Aliye jirani na Kocha Mbovu kuwahi kutokea Taifa Stars Amunike anisaidie Kuniulizia Kwake haya Maswali yangu 11 tu tafadhali

Timu jana ilicheza kama timu ya Shule flani inayoshiriki mashindano ya Umitashumta. Nilimuonea sana huruma Mbwana Samatta kuwa ktk kundi la wachezaji waliocheza namna ile
Unajuwa ndio maana wenzetu hata wale wanaocheza first eleven EPL na wanataka kunuliwa kwa pesa nyingi utaona wanapelekwa under 21 ili wapate experiance sasa unamchukuwa mtu kama Fey Toto ambaye sio kwamba mchezaji mbaya ila unampa majukumu ambayo sio wakati wake katika stage kubwa kama ile unaweza kumuharibia maisha yake ya kimpira huyu mtoto sijui kama jana kalala maana atajiuliza maswali mimi nilidhani nimefika kumbe bado sana na baya zaidi kocha anaenda kumtoa dakika 43 sijui sio udhalilishaji huo? muite mwambie slow down cheza simply dakika chache hizo half time mtoe. Nimemuonea huruma sana jana japo kabla ya mechi nilimwambia rafiki mmoja huyu mtoto sio wa kumpanga wacha ajifunze kuangalia tu kwanza.
 
Kati ya mkude na niyonzima Yupi alibadilisha timu ya simba ikavuka robo fainali?
naona amunike ameanza kupewa maneno yale aliyopewa maximo.
Ile ni Senegal ni level nyingine sio vita fc , nkana au js soura
umewahi kumwona Amunike akicheza enzi zake?
Nimegundua walichofanya wachezaji jana ni kupunguza magoli nawapongeza sana .
Tanzania haina wachezaji wazuri zaidi ya wale waliopangwa jana .
Nyoni na Banda wikuwepo Tanzania ikifurumushwa na lesotho.
Yousef kama hakujituma mazoezini asitegemee namba
 
1. Kikosi cha jana dhidi ya Senegal alikipinga Yeye au alisaidiwa na akina Karia pamoja na Mwakyembe?

2. Ni kwanini ana Chuki sana na Wachezaji Nyota wanaotoka Klabu ya Simba Sports Club?

3. Kwanini alimpanga Beki David Mwantika ambaye alimuita kutoka Tanzania, hakuwa na Mazoezi ya pamoja na Wenzake, wala match Fitness na akampanga huku akimpanga Benchi Mchezaji Kiraka Erasto Nyoni?

4. Anaweza kunipa sababu ya Yeye kupenda kuwatumia Wachezaji kama Himid Mao na Mudathiri Yahaya katika Kiungo cha Ukabaji huku akimuacha na Kumchukia kabisa Natural Defensive Midfielder na ambaye yupo katika Kiwango cha juu Tanzania nzima kwa miaka kadhaa sasa Jonas Gerald Mkude?

5. Je zile Rafu za Kipumbavu ( Kiduduna ) walizokuwa wakizicheza akina David Mwantika, Faisal Salum na Himid Mao Yeye ndiye aliwatuma hivyo walikuwa wakitekeleza Maelekezo yake?

6. Je mpaka hivi sasa Kichwani mwake ana Kikosi chake cha Kwanza kiasi kwamba hata nikimuamsha tu Usiku wa Manane atanitajia bila matatizo yoyote?

7. Je baada ya Beki wake Aggrey Morris Kuumia alipaswa amuite Beki Abdi Banda ambaye alikuwa nae huko huko Kambini Misri au alipaswa amuite Beki David Mwantika ambaye hapo mwanzoni hakumjumuisha katika Kikosi chake kile cha Wachezaji 33 alioondoka nao?

8. Ni kwanini anawapenda sana Wachezaji Thomas Ulimwengu na Himid Mao kiasi kwamba hata kama wakiwa hawako katika Form au Majeruhi lakini Yeye ni lazima tu atawaita na kwenda nao popote pale ambapo Taifa Stars itaweka Kambi yake?

