Alipost chats kuhusu ujauzito wangu kwenye group la familia, huu sio udhalilishaji?

Alipost chats kuhusu ujauzito wangu kwenye group la familia, huu sio udhalilishaji?

Joined
Dec 9, 2025
Posts
89
Reaction score
213
Ila mimi naye nimeshapitia mengi jamani😭

Wakati nipo chuo, sitasahau siku nilipomtaarifu dada yangu kwamba nina ujauzito. Wiki mbili baadaye tukagombana. Kama njia ya kunikomesha, akachukua zile chats kwenye group la familia ambako mama na baba wote wamo. Nilifuta WhatsApp hapo hapo.

Sikuwai kufikiria ingekuwa ndo mwanzo wa mimi na ndugu yangu wa damu kujengeana chuki ambayo nilijihaidi kuwa ya milele.

Nilijiuliza sana dhamira yake kutuma chats zetu kwenye group ili wazazi waone ilikuwa ni nini? Mtu niliyemuamini kweli?. Wazazi wangu walikasirika sana na nilihisi heshima hasa kwa jitihada zao zote za malezi.

Ila maisha ndo yalivyo, wanadamu si wakamilifu leo utakosea wewe kesho yeye, baada ya muda niliamua kujipa sababu kwamba wenda dada yangu alikuwa ananiwazia mema na kunisaidia nisije kufanya maamuzi ya kijinga kwenye maisha yangu. Nashukuru wazazi walikuwa waelewa

Mtu wako wa karibu alishawahi kuvujisha chats zenu ili kukudhalilisha? Ilikuwaje
 
Ofcz, ni imekuimiza lakini hakukuwa na haja ya wewe kumchukia muhisika šŸ¤

Si ni kweli ulikua na mimba? Au haikuwepo? Na kama umejifungua si wote mmemuona aliyezaliwa? Unless otherwise uliomba ushauri wa mimba kutolewa au ulikua hujui ni nani baba wa mtoto au ni mbabu ndiye uliyezaa naye.

Kosa lake ni kuishirikisha jamii ambayo wewe hukutaka ijue, ila ingejua tu' kuwa una mimba

Acha utoto
 
Back
Top Bottom