Alivyoifanya Mobutu Congo DR ndio wanavyoifanya CCM Tanzania. Ni suala la muda tu Tanzania itakuwa kama Congo

Mkuu imagine mtazamo wako ndo uwe unaaksi 80% ya mtazamo wa watz.
Hata ubinafsi wa wacongo utakuwa nafuu mara kumi elfu kuliko sisi.

Pia uzi kama huu matusi ya nguoni kulikon?.kuisema ccm na viongoz walio madarakani kwa nia ya kujenga taifa msichukulie kuwa ni kukosa kaz au chuki binafsi. Ujue hata mchezaj mwenye mpira ndiye anasemwa au kutazamwa,akimpasia mwingine naye huyo atasemwa pia.
 
Utabisha ila ukweli ni kuwa mpenda demokrasia aling'atuka akaacha nchi ikiwa hoi kiuchumi ' mkondo wa uchumi ulikuwa umechafuka kwa zaidi ya miaka kumi huku mashirika ya Umma yakijiendesha kwa hasara'. Hizi ni nukuu za Prof. Mukandala akimuelezea Rais Ali Mwinyi katika uzinduzi wa Kitabu chake cha Mzee Rukhsa, soma uk. 205 wa kitabu chake.



Cleopa David Msuya akiwa Waziri wa Uchumi, Fedha na Mipango ndio aliyeokoa uchumi wa Tanzania enzi za Mwinyi kwa kufuta ushauri na andiko lake kwa mjibu wa Rais Ali Mwinyi mwenyewe.
 

Attachments

Kwa tukio la kutekwa Mtanzania mwenzetu
Tanzania ishakuwa kama kongo mbona .......
Namba moja watu wameaminishwa burudani
Uchawa nk
Dar naiona kama Kinshasa vile

Ova
Nakubaliana na wewe ndugu.

Nimeangalia ile clip inayoonesha tukio la mtu kutekwa mchana kweupe huko Pwani alafu watu wanachukuq video wanashindwa hata kumsadia.

Nimeumia sana maana inathibitisha haya ndo madhara ya kutengenezewa kizazi cha vijana wanaowaza uchawa, kujipendekeza na starehe. Kizazi kisicho na maarifa na kisichoelewa maana ya Haki.
 
basi itoshe kusema kwamba awamu ya 4 iliharibu hii nchi, itachukuwa generation kuirudisha hii kwenye mstari, ni kama laana iliyo kwenye ukoo inaharibu vizazi hadi vizazi, tuiombee nchi yetu …
 
basi itoshe kusema kwamba awamu ya 4 iliharibu hii nchi, itachukuwa generation kuirudisha hii kwenye mstari, ni kama laana iliyo kwenye ukoo inaharibu vizazi hadi vizazi, tuiombee nchi yetu …
Ni hatari sana.

Masuala haya ya kutekana hapa Tanzania jinsi yanavyofanyika ni kama vile ilivyokuwa nchini Zaire (DRC) enzi za Utawala wa Dikteta Mobutu Sese Seko, Watu walikuwa wanatekwa mchana kweupe kama hivi wanavyofanya hawa Watekaji kwenye video hii. Nchini Zaire ilikuwa ukitekwa namna hiyo basi utapelekwa moja kwa moja nyumbani kwake Rais Mobutu Sese Seko kwenye makazi yake yaliyopo katika Kijiji Cha Gbadolite ili ukateswe na kisha kuuawa. Hali ilikuwa mbaya sana kupita kiasi nchini Zaire, naona hali kama hiyo hiyo sasa hivi ipo nchini Tanzania. Ni hatari kubwa sana kwa Usalama wa Umma na nchi yote kabisa kwa ujumla wake.
Matukio ya namna hii yana madhara mabaya sana ambayo kamwe hayataweza kuja kurekebishika.

Nashangaa Sana kuona kwamba Serikali iliyopo ipo kimyaaa kabisa licha ya kwamba vilio vya Wananchi ni vikubwa sana katika kulaani matukio ya namna hii. Kulikoni hasa huko Serikalini?
 
basi itoshe kusema kwamba awamu ya 4 iliharibu hii nchi, itachukuwa generation kuirudisha hii kwenye mstari, ni kama laana iliyo kwenye ukoo inaharibu vizazi hadi vizazi, tuiombee nchi yetu …
Kwwki kabisa. Shida za msingi zilianzia hapa
 
Sahihi kabisa
 
Itafika wakati na wao watakuwa wanatekwa piga nkupige kama Mexico

Ova
 
Hongera sana mleta mada. Uliyoyasema ni ukweli mtupu.

Leo hii karibia kila nafasi muhimu ya uongozi ambayo ingetoa mwanga kuelekea kwenye maendeleo, wapo machawa wapuuzi kabisa wenye upeo duni, wasiojua chochote zaidi kumtajataja Samia na kumwabudu.

Mchango wa CCM kuiangamiza Tanzania, kuua ubunifu na maendeleo ya nchi, hautaweza kusahaulika kamwe.

