imhotep
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 55,997
- 88,219
"Kijeshi"?! 🤔yalikuwa ni Mapinduzi ya Kijeshi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
"Kijeshi"?! 🤔yalikuwa ni Mapinduzi ya Kijeshi.
Mkuu imagine mtazamo wako ndo uwe unaaksi 80% ya mtazamo wa watz.Jobless unatokwa na mapovu, huu muda ungeutumia kutafuta kibarua upate hata hela ya kula... Uzembe wako na familia yako kushindwa kujiimarisha kiuchumi usitafute watu wa kuwalaumu...
Tangu uanze kubwabwaja umefaidika nini sasa? Eti una kazi nzuri ipi hiyo ya kuuza matrako labda
Utabisha ila ukweli ni kuwa mpenda demokrasia aling'atuka akaacha nchi ikiwa hoi kiuchumi ' mkondo wa uchumi ulikuwa umechafuka kwa zaidi ya miaka kumi huku mashirika ya Umma yakijiendesha kwa hasara'. Hizi ni nukuu za Prof. Mukandala akimuelezea Rais Ali Mwinyi katika uzinduzi wa Kitabu chake cha Mzee Rukhsa, soma uk. 205 wa kitabu chake.Ndiyo maana nakuita Tahira. Msuya alianza kazi lini? Alikua waziri wa biashara na viwanda na baadaye akawa Waziri Mkuu mara mbili wakati wa Nyerere na Mwinyi.
Uchumi wa Tanzania uliporomoka kikubwa zaidi baada ya Vita ya Uganda- 1978/ baada ya hapo ndiyo kukawa Hakuna pesa na baadaye shillingi kuporomoka.
Sasa Mwinyi alifanya nini? Mwaka 1992 nchi ilifirisika. Aliyeanza kuinua nchi alikua Mkapa.
Wewe unamsikiliza Zitto? Soma vitabu
Nakubaliana na wewe ndugu.Tanzania ishakuwa kama kongo mbona .......
Namba moja watu wameaminishwa burudani
Uchawa nk
Dar naiona kama Kinshasa vile
Ova
Kwa tukio la kutekwa Mtanzania mwenzetu
Nakubaliana na wewe ndugu.
Nimeangalia ile clip inayoonesha tukio la mtu kutekwa mchana kweupe huko Pwani alafu watu wanachukuq video wanashindwa hata kumsadia.
Nimeumia sana maana inathibitisha haya ndo madhara ya kutengenezewa kizazi cha vijana wanaowaza uchawa, kujipendekeza na starehe. Kizazi kisicho na maarifa na kisichoelewa maana ya Haki.
Ni hatari sana.basi itoshe kusema kwamba awamu ya 4 iliharibu hii nchi, itachukuwa generation kuirudisha hii kwenye mstari, ni kama laana iliyo kwenye ukoo inaharibu vizazi hadi vizazi, tuiombee nchi yetu …
Kwwki kabisa. Shida za msingi zilianzia hapabasi itoshe kusema kwamba awamu ya 4 iliharibu hii nchi, itachukuwa generation kuirudisha hii kwenye mstari, ni kama laana iliyo kwenye ukoo inaharibu vizazi hadi vizazi, tuiombee nchi yetu …
Sahihi kabisaNi hatari sana.
Masuala haya ya kutekana hapa Tanzania jinsi yanavyofanyika ni kama vile ilivyokuwa nchini Zaire (DRC) enzi za Utawala wa Dikteta Mobutu Sese Seko, Watu walikuwa wanatekwa mchana kweupe kama hivi wanavyofanya hawa Watekaji kwenye video hii. Nchini Zaire ilikuwa ukitekwa namna hiyo basi utapelekwa moja kwa moja nyumbani kwake Rais Mobutu Sese Seko kwenye makazi yake yaliyopo katika Kijiji Cha Gbadolite ili ukateswe na kisha kuuawa. Hali ilikuwa mbaya sana kupita kiasi nchini Zaire, naona hali kama hiyo hiyo sasa hivi ipo nchini Tanzania. Ni hatari kubwa sana kwa Usalama wa Umma na nchi yote kabisa kwa ujumla wake.
Matukio ya namna hii yana madhara mabaya sana ambayo kamwe hayataweza kuja kurekebishika.
Nashangaa Sana kuona kwamba Serikali iliyopo ipo kimyaaa kabisa licha ya kwamba vilio vya Wananchi ni vikubwa sana katika kulaani matukio ya namna hii. Kulikoni hasa huko Serikalini?
Itafika wakati na wao watakuwa wanatekwa piga nkupige kama MexicoNi hatari sana.

Ndo tunapoelekea.Itafika wakati na wao watakuwa wanatekwa piga nkupige kama Mexico
Ova
Asante mkuu! In short CCM wametuulia Taifa. Tusubiri maziko yetu.Hongera sana mleta mada. Uliyoyasema ni ukweli mtupu.
Leo hii karibia kila nafasi muhimu ya uongozi ambayo ingetoa mwanga kuelekea kwenye maendeleo, wapo machawa wapuuzi kabisa wenye upeo duni, wasiojua chochote zaidi kumtajataja Samia na kumwabudu.