9. Je kati ya Thomas Ulimwengu na Rashid Mandawa ni Mchezaji gani ambaye Kiuhalisia na jinsi Mechi ilivyokuwa Jana alitakiwa ndiyo amuingize ili aweze kuleta Uhai au Mabadiliko katika Timu?

10. Kama tukiamua Kuangalia Mchezaji ambaye amepata Uzoefu wa Michuano mikubwa mikubwa ya Kimataifa je Kwake Yeye kati ya Mohammed Hussein Tshabalala kutoka Simba SC na Gadiel Michael kutoka Yanga SC ni nani angefaa na pengine hata Kumuanzisha katika Mechi ya Jana?

11. Tanzania tunajivunia sana Wachezaji wanaocheza Ligi Kubwa tena za Ulaya kama Samatta anayecheza KRC Genk ya Ubelgiji na Yousuf anayecheza Blackpool ya Uingereza ni kwanini ameamua tu Kumtumia Samatta na Wachezaji wengine wa Kulipwa ila wanacheza Klabu za hapa hapa barani Afrika zisizo na Mafanikio akina Msuva, Himid na Ulimwengu na akimuacha Yousuf benchini?

Mwisho kabisa akishanijibu haya Maswali yangu Kumi na Moja ( 11 ) naomba anisaidie pia kuniambia ni lini atatuachia Timu yetu ya Taifa Stars ili waje Makocha wenye Kuujua Mpira kuliko Yeye, wasio na Chuki wala Visasi kwa Wachezaji kabla Mimi na Wenzangu wenye Uchungu na Hasira kali dhidi yake hatujaamua Kumvizia pale Uwanjani JNIA akirudi na Timu kisha tumpopoe na Mawe na aione Tanzania hii Chungu Kwake!

Msisahau kumwambia kuwa mwana JamiiForums Mimi An Eagle a.k.a BRAINIAC namsalimia ila simkubali kabisa na aondoke tu.
Hao wa Simba wangefanya nini chanya?
 
Faisal Salum ( Fei Toto ) anahitaji Kucheza Mechi 1000 ili aweze Kuufiki uwezo mkubwa na Kiwango Kikubwa cha Mtalaam na Fundi wangu Kipenzi Kiungo Bora wa Ukabaji kwa Tanzania kwa miaka takribani Mitatu Minne iliyopita Jonas Gerald Mkude. Kama Yanga SC mnamtaka Kocha Emanuel Amunike ili asaidiane na Mpuuzi wenu mwingine Mwinyi Zahera mchukueni ila kwa Timu yetu ya Taifa Stars hatumtaki na asipoangalia Siku akirejea pale JNIA tutampopoa na ama Mawe au Mayai Viza.
Mkude anacheza Simba miaka zaidi ya 5 lakini hakuna kocha hata mmoja wa Stars ambaye huwa anampanga
Wakati mnapewa dozi za 5 na Vita,Ahly,Mazembe Mkude ndio alicheza kiungo mchezeshaji ,je angeweza kuwazuia kina Gueye,Diatta,Ndiaye ?
 
Hao wa Simba wangefanya nini chanya?

Wangeipeleka Taifa Stars hii hadi Fainali ya AFCON 2019 hadi tungebeba na Kombe lenyewe. Waliotufungisha Jana walikuwa ni Wachezaji Wawili wa Yanga SC Faisal Salum ( Fei Toto ) na Kelvin Yondani bila kusahau na wale Wachezaji Wawili wa zamani wa Yanga SC Simon Msuva na Ramazan Kessy. Mchezaji pekee aliyetuokoa Jana alikuwa ni Kipa bora kwa sasa Afrika Mashariki kama siyo Kusini mwa Afrika Tanzania One Aishi Salum Manula anayechezea Klabu bora Afrika ya Simba Sports Club.

Je una Swali lingine?
 
Mkude anacheza Simba miaka zaidi ya 5 lakini hakuna kocha hata mmoja wa Stars ambaye huwa anampanga
Wakati mnapewa dozi za 5 na Vita,Ahly,Mazembe Mkude ndio alicheza kiungo mchezeshaji ,je angeweza kuwazuia kina Gueye,Diatta,Ndiaye ?

Mtu anayejua Mpira hawezi Kusema Kiungo Jonas Gerald Mkude ni mbaya au hafai.
 
Wangeipeleka Taifa Stars hii hadi Fainali ya AFCON 2019 hadi tungebeba na Kombe lenyewe. Waliotufungisha Jana walikuwa ni Wachezaji Wawili wa Yanga SC Faisal Salum ( Fei Toto ) na Kelvin Yondani bila kusahau na wale Wachezaji Wawili wa zamani wa Yanga SC Simon Msuva na Ramazan Kessy. Mchezaji pekee aliyetuokoa Jana alikuwa ni Kipa bora kwa sasa Afrika Mashariki kama siyo Kusini mwa Afrika Tanzania One Aishi Salum Manula anayechezea Klabu bora Afrika ya Simba Sports Club.

Je una Swali lingine?
Mahaba Niue.
 
Kwa Kikosi nilichokiona jana, Mchezo mbovu kabisa tulioucheza jana na kwa aina ya Kocha Mbovu Emanuel Amunike hata hiyo Sare ( Draw ) unayoiombea kutoka kwa Kenya ( Harambee Stars ) hutoipata. Kwa aina ya Maandalizi ya Wakenya kwa Kiwango kile Kikubwa walichokionyesha jana walipocheza na Algeria japo nao Walifungwa kuna uwezekano hiyo Siku ya Alhamisi Tanzania ( Taifa Stars ) tukapata Kipigo Kitakatifu kutoka Kwao.

Kocha Amunike hakupaswa Kuwaacha Wachezaji muhimu na wazuri Kikosini ambao nina uhakika wangemsaidia sana kama akina Mkude, Ajib, Banda, Chilunda na Kichuya. Hii Timu ya Taifa Stars nina uhakika kwa Maandalizi haya waliyoyapata kama Makocha wangekuwa Jamhuri Kihwelo na Fred Minziro na kwa jinsi wanavyowajua vyema Wachezaji wa Kitanzania na Saikolojia yao jana Senegal asingetusumbua na kututesa vile na pengine tungefanya Makubwa kuliko vile ambavyo wengi wangetegemea.
Acha utani ,Julio na Minziro hawana leseni za CAF kuwawezesha kukaa benchi la National team! Pili km makocha wetu wana ubora unaofikiria wewe mbona hawaendi kufundisha nje ya nchi? Wanabaki hapa kwa ajira zisizokuwa na mkataba?
 
Mtu anayejua Mpira hawezi Kusema Kiungo Jonas Gerald Mkude ni mbaya au hafai.
Mkude ni average player kwa mashindano Yale!Anatamba dhidi ya Lipuli au Alliance tu, kwa National team hajawahi kung'ara hta kabla ya Amunike
 
Acha utani ,Julio na Minziro hawana leseni za CAF kuwawezesha kukaa benchi la National team! Pili km makocha wetu wana ubora unaofikiria wewe mbona hawaendi kufundisha nje ya nchi? Wanabaki hapa kwa ajira zisizokuwa na mkataba?

Wanabaki hapa kwakuwa Tanzania ni Kutamu Kiongozi. au Wewe hulijui hilo?
 
Mkude ni average player kwa mashindano Yale!Anatamba dhidi ya Lipuli au Alliance tu, kwa National team hajawahi kung'ara hta kabla ya Amunike

Naona unafanana kwa kuwa na Upeo mdogo kama alionao Kocha wako Emanuel Amunike a.k.a Bichwa Pua.
 
Tatizo lako ni mahaba kwa Simba na siyo ubovu wa kocha. Kwani mkude amecheza mechi ngapi na hatujafanya vizuri
1. Kikosi cha jana dhidi ya Senegal alikipinga Yeye au alisaidiwa na akina Karia pamoja na Mwakyembe?

2. Ni kwanini ana Chuki sana na Wachezaji Nyota wanaotoka Klabu ya Simba Sports Club?

3. Kwanini alimpanga Beki David Mwantika ambaye alimuita kutoka Tanzania, hakuwa na Mazoezi ya pamoja na Wenzake, wala match Fitness na akampanga huku akimpanga Benchi Mchezaji Kiraka Erasto Nyoni?

