Aliyeachiwa kwa msamaha wa Rais ahukumiwa miaka 30 jela

Mshtakiwa huyo alipopewa nafasi ya kujitetea kutokana na kosa linalomkabili, aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa hakuwa na fedha ya kujikimu baada ya kutoka gerezani, ndiyo sababu ya kupora.
Duu jamaa alishindwa hata kuwa kuli?
 
In short alichofanya ni kumtukana aliyemsamehe. Kwa trend hii, sheria ya msamaha ibadilishwe kulinda heshima ya rais!
misamaha iendelee kuwepo ila iangalie aina za makosa na rekodi za watenda makosa. Wakosaji wengine akili zao haziko sawa wakisamehewa hurudia makosa yao badala ya kujiepusha kurudia makosa
 
Mshtakiwa huyo alipopewa nafasi ya kujitetea kutokana na kosa linalomkabili, aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa hakuwa na fedha ya kujikimu baada ya kutoka gerezani, ndiyo sababu ya kupora.

Binafsi huwa sioni mantiki ya wewe kurudia tulichokisoma kwenye uzi, ni maoni yangu tu hayo, maana huna unachoongeza kwenye mjadala.
 
ndio utaona umuhimu wa Sharia hapo.
Sharia ndio suluhisho la matatizo ya binadamu,kisiasa,kiuchumi,kijamii n.k
Kwa hio kwa kutumia Sharia akipiga mapanga mwenzie na yeye apigwe mapanga?
 
Mahakama zingekuwa zinatoa adhabu sawasawa na mtuhumiwa alivyotenda...

Kama huyu wa kukata wenzake na mapanga, ilibidi ahukumiwe kucharangwa mapanga + kifungo...
Umebaka?

Unabakwa.

Unatoa hoja.

Nilibaka mwanamke basi nibakwe na mwanamke pia.

Mahakama inapinga.

Kimaumbile inabidi udumbukizwe kitu.

Unapinga pingo la mahakama.

Na kimaumbile mimi sina uke. So hamuwezi kunifanyia nilichofanya.

Mahakama.

Ok sawa, utafanyiwa operation ya kuwekwa uke ili utumikie adhabu