aimen 🙏
 
Hatari sana
 
Nimekusifu kwakujielewa na kujiamini.
Lazima binti uelewe kuwa 'anga' za shetani huwa ni ndoa ama mahusiano, pamoja na mali.

Kwenye pre ndoa utakumbana na fitina nyingi sana, si tu kutoka kwa huyo zilipendwa wako, hata ndugu zako wa karibu na wa damu, hakuna anayependa wewe ufanikishe jambo la kheri, labda ni wazazi wako pekee.

Nakushauri, wewe na mchumba wako mzibe masikio yenu kwa nta ya nyuki ndiyo mtafikia malengo yenu.
Lakini mkaruhusu kusikiliza ushauri sijui maoni, kufanikisha kutakuwa kugumu sana kama ngamia kuingia kwenye tundu la sindano.

Nayaongea kwa uzoefu mkubwa, nikutakie kila la kheri mama na Mungu akuongoze uyafikie malengo yako sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…