Aliye jirani na Kocha Mbovu kuwahi kutokea Taifa Stars Amunike anisaidie Kuniulizia Kwake haya Maswali yangu 11 tu tafadhali

1. Hatuna mikakati
-Senegal wanamikakati, aliefunga goli lapili jana alikuwa under 20 mwaka 2018

- Juzi tu yameisha mashindano ya u20 world cup Senegal, mali, Colombia, Uruguay Japan, Korea nk wanatimu nzuri balaa sisi kunanini?

2. Serilali ya CCM hakuna popote inapoweka mikakati ya kufanikiwa mbeleni
- Elimu imeshuka ipo taabani
- kilimo tumeshuka tupo taabani
- viwanda tumeshuka tupo taabani kiasi kwamba cherehani za nguo nne tunaita kiwanda
- michezo tumeshuka vibaya sio Soccer, Riadha, ndodi wala mieleka tumpo mkiani

Ukuzingatia sababu hizo mbili kuhusu michezo na mafanikio sahau vikombe...Coach hana kosa lolote,

Unawezaje kupambana na mtu mwenye vikosi bora vitatu au vinne ?

Unawezaje kupambana bila mikakati? Wenzetu wanaandaa timu, sisi namagalasa!

Kwanini coach alaumiwe? Mchawi wetu kwa kila jambo Tanzania ni CCM na Serikali yake.

Hawana vision
Hawana strategies
Hawana lolote Ila wao CCM wanaishi kwa propaganda. Soccer sio umbea, sio maneno ni vitendo
 
Watu tupo bongo hatujui hata maendeleo ya kambi kama kuna injuries zozote au matatizo ya kiafya tunabaki kulalama, tumebakia kuwavimbisha kichwa wachezaji wetu wachache wenye kuamini bila wao timu haiwezi kusonga mbele!!
 
Hivi Simba walivyokung'utwa 5-0 na Vita Kinshasa hao Tshabalala, Mkude, Nyoni hawakuwepo? 😂🤣😅!
 
Mechi ijayo tutacheza 12 ndani walai yeye akipanga kikosi chake cha hovyohovyo na sie tunamweka Nyoni ndani akapambane pia....alisikika mlevi mmoja akisema
 
Mkude angetoka mapema sana kwa red card. Pia wale jamaa asingewaweza kabsaaa kasi yao mana yupo slow.
-Kwa upande Wa shabalala umeongea kwa mihemko siyo uhalisia,vipi kwenye mechi zilizopita plus ile iliyotupeleka Afcon huyo Gadiel alicheza vibaya kama alivyocheza Jana?
- Nieleze ni mchezaji gani Jana alikuwa kwenye kiwango plus kapteni mwenyewe.
-Unamlaumu kocha kumchezesha Msuva unaweza nitajia wachezaji angalau watatu Wa taifa stars waliokuwa na influence ya kuifikisha ile timu pale?
-Hivi ulimwengu hakuwa na impact yoyote Jana?

Kiujumla timu yote ukiondoa walioingia ilicheza hovyohovyohovyohovyo isiyosemekana. Kocha ana cha kulaumiwa pia ila wachezaji walaumiwe zaidi
 
chuki ya kocha kwa wachezaji wa Simba inawezekanaje ilihali mabosi wa timu kina Bashite na Karia wote ni Simba?
 
Anataka baadae aje kuifundisha timu ya wananchi kama alivyofanya kocha Maksimo.
Hukumbuki zile enzi za
Nsajiiigwa
 
Naamini Ajib,Mkude na kichuya wasingesaidia chochote,labda Banda. Kwa aina ya wachezaji tuliokuwa nao na namna walivyocheza wanaweza kutoa picha ni namna gani Mkude angetia aibu tena naamini angepata red card mapema sana kwa sababu yuko slow halafu nguvu hana wakati jamaa walikuwa shapu na physic ya kutosha, Ajib na ule unyoronyoro wake jamaa wangekuwa wanachukua mipira wanamwacha kakaa tu, kama msuva alishindwa kucheza basi naamini Shiza angeshindwa zaidi kwa sababu hana nguvu, anakaa sana na mpira na mbiyo hana kama msuva
 
Shukuru CAF kuongeza idadi ya team na Uganda kuonesha uzalendo wa EA
Acha uprimitive,porojo na kukaririshwa wewe,kwani pamoja na kuongezwa timu in mataifa mangapi makubwa kisoka kuliko sisi hayajafuzu? Wapi Zambia, wapi Gabon, Wapi Bukinabe, wapi jirani zetu Rwanda n.k? Au wenyewe hawakutaka kushiriki kwa sababu Misri kuna joto sana!?

Kocha akosolewe tena siyo kwa kujidanganya kwamba ameacha wachezaji wazuri,labda namna ya ufundishaji na mipango lakini apongezwe pia kwa kukufanikishaia wewe na Mimi kuiangalia timu yetu ya taifa kwenye TV ktk mashindano makubwa haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…