Mchango wa CCM kuiangamiza Tanzania, kuua ubunifu na maendeleo ya nchi, hautaweza kusahaulika kamwe.
Tazama ndani ya Serikali kuu, nani unaweza kusema ni super intelligent, siyo mnafiki, mbunifu, mwadilifu na ambaye anaonesha uongozi wenye matumaini? Hakuna, hakuna kabisa. Hakuna hata mmoja!!
Hawa machawa wa Rais wanaipeleka Tanzania kuwa koloni la waarabu ambao wanapewa kila rasilimali muhimu ya nchi ili washikilie uchumi, na watanzania wabakie kuwategemea hao waarabu kwa kila kitu. Usipomiliki uchumi, ujue umekuwa mateka na mtumwa ndani ya nchi yako.
Hongera sana kwa andiko hilo muhimu, mleta mada. Na wale ambao tayari akili yao imekwishapofushwa, machawa punguani, watakukejeli, lakini ukweli wa andiko hili utasimama daima. Na tufahamu kuwa hakuna chawa mwenye akili timamu na mkweli wa nafsi. Ili uwe chawa, lazima kichwani kuwe kumeyumba, na uamini kuwa bila kujibanza kwa mtu fulani, huna uwezo wa kuishi kwa kutegemea uwezo na maarifa yako. Na hawa machawa ndiyo sasa waliojazana Serikalini, halafu kuna watu bado wanatarajia kuwa haya machawa yataliongoza Taifa kuelekea kwenye maendeleo ya kweli.
Naona una hasira kali kweli!Hongera sana mleta mada. Uliyoyasema ni ukweli mtupu.

Hapa umetetea nini kilogic?Mobutu ni kama Amin wanasingiziwa mambo mengi sana ila walikuwa mtu wema. Mobutu katawala miaka 32 wakati mpenda demokrasia wetu katawala miaka 22 wote kwa pamoja wameacha uchumi wa nchi zao ukiwa goigoi na dhaifu kuliko awali. Tuepuke propaganda za kumsingizia Mobutu.
Kwani kipindi cha Mobutu watu hawakutusua? Hivi hoja ya mleta mada ni kutusua?kny huohuo mfumo watu wanatusua ni akili tu
Samia anafanya kazi sana na inaonekana kila mahali. Uchawa wa kulaumiwa ni Mwalimu Nyerere aliyekubaliana na ule muitikio wa 'zidumu fikra sahihi za mwenyekitiiiii' na hadhira ikaitikia 'zidumuuu' ule ulikuwa mwanzo kabisa wa uchawa.Mwaka 2020 niliandika uzi humu jamvini kuhusu tofauti ndogo iliyokuwepo baina ya Congo ya Mobutu na Tanzania!
Niliandika uzi ule kwa sababu kuna vitu vingi sana vilivyokuwa vinatokea wakati ule havikuwa na tofauti na mambo yaliyokuwa yanatokea nchini Congo kipindi cha Mobutu. Niliweka na Documentary waliyoiandaa wazungu inayoonesha namna Congo ya Mobutu ilivyokuwa (Nashauri wanabodi muiangalie hadi mwisho bila kuchoka na mtajifunza kitu hakika).
Hii ndo ilikuwa Congo ya Mobutu Sese Seko
Amani iwe nanyi Nimeambatanisha na video ya documentary ya Mobutu Sese Seko, aliyekuwa Raisi wa Congo ( Zaire) ili wajumbe mjionee wenyewe Nilichogundua kutoka kwenye documentary hii ambayo ina sub-title ya kiingereza ni kuwa 1. Mobutu alitengeneza kundi kubwa sana la wanafiki waliokuwa...www.jamiiforums.com
Labda watu hawafahamu.
Congo tunayoiona leo ya vijana kuwasifia watu wenye hela na kuwaabudu badala ya kujikita kwenye kupata maarifa ya kuisaidia nchi yao kwenda mbele iliasisiwa na aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo Mobutu Seseko Kuku wa Zebanga.
Baada ya kushika madaraka, Mobutu alitengeneza Congo ya machawa. Ilikuwa huwezi kupata cheo au nafasi Serikalini bila kuonesha unyenyekevu wako na kujipendekeza kwako kwake.
Chama chake alikiita chama dola na kuwatengeneza wa Congo kukisifu chama chake na yeye binafsi. Zilitungwa nyimbo za kumsifu, zilitengenezwa nguo zenye picha zake pamoja na kofia ambazo vijana, wamama na watu wa Congo walitengenezewa utaratibu wa kuzivaa ili kumsifu na kuonesha kuwa maendeleo ya Congo ni yeye na hakuna Congo bila yeye.
Badala ya wananchi wa Congo kutengenezwa kufikiri vizuri kwa fikra huru kwa ajili ya maendeleo yao kwa miaka mingi ijayo, walitengenezwa kuwaza maendeleo ni mtu na bila kumsifu huyo mtu mkono hauwezi kwenda kinywani.
