Alivyokamtwa Lema kwenye ndege ni sawa tu alivyochukuliwa mzee Ali Kibao kwenye basi

Ninakubaliana na wewe.
Swali ambalo ninge shukuru kupata jibu lake ni hiyo "nguvu ya wananchi" inavyo patikana

Kwa nini hawa CHADEMA hawana nguvu ya wananchi; kama ni kweli hawana.
Wamepuuzwa kw sababu ni vibaraka wa Mabeberu
 
Wasingesambaza police wenye silaha kali na vitisho kila mahali , hapo ndio ungekua na nguvu yakusema chadema hawakuungwa mkono na wananchi kwa sababu ulizotaja.
Ili kitokee nini? Nchi zingine mbona Polisi wanasambazwa lakini watu wanaandamana? πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†

Unampambania Mtanzania au siyo? πŸ€ͺπŸ€ͺπŸ€ͺ

Mtanzania hana njaa kwamba anahitaji kupambaniwa
 
Bila hata kuingia uwanjani, Chadema 2, dola 0. Ni wachache sana humu ndani ya hii JF ya sasa wana uwezo na akili ya kuweza kuelewa hilo.

Mambo mawili kwa, mawazo yangu, hivi sasa yamejionesha wazi. Waliomteka Ali Kibao (RIP) ndio hao hao waliomteka Godbless Lema (QED)

Kama ningeweza kutoa ushauri tu wa bure kama Mtanzania mzalendo. Dola mmevuliwa nguo, kama bado mna heshima na hekima chutameni!
 
Sisi raia wema tuliokua kwenye ndege tunaona ni sawa kwa muhalifu anaechochea machafuko kukamatwa , biashara zimeanza kwenda vizuri wao wanataka kuturudisha nyuma
 
Kwa upande wangu niko tofauti kidogo na wewe hawa chadema wamekata tamaa hawana lengo la kushika dola wana lengo la kutafuta mkate wa kila siku tofauti na mwanzo hivyo wananchi wamechoka kusikia ngonjela ambazo hazina matokeo chanya nijuavyo mimi ccm haina uwezo wa kuongoza nchi ni vile tu hakuna mbadala wake na chadema yenyewe inajitafuta kwa kifupi hakuna chama chochote cha siasa kitawafaa wananchi sio ccm wala chadema
 
ccm haitaki upinzani. wapinzani hawaelewi tu? akina mbowe na lisu waachane na mambo ya kutetea watanzania. watanzania hawastahili kusaidiwa wanatakiwa wateseke mpaka ccm watakapochoka wenyewe kuwatesa. kila mtu aishi maisha yake. wa kufa afe wa kupona apone. nchi ilishazindikwa kichawichawi toka awamu ya kwanza. uchawi na maendeleo wapi na wapi.
 
Wasingesambaza police wenye silaha kali na vitisho kila mahali , hapo ndio ungekua na nguvu yakusema chadema hawakuungwa mkono na wananchi kwa sababu ulizotaja.
Acha visingizio wewe Kenya walisambaza polisi na jeshi na silaha nzito hadi magari ya jeshi mbona wananchi waliendelea na maandamano bila woga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…