"Aliou Sawadogo" kijana wa Burkina Faso aliyeitungua "Drone" ya Ufaransa kwa manati

"Aliou Sawadogo" kijana wa Burkina Faso aliyeitungua "Drone" ya Ufaransa kwa manati

Novemba 24, 2021 Kijana wa miaka 13 raia wa Burkina Faso, Aliou Sawadogo akiwa na manati yake porini akiwinda ndege, aliona kitu kikiambaa angani.

Sawadogo akatoa jiwe kutoka katika kaptula yake kisha akaliweka katika kigozi cha manati na kuanza kutafuta shabaha.

Akavuta pumzi na kuzishusha kwa kuachia jiwe lililoenda kuidungua ndege nyuki (drone) iliyokuwa angani.

Ndege nyuki hiyo ilikuwa ikipiga picha za kijasusi ambazo serikali ya Ufaransa huzitumia kwa manufaa yake.

Baada ya kuidondosha "drone" hiyo akaiokota kurudi nayo mjini.

Wananchi wakamtunza tuzo ya ushujaa kwa kumuinua juu kisha kuzunguka naye mitaani huku wakiimba nyimbo za kumsifu mtoto huyo.

Ndimi Juma Wage
Dodoma.

View attachment 2753072View attachment 2753073
Unasifia manati? Afrika bado sana!
 
Hii makala iliibwa na kuondoshwa jina langu.

Plz tuache kutenda huo uovu.
 

Attachments

  • Screenshot_20230920-223030.jpg
    Screenshot_20230920-223030.jpg
    113.3 KB · Views: 4
  • Screenshot_20230920-223237.jpg
    Screenshot_20230920-223237.jpg
    106.4 KB · Views: 4
Tunajifunza kutokana na Makosa. Hayakusemwa ni Makosa ya nani, yaweza kuwa ya kwetu au ya wengine.

Muhimu ni kujifunza (funzo).

Kijana alistahili zaidi ya hicho, huenda walimpatia maana taarifa zaidi kumuhusu huyo dogo zimekuwa ngumu kupatikana.
Analipiginia Taifa lake! Awe amepewa au lah ila amelinda taifa lake.
 
Analipiginia Taifa lake! Awe amepewa au lah ila amelinda taifa lake.
"Siku moja nitakuwa Mwanajeshi nitakayelinda rangi zote za Taifa langu" Aliou Sawadogo.
 

Attachments

  • Screenshot_20230921-113452.jpg
    Screenshot_20230921-113452.jpg
    88.2 KB · Views: 4
Back
Top Bottom