Salaam wana jukwaa!
Miaka ya nyuma nikiwa shule nilikuwa na mpenzi (ambae tulianza mahusiano tukiwa kidato cha 3), huyu mpenzi alinipenda kwa kuwa nilikuwa napata mia kwenye hisabati na fizikia na kemia na bayolojia n.k
Tuliishi kikavu kavu mpaka kidato cha 4 tukamaliza bila kutikisa nyavu...akaniambia tutaishi vile mpaka lini? Nikaona aah wacha tuvunje chaga tu.
Alikuja kwenda kusoma kwa museveni kidato cha 5 na 6, akiwa huko tuliwasiliana mno mi nikiwa pale uboizini moshi. Aliporudi likizo maeneo ya kcmc tulivinjari huku nikikosa mapindi kedekede pamoja na ugumu wa people calculate like machine.
Alipokuja chuo kikuu akapangwa hapa DSM na mm nikaenda canada kupiga shule kabla hatujaenda vyuoni akanichana live kuwa ameona hatutofika mbali kwa sababu ya utofauti wa kiimani -dini. Kwa hiyo tusitafutane ye atapata wa imani yake na mimi nichanganye mbiliga zangu.
Niliumia ila sikuwa na namna nilipomuomba game kwa mara ya mwisho akaniambia iwe mara ya mwisho kweli nikamchapa kisawa sawa, nikasepa.
Saivi ana watoto 2 huko Arusha lakini anatafuta mawasiliano yangu kinoma noma na ana mume huko kwa taarifa nilizopewa na wanangu waliopo huko.
Mimi nimewambia wanangu wakazie wasimpe namba waseme hawana namba yangu ila sasa wananitumia screenshot za malalamiko yake anasema yupo tayari kuinunua namba maana amesikia nipo town na kasikia mi sirudi tena majuu. (Ni kweli sirudi) ila si aliniambia kila mtu na zake na kubwa kuliko yeye ni mke wa mtu.
Iweje arudi nyuma tena (maana anawambia kabisa wanangu anataka kurudisha majeshi). Au huu ni mtego?