Aliyekuwa Mfanyakazi wa Nyumbani Jijini Mwanza, Faima Yasin Twaibu (17), ameachiwa huru na Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala ya Mwanza, baada ya shauri la jinai lililokuwa likimkabili kufutwa kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kuwasilisha ushahidi wa kutosha kuthibitisha shtaka dhidi yake.
Faima alikuwa akikabiliwa na Kesi ya Jinai Na. 15883/2026, Jamhuri dhidi ya Faima D/O Yasin Twaibu, iliyosikilizwa mbele ya Jaji Kisanya, alishtakiwa kwa tuhuma za kujaribu kumuua mtoto wake mchanga, baada ya kudaiwa kumweka mtoto huyo juu ya paa la Nyumba muda mfupi baada ya kujifungua kwa hofu mwajiri wake asigundue kuwa alikuwa mjamzito.
Soma zaidi: Tabora: Baba adaiwa kuchinja mtoto mchanga akidai si wake
Katika kipindi cha kesi hiyo, Shirika la WoteSawa Jijini Mwanza lilifuatilia shauri hilo na kumpatia Faima msaada wa kisheria, kijamii na kisaikolojia, pamoja na kuhakikisha yeye na mtoto wake wanapata ulinzi na huduma stahiki.
Uamuzi huo umehitimisha mchakato wa kisheria dhidi ya Faima, huku Mahakama ikisisitiza umuhimu wa mashauri ya jinai kuamuliwa kwa kuzingatia ushahidi wa kutosha, pamoja na kulinda haki na ustawi wa watoto na wasichana walio katika mazingira hatarishi.
Source: Millardayo