Aliye mfano wa mwanadamu aketiye katika Kiti cha enzi Mbinguni ni nani?

Aliye mfano wa mwanadamu aketiye katika Kiti cha enzi Mbinguni ni nani?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, shalom!!

( Isaya 6:1-10), Mwanzo 1:26-28). (Matendo 9:4)

Maandiko ya atwambia Mbingu na Dunia zimejaa utukufu wa Mungu, hii inamaanisha Mungu yupo everywhere.

Hapo hapo maandiko yanatwambia kuwa, Mbinguni kipo KITI Cha enzi, na aketiye katika KITI Cha enzi ana mfano wa mwanadamu.

Ni nani huyo?

Je Mungu ana mfano wa mtu/mwanadamu?

Karibuni 🙏

Reference: (Isaiah 6:1-10), (Genesis 1:26-28.). (Ufunuo 1:13-14), ( Daniel 7:9,13,14), (Matendo 9:4).
 
Yesu Kristu, ndio maana kuna wakati tunamuita Mungu.

" Nakwenda kwa baba kuwaandalia makao, ili nilipo mimi, nanyi muwepo".

" Huyu ndie mwanangu mpendwa niliyependezwa nae, msikilizeni yeye"

Ukisoma vizuri hapo juu utaona alikaimishwa majukumu, tukimsikiliza yeye ni sawa na kumsikiliza Mungu.
 
Viumbe vyote vinaongea,

Vyote uvionavyo vinaongea,

Punda aliongea vizuri kabisa, hata mawe yanaweza kuongea pia.

Adamu aliongea na viumbe vyote, vya kimwili na kiroho.
Viumbe wengine nafahamu huwa wanawasiliana kwa sauti za milio na ishara mbalimbali, unajua kinachosababisha aunde maneno tofauti na viumbe wengne ndani ya mwili wake ?
 
Yesu Kristu, ndio maana kuna wakati tunamuita Mungu.

" Huyu ndie mwanangu mpendwa niliyependezwa nae msikilizeni yeye"

Ukisoma vizuri hapo juu utaona alikaimishwa majukumu, tukimsikiliza yeye ni sawa na kumsikiliza Mungu.
Hili Lina UKWELI,

Maana Paulo akiwa njiani kuelekea dameski kuua WATAKATIFU, alitokewa na Mtu aliyengaa kuliko jua, na akawa kipofu pale pale,

Na alipomuuliza u nani wewe ninayekuudhi,

Alisema Yeye ni YESU KRISTO.

GOD IS ONE🤔

Tuendelee kupata majibu ya HOJA hapo juu 🙏
 
Hili Lina UKWELI,

Maana Paulo akiwa njiani kuelekea dameski kuua WATAKATIFU, alitokewa na Mtu aliyengaa kuliko jua, na akawa kipofu pale pale,

Na alipomuuliza u nani wewe ninayekuudhi,

Alisema Yeye ni YESU KRISTO.

GOD IS ONE🤔
Uzi wako ungeuweka kwenye jukwaa la dini ili watu wa huko waujadili kwenye box la dini.
 
Jikite kwenye mada.
Ngoja nijikite humo, Mungu ni wewe mimi na yule , hakuna Mungu kama kitu kimoja chenye nguvu zaidi njee na wewe mimi yule na kile , ukishasema Mungu yupo mahali fulani tayari ushapunguza sifa ya Mungu kuwa Mungu.

Yani kila kitu ni Mungu na Mungu ni kila kitu , na wala hana mahitaji ya kusifiwa wala kuabudiwa , wala hama sababu ya kuwa na chawa ( viongozi wa dini , manabii mitume na nk) ili kufikisha chochote kwa mtu wala kitu ambacho bado ni yeye mwenyewe .
 
Ok,

Ahsante Kwa mchango wako,

Tulia sasa tusikie na wengine wasemaje!!
 
Back
Top Bottom