Tazama ndani ya Serikali kuu, nani unaweza kusema ni super intelligent, siyo mnafiki, mbunifu, mwadilifu na ambaye anaonesha uongozi wenye matumaini? Hakuna, hakuna kabisa. Hakuna hata mmoja!!

Hawa machawa wa Rais wanaipeleka Tanzania kuwa koloni la waarabu ambao wanapewa kila rasilimali muhimu ya nchi ili washikilie uchumi, na watanzania wabakie kuwategemea hao waarabu kwa kila kitu. Usipomiliki uchumi, ujue umekuwa mateka na mtumwa ndani ya nchi yako.

Hongera sana kwa andiko hilo muhimu, mleta mada. Na wale ambao tayari akili yao imekwishapofushwa, machawa punguani, watakukejeli, lakini ukweli wa andiko hili utasimama daima. Na tufahamu kuwa hakuna chawa mwenye akili timamu na mkweli wa nafsi. Ili uwe chawa, lazima kichwani kuwe kumeyumba, na uamini kuwa bila kujibanza kwa mtu fulani, huna uwezo wa kuishi kwa kutegemea uwezo na maarifa yako. Na hawa machawa ndiyo sasa waliojazana Serikalini, halafu kuna watu bado wanatarajia kuwa haya machawa yataliongoza Taifa kuelekea kwenye maendeleo ya kweli.
 
Asante mkuu! In short CCM wametuulia Taifa. Tusubiri maziko yetu.

Hali ni mbaya sana maana naskia hadi wenye akili na mawazo mazuri na huru huko Serikalini wanatengwa na kunyimwa nafasi kwa kigezo eti hawana nidhamu.

Kwa ninavyoona the only way out ili tuweze kurekebisha palipoharibiwa sana ni CCM kuondoka madarakani either kwa njia halali au haramu. Na walivyo na kiburi na kutengeneza wajinga wengi hadi kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Njia pekee ninayodhani itawayoa ni coup.
 
Naona una hasira kali kweli!
 
Hapa umetetea nini kilogic?
 
Samia anafanya kazi sana na inaonekana kila mahali. Uchawa wa kulaumiwa ni Mwalimu Nyerere aliyekubaliana na ule muitikio wa 'zidumu fikra sahihi za mwenyekitiiiii' na hadhira ikaitikia 'zidumuuu' ule ulikuwa mwanzo kabisa wa uchawa.

Marais waliofuatia walijikuta wakifuata tabia za kiutawala walizozirithi kwa watangulizi wao wakidhani wanapita katika njia za kawaida za kichama kumbe wanaleta hulka mbaya ya uchawa.
 
Wakongo uchawa walisababishiwa na Wabelgiji waliowatawala, Mobutu aliurithi huo ujinga kutoka kwa mkoloni.

Mzungu alihakikisha anajenga shule nzuri za muziki na vijana wengi wanaoufahamu ili awapumbaze apate kuwaibia vizuri madini yao.

Alipoibuka Lumumba na sera zenye nia ya kumtetea mwananchi wa kawaida akauwawa haraka sana.

Uchawa wa Tanzania ulianzishwa na Mwalimu Nyerere, alipenda kuzungukwa na wapambe wenye umri mdogo akiwa na lengo la kuwalea kisiasa ili waje kurithi nafasi za viongozi wa kwanza wa Tanzania, lengo lake lilikuwa zuri lakini katika michakato ya kichama likazaa hulka ya uchawa.

Walimpamba sana ili malengo yao ya kibinafsi yaweze kufanikiwa, aliwahi kusema wapambe walimwambia Mwalimu usistaafu kwanza wananchi bado wanakupenda na akaendelea kwa miaka mitano mingine lakini baadae machale yakamcheza akagundua kwamba waliomwambia asistaafu kwanza walitaka kutimiza malengo yao binafsi.

Chawa akipewa uhuru wa kuwepo anatimiza lengo lake binafsi la kimaisha , ni watu wanaofukuza na muda wanaopewa baada ya kuufanya upambe wao kwa kiongozi anayekuwepo madarakani.
 
Un
Kuna hoja gani ya kutoa hapa? Yaani Tanzania inafananishwa na Zaire ya Mobutu halafu mimi Mtanzania wa kweli nikae kimya? Eti nitoe hoja!? Upumbavu haujadiliwi!!!!
Ungeacha wajadili watu wenye akili timamu. Wewe ni hao walioharibiwa akili kiasi cha kupofuka kabisa.

Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kuipuuza hii hoja muhimu sana inayoangalia mstakabali wa Taifa.
 
Ha
Mwashambwa..Tlaatlah...Mwijaku, Babalevo...vijana wenye mchango mdogo mnoo kwa taifa
Hao hawana mchango hata kidogo. Hao ni hasara kwa Taifa na familia zao.

Kuwa chawa ni kukubali kuwa punguani mnafika. Mtu aliyeamua kuwa punguani na mnafiki, anakuwa na faida gani??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…