4. Anaweza kunipa sababu ya Yeye kupenda kuwatumia Wachezaji kama Himid Mao na Mudathiri Yahaya katika Kiungo cha Ukabaji huku akimuacha na Kumchukia kabisa Natural Defensive Midfielder na ambaye yupo katika Kiwango cha juu Tanzania nzima kwa miaka kadhaa sasa Jonas Gerald Mkude?

5. Je zile Rafu za Kipumbavu ( Kiduduna ) walizokuwa wakizicheza akina David Mwantika, Faisal Salum na Himid Mao Yeye ndiye aliwatuma hivyo walikuwa wakitekeleza Maelekezo yake?

6. Je mpaka hivi sasa Kichwani mwake ana Kikosi chake cha Kwanza kiasi kwamba hata nikimuamsha tu Usiku wa Manane atanitajia bila matatizo yoyote?

7. Je baada ya Beki wake Aggrey Morris Kuumia alipaswa amuite Beki Abdi Banda ambaye alikuwa nae huko huko Kambini Misri au alipaswa amuite Beki David Mwantika ambaye hapo mwanzoni hakumjumuisha katika Kikosi chake kile cha Wachezaji 33 alioondoka nao?

8. Ni kwanini anawapenda sana Wachezaji Thomas Ulimwengu na Himid Mao kiasi kwamba hata kama wakiwa hawako katika Form au Majeruhi lakini Yeye ni lazima tu atawaita na kwenda nao popote pale ambapo Taifa Stars itaweka Kambi yake?

9. Je kati ya Thomas Ulimwengu na Rashid Mandawa ni Mchezaji gani ambaye Kiuhalisia na jinsi Mechi ilivyokuwa Jana alitakiwa ndiyo amuingize ili aweze kuleta Uhai au Mabadiliko katika Timu?

10. Kama tukiamua Kuangalia Mchezaji ambaye amepata Uzoefu wa Michuano mikubwa mikubwa ya Kimataifa je Kwake Yeye kati ya Mohammed Hussein Tshabalala kutoka Simba SC na Gadiel Michael kutoka Yanga SC ni nani angefaa na pengine hata Kumuanzisha katika Mechi ya Jana?

11. Tanzania tunajivunia sana Wachezaji wanaocheza Ligi Kubwa tena za Ulaya kama Samatta anayecheza KRC Genk ya Ubelgiji na Yousuf anayecheza Blackpool ya Uingereza ni kwanini ameamua tu Kumtumia Samatta na Wachezaji wengine wa Kulipwa ila wanacheza Klabu za hapa hapa barani Afrika zisizo na Mafanikio akina Msuva, Himid na Ulimwengu na akimuacha Yousuf benchini?

Mwisho kabisa akishanijibu haya Maswali yangu Kumi na Moja ( 11 ) naomba anisaidie pia kuniambia ni lini atatuachia Timu yetu ya Taifa Stars ili waje Makocha wenye Kuujua Mpira kuliko Yeye, wasio na Chuki wala Visasi kwa Wachezaji kabla Mimi na Wenzangu wenye Uchungu na Hasira kali dhidi yake hatujaamua Kumvizia pale Uwanjani JNIA akirudi na Timu kisha tumpopoe na Mawe na aione Tanzania hii Chungu Kwake!

Msisahau kumwambia kuwa mwana JamiiForums Mimi An Eagle a.k.a BRAINIAC namsalimia ila simkubali kabisa na aondoke tu.
 
Unaweza kumpa mtu mawazo uliyotaka kuyasema aandike ili na sisi tusome tuelewe.

Wewe usilete usimba wako na uyanga wako hii ni timu ya taifa majungu yako weka mfukoni Mudathir na Mkude wapi na wapi?

