Aliwahi kusema jaji Augustino Ramadhani,kesi zote hua zinasikilizwa sehemu mbili

Aliwahi kusema jaji Augustino Ramadhani,kesi zote hua zinasikilizwa sehemu mbili

Lee Van free

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2024
Posts
2,833
Reaction score
8,777
Aliwahi kuwa Jaji Mkuu kama sikosei Jaji Augustino Ramadhani,aliwahi kusema kua kesi zote dunianiani hua zinasikilizwa sehemu mbili.
Sehemu ya kwanza ni ndani ya Mahakama na sehemu ya pili ni nje ya mahakama.

Ndani ya mahakama ni ndani ya mahakama kabisa chini ya mahakimu na mauaji.

Kesi hiyohiyo pia hua inasikilizwq,inafatiliwa na kutolewa hukumu na watu wa kawaida ambayo sio majaji wala mahakimu hukumu nje ya mahakama.
Hawa ni watu wote wanaofatilia juu ya shauri hilo wenyw ufahamu na nia ya kutaka kujua kila kitu kinachoendelea mahakamani.

Hii ni Kwa kesi ya aina yoyote.
Maana yake Jaji au hakimu akiamua shauri lolote kimakosa watu hua hawaridhiki na akiamua vema watu huridhika.

Kesi ya Lisu ni moja ya kesi inaendeshwa ndani ya mahakama na pia kuna watu taasisi na jumuiya za kitaifa na kimataifa zinaiendesha kesi hii kila mmoja kivyao.

Kama Tundu lisu kweli ni mkosefu akihukumiwa Dunia itashangilia,loni kama akionewa Dunia itapiga kelele.

Tulishuhudia kesi za majambazi waliouwa watu,wananchi wengi walikua upande wa maamuzi ya mahakama.
Lakini zipo kesi ziliamriwa wananchi wakawa kinyume na mahakama.

Sasa ni angalizo kwenu Mahakama na majaji kuamua Kwa haki kesi ya Lisu.
Vinginevyo muwe tayari Kwa matokeo ya maamuzi yenu.
Kesi hii inafatiliwa na Dunia mzima.

Mjipange,muwe tayari Kwa mrejesho kutoka ndani na nje ya nchi.
Jumuiya ya kimataifa inafatilia Kwa makini kesi hii.
 
Sasa ni angalizo kwenu Mahakama na majaji kuamua Kwa haki kesi ya Lisu.
Vinginevyo muwe tayari Kwa matokeo ya maamuzi yenu.
Kesi hii inafatiliwa na Dunia mzima.
Karayemaha....mhaya, Ndunguru.....Mngoni most probably, Kiwonde sijui

  • Jaji Dunstan Ndunguru (Kiongozi wa jopo)
    • Jaji James Karayemaha
    • Jaji Ferdinand Kiwonde
 
Back
Top Bottom