Matokeo ya hayo ni kwamba badala ya kutengeneza vijana na watu wenye akili kwa faida ya nchi yao, walitengeneza mapooza kichwani ambao ndo walipewa madaraka na Mobutu, hivyo nchi ya Congo alishindwa kustawi na kuhimili maadui wa ndani na nje maana walioshika uongozi hawakushika kwa merit ila kwa kujipendekeza kwao kwa Mobutu na chama chake.
Hali hii ndo yanayotokea sasa nchini Tanzania, kwetu Mobutu wetu ni CCM.
Kuanzia mwaka 2012, CCM walianza kutengeneza mfumo wa siasa zilizoshika hatamu leo hii. Walitengeneza mfumo wa vijana wanaoonesha kuwapigania, kuwatetea na kuwasemea vizuri viongozi wao kupewa madaraka makubwa ya uongozi kwenye utumishi wa Umma. Hii ilianza kwa Nape baada ya kumtukana Lowasa na kuonesha kuwa chawa wa JK alikabidhiwa Ukuu wa Wilaya na baadae cheo ndani ya CCM.
Ilifuata kwa Makonda ambaye nae baada ya kuonesha kuwa chawa wa JK kwa kumsema vibaya Lowassa akazawadiwa ukuu wa wilaya.
Kubwa zaidi ni Magufuli ambaye kwenye kila hotuba za kuzindua miradi ya ujenzi alikuwa anamsifia JK mwishowe JK akaona ndo awe Rais wa Tz.
Kipindi cha JK, vijana waliokuwa vyuoni waliotengenezwa na siasa za namna hiyo walianza kuzawadiwa nafasi ya uongozi na utumishi Serikalini kama DAS, DED, DC na nyinginezo.
Alipokuja Magufuli ndo alilifanya suala hili zaidi ya alivyofanya Kikwete. Magufuli alikuwa akikuona leo umemuongelea vizuri kwenye chombo cha habari kesho yake unasikia Msigwa kakutangaza wewe kuwa DC/DED/DAS/RAS/KM au Mwenyekiti wa Bodi au Mjumbe wa Bodi. Watu waliacha kupewa vyeo kwa uwezo wao ila kutokana na uchawa wao kwa Rais na chama chake.
Matokeo yake hali hii imeendelea na kukua hadi kwenye maisha ya kawaida. Mitaani machawa ndo wanqpewa fursa, kwa wasanii wanaotunga nyimbo za kuwasifia viongozi ndo wanapewa tenda za kufanya kazi na Taasisi za Umma ili wapige hela.
Sasa hali hii imefika climax. Siku hizi fedha za umma (kodi za wananchi) zinazotengwa kwenye bajeti ya Serikali kutekeleza miradi mbalimbali zinahusishwa na mtu kusifiwa binafsi kuwa anafanya yeye. Utasikia Magufuli kafanya haya, hakuna kama Magufuli, mara Samia kafanya haya, hakuna kama Samia.
Sasaivi huko CCM kama huvai kofia yenye nembo ya SSH au Samia au nguo yenye picha ya Samia unaonekana kama sio mwenzao.
Kwa wasio na akili wanaweza kuona jambo hili ni la kawaida sana ila kwa wenye akili napenda kuwaambia hizi ni dalili rasmi kuwa Tanzaniartunaenda kuwa kama Congo.
Suala hili linaenda kudumaza sana akili za Watanzania, suala hili linaenda kututengenezea jamii iliyopo Congo leo nchini Tanzania ambayo inaamini kwenye kujipendekeza, kutukuza wenye hela hali iliyofanya Taifa lile leo kufa na kuwa shamba la bibi kwa watu wenye akili (Mataifa mbalimbali ambayo yanaliibia ikiwemo Rwanda na Uganda)
Leo hii Tanzania, Vijana ambao wanashika nafasi zinazopaswa kushikwa na watu smart na intelligent ni vijana ambao wanaamini bila kujipendekeza kwao kwa CCM na Viongozi wao wakuu wasingefika hapo. Vijana hawa hawataweza kuifanya nchi yetu kuhimili hila za maadui wa ndani na nje ambao nchi zao zinawatengeneza kwa kuwapa exposure na kuwatengeneza kuwa smart isivyo kawaida.
Vijana hawa hawataweza kutengeneza Tanzania Dream ambayo inapaswa kutengenezwa na watu wanaoshika nafasi za maamuzi kwa merit na sio uchawa. Watu wanaofanya research na kuandika mambo makubwa na kuyasimamia yawe kweli.
Naionea huruma Tanzania. Kama Vyombo vya dola havitaisaidia kuiondoa CCM madarakani. Sisi ni Congo tunaofuata.
Ungeacha wajadili watu wenye akili timamu. Wewe ni hao walioharibiwa akili kiasi cha kupofuka kabisa.Kuna hoja gani ya kutoa hapa? Yaani Tanzania inafananishwa na Zaire ya Mobutu halafu mimi Mtanzania wa kweli nikae kimya? Eti nitoe hoja!? Upumbavu haujadiliwi!!!!
Hao hawana mchango hata kidogo. Hao ni hasara kwa Taifa na familia zao.Mwashambwa..Tlaatlah...Mwijaku, Babalevo...vijana wenye mchango mdogo mnoo kwa taifa