Mkuu 'Umkhonto', naamini wewe unaamini hivyo ulivyo elezea. Mimi siamini hivyo hata mara moja.
Kwanza hiyo dhana ya 'Tanzania ni nchi ya amani" maana yake ni nini hasa? Amani ni kutekwa watu, kupotezwa na kuuawa? Hii ni amani ya namna gani?
"WaTanzania hawajazoea vurugu"? Kuna binaadam anaye zoea na kukubali kuvurugwa?
Angalia upotofu mkubwa unao uonyesha: eti "usitegemee kupata nguvu yoyote ya umma kuwaunga (CHADEMA) mkono"? Wewe huu uhakika umeupata wapi. Kwa vile leo gharama kubwa imetumika kuzuia maandamano ndiyo kiwe kigezo cha kujivuna hivi? Hivi huelewi ni kiasi gani viongozi wako huko CCM walivyo na hofu kuu sana ya haya yanayo endelea nchini, au ni kujipa tu moyo unapo ingia humu JF.
Wewe unadhani umma wa waTanzania umetulizana kama ulivyo kuwa umetulizana miaka yote? Huoni kabisa tofauti yoyote inayojiongeza kila siku mnavyo vuruga utulivu huo?
Ni hivi: Hakuna binaadam yeyote anayeweza kuwa mtulivu huku akiona maovu yanayo fanyika kila siku ndani ya nchi yake.
Hao Kenya unao watolea mfano, inaeleweka, hawajawahi kuwa na utulivu ndani ya nchi hiyo, kwa sababu ya ukabila na mauchafu mengine. Sasa mambo hayo hayo ndiyo CCM inayo yapalilia hapa kwetu, na bado watu kama wewe mnaamini waTanzania ni watulivu tu, hawajawahi kupigana popote!
'Umkhonto', wewe hukuchukulia tofauti kidogo na washabiki wenzio wa huko CCM mliomo humu JF, kwa sababu pamoja na ushabiki huo, lakini nadhani bado akili za kuchambua hali halisi ya nchi yetu bado unazo. Lakini kama huoni tunako elekea kama unavyoonyesha hapa, naona mambo yamezidi kuharibika zaidi huko ndani ya hicho chama.
Hii mitutu ya bunduki uliyo iona; halafu bado ukadhani Tanzania ni tulivu? Utakuwa unajidanganya mwenyewe.