Mudathir anauwezo mkubwa sana kuliko mkude wako anarukaruka tu pass hazifiki mechi ya congo
 
Bao 2 tulizopigwa ni sawa na ushindi kwetu ukizingatia kipa wetu ndio alikua MAN OF THE MATCH kwasbb timu tulio cheza nayo ni COMBINE YA ULAYA ndio ilitupiga mande

*SENEGAL SQUAD*

*Goalkeepers:*

-Abdoulaye Diallo (Rennes, France)
-Alfred Gomis (Spal, Italy)
-Edouard Mendy (Reims, France)

*Defenders:*

-Kalidou Koulibaly (Napoli, Italy)
-Moussa Wague (FC Barcelona, Spain)
-Pape Abdou Cisse (Olympiacos, Greece)
-Salif Sane (Schalke,Germany)
-Youssouf Sabaly (Bordeaux,France)
-Lamine Gassama (Goztepe, Turkey)
-Saliou Ciss (Valenciennes, France)
-Cheikhou Kouyate (Crystal Palace, England)

*Midfielders:*

-Alfred Ndiaye (Malaga, Spain)
- Santy Ngom (Nancy, France)
- Idrissa Gana Gueye (Everton, England)
-Keprin Diatta (Club Brugge, Belgium)
-Pape Alioune Ndiaye (Galatasaray, Turkey)
-Sidy Sarr (Lorient, France)
-Henri Saivet (Bursaspor, Turkey)

*Forwards:*

-Ismaila Sarr (Rennes, France)
-Keita Balde (Inter Milan, Italy)
- Mbye Niang (Rennes, France)
-Moussa Konate (Amiens, France)
-Mbaye Diagne (Galatasaray, Turkey)
- Sada Thioub (Nimes, France)
-Sadio Mane (Liverpool, England)

Mungu ibarik taifa stars .......[emoji1324]‍♂
 
Mimi ni shabiki wa yanga haswaaa kwenye feitoto na himid nakubaliana nawe toto bdo kwa game km zle mara nyng akiingia dk za 70 hv 75 ndio anaonekana na himid pia sio yle wa azam kadrop sana ple nyoni, mudathir na hata mkude wangefaa nadhani nyoni ni mgonjwa hata benchi sikumuona tusilaumu sana banda pia alifaa sana badala ya mwantika sijui kocha ana nn ila kwa tshabalala kumuweka benchi gadiel labda aende mbingu ya saba arudi ndio hlo litokee tshabalala bdo sana kwa yle mtoto gadiel ana balaa kk tuweke ushabiki pembeni tuangalie maslahi mapana ya nchi narudia tena tshabalala bado sana asee anakaba kwa macho anajua kupandisha timu ila kwenye kurudippp mtihani!
 
Kwa Kikosi nilichokiona jana, Mchezo mbovu kabisa tulioucheza jana na kwa aina ya Kocha Mbovu Emanuel Amunike hata hiyo Sare ( Draw ) unayoiombea kutoka kwa Kenya ( Harambee Stars ) hutoipata. Kwa aina ya Maandalizi ya Wakenya kwa Kiwango kile Kikubwa walichokionyesha jana walipocheza na Algeria japo nao Walifungwa kuna uwezekano hiyo Siku ya Alhamisi Tanzania ( Taifa Stars ) tukapata Kipigo Kitakatifu kutoka Kwao.

Kocha Amunike hakupaswa Kuwaacha Wachezaji muhimu na wazuri Kikosini ambao nina uhakika wangemsaidia sana kama akina Mkude, Ajib, Banda, Chilunda na Kichuya. Hii Timu ya Taifa Stars nina uhakika kwa Maandalizi haya waliyoyapata kama Makocha wangekuwa Jamhuri Kihwelo na Fred Minziro na kwa jinsi wanavyowajua vyema Wachezaji wa Kitanzania na Saikolojia yao jana Senegal asingetusumbua na kututesa vile na pengine tungefanya Makubwa kuliko vile ambavyo wengi wangetegemea.
Hakuna kitu hapoo tz mnapiga kelele ndio maana kila siku hamkosi sababu..kama wachezaji wana nidhamu mbovu..hata kama ana jua kucheza vp ni kupigwa chini..wa tz bwana alikuwepo Maximo alijitahidi sn kuitengeneza national spirit mkamsema ooh anachagua sn Yanga anapendelea lkn ndiye aliyedhubutu wa wapanga hata wachezaji wa mtibwa, mbeya city nk ilimladi tu amekidhi vigezoo
Tz haita weza kusonga kimichezo mpaka pale mashabiki watakapo ondoa usimba na uyanga..hata tim za mikoani zingekua zinashabikiwa...
 
Back
Top Bottom