Aliye jirani na Kocha Mbovu kuwahi kutokea Taifa Stars Amunike anisaidie Kuniulizia Kwake haya Maswali yangu 11 tu tafadhali

Kwahiyo tulihangaika ili tufuzu tukashiriki au tufuzu tukashindane kama wengine?
Punguza kiherehere na kujifanya una uchungu kama mama mjamzito, Amunike awachukie wachezaji wa Simba kwani anakaa nao mtaa mmoja tuseme wanagombea demu?

Hao wachezaji unaoorodhesha hapa, si siku zote wanacheza na tunafungwa? Yaani hii nchi kila mtu kocha.
 
Ishukuru CCM kwa kufanya mafekeche na Uganda ili kulainisha Mambo.

Kumbuka Tz na Ug zina historia ndefu.
Wewe ni mwepesi sana kusahau, umesahau hao Uganda kwao walinusurika kula kichapo tukatoa draw,na kwenyewe CCM ilienda kuongea nao? Uganda tuliwafunga kihalali kabisa na walikuja kupambana kwelikweli
 
Wewe ni mwepesi sana kusahau, umesahau hao Uganda kwao walinusurika kula kichapo tukatoa draw,na kwenyewe CCM ilienda kuongea nao? Uganda tuliwafunga kihalali kabisa na walikuja kupambana kwelikweli
Hahah, amini nakwambia shukuru uhusiano mzuri ulipo kati ya nchi hizi.

Diplomasia ilitumika kumaliza haya mambo,na sio vinginevyo.
 
Mbona Uganda kwao hawakutufunga. .acheni hizo huyo Mkude away game zote za Simba alifanya nini?
Mimi sijasema Mkude wala nani wote ni walewale tu sijui Fey Toto mimi kwangu bado kupambwa na magezeti tu sasa jana ilikuwa reality check kila mtu kajuwa level yake, Uganda level sio yetu hata kama tulitoka draw kikubwa hapa sababu ya sisi kuwa Egypt kuruhusu team 24 ingekuwa 16 tungesubiri miaka 39 mingine huo ndio ukweli.
 
Yaani Rwanda, Burkina na Gabon nchi kubwa kisoka? sasa leo South Africa anacheza na nani sio Ivory? ungesema Zambia sawa. Team kubwa zote Africa zipo. Egypt, Tunisia, Morocco, Nigeria, Algeria, Senegal, Ghana na Cameroon hawa ndio wafalme wa soka la Africa hao wengine wapo hawapo. Kwa hiyo kama kuna joto ndio maana Zambia alijitoa au? mashindano yote yanachezwa kipindi cha joto kwa taarifa yako mechi ya jana ilikuwa ni 28 Temp hata Dar joto.
 
Ila ndugu nadhani ongezeko la timu limeziathiri timu kubwa kubwa kama Ivory coast, S.A,Gabon, Zambia,jirani zetu Rwanda n.k mana imebidi zisubiri. Au unasemaje?
 
kiukweli hili Kocha ni bovu kuliko yaan linakera ningekuwa na bunduki ningekusubiri Airport nikupige risasi. watanzania kila siku tunasononeka ni lini tutafurahi?

Nilidhani ninayemchukia sana Tanzania nzima nipo peke yangu kumbe tupo wengi! Halafu hata Jana ile Makocha wenzake wakisimama unaona kabisa wanavyohangaika Kuwaelekeza huku na kule Wachezaji wao na Midadi juu muda mwingine lakini lenyewe ( Amunike ) jana lilikuwa linaamka muda mchache na muda mwingi linakaa tu na Mpua wake na Mbichwa wake Mkubwa kama Madafu ya Mafia na Kilwa.
 
Kwahiyo tulihangaika ili tufuzu tukashiriki au tufuzu tukashindane kama wengine?
Mbali ya madhaifu ya kocha Amunike, lkn upumbavu wa Mkude kaeni nao nyie. Hakuna kocha anayejitambua akaingiza kambini timu kwa siku 6 mchezaji anaripoti siku ya 5 jioni.
 
Nlikosea hapo S.A na ivory coast. Ila nnachosema hapa ni kwamba kuongezeka kwa timu siyo factor kubwa sana mana kuna nchi hazijafuzu pamoja na onhezeko hilo.
Burkinafaso,Zambia na Gabon wametuzidi mbali tu kisoka. Na Rwanda hapo nlitolea mfano tu kwamba nao kwa nn wasitumie daraja la ongezeko la timu?
 
Ila ndugu nadhani ongezeko la timu limeziathiri timu kubwa kubwa kama Ivory coast, S.A,Gabon, Zambia,jirani zetu Rwanda n.k mana imebidi zisubiri. Au unasemaje?
Katika hizo Ivory coast wako na wanacheza na South Africa leo hawa kina Rwanda wa kawaida tu hawana ukubwa wowote Africa wala Gabon. Zambia ndio wa kushangaa kakosa vipi lakini super power wote wako huko na ushindani ni mkubwa. Turudi katika mada kuongezwa team imesaidia kama sisi kupata nafasi na ni nzuri kupata ujuzi ili isiwe mwaka huu tu na mashindano yajao tuwepo tatizo letu kubwa ni lazima tukubali bado mpira wetu kuna changamoto nyingi katika uelewa wa tactic wa wachezaji wetu. unaweza kuwa wametuzidi lakini nidhamu muhimu jana hata defence line walikuwa wanashindwa kukaa line moja
 
Naunga mkono hoja
Huyo jamaa maswali yake hayajibiki kamwe kama tukiamua kuchukua kiwango cha mchezaji mmoja mmoja kwa kuwafananisha na wale senegali......
Namshukuru kocha Amunike kwa kuiwezesha timu yetu kushiriki michuano ya afcon ..... Ni miaka 39 imepita tangu mara ya mwisho kushiriki
 
We mpira hutaujua kamwe
 
Mimi nakubaliana na wewe Zambia siku zote wamekuwa zaidi ya sisi ila Gabon ni level yetu wala hao Rwanda kawaida sana, Burkina wao wamekuwa wazuri ila sio kuwa wakubwa kisoka maana hawajahi kufanya vitu vya ajabu. Hao niliowataja North na West Africa ndio wamekuwa vinara wa soka letu huyo South Africa tu ilikuwa tabu kupata nafasi
 
Timu jana ilicheza kama timu ya Shule flani inayoshiriki mashindano ya Umitashumta. Nilimuonea sana huruma Mbwana Samatta kuwa ktk kundi la wachezaji waliocheza namna ile
 
Mbali ya madhaifu ya kocha Amunike, lkn upumbavu wa Mkude kaeni nao nyie. Hakuna kocha anayejitambua akaingiza kambini timu kwa siku 6 mchezaji anaripoti siku ya 5 jioni.

Faisal Salum ( Fei Toto ) anahitaji Kucheza Mechi 1000 ili aweze Kuufiki uwezo mkubwa na Kiwango Kikubwa cha Mtalaam na Fundi wangu Kipenzi Kiungo Bora wa Ukabaji kwa Tanzania kwa miaka takribani Mitatu Minne iliyopita Jonas Gerald Mkude. Kama Yanga SC mnamtaka Kocha Emanuel Amunike ili asaidiane na Mpuuzi wenu mwingine Mwinyi Zahera mchukueni ila kwa Timu yetu ya Taifa Stars hatumtaki na asipoangalia Siku akirejea pale JNIA tutampopoa na ama Mawe au Mayai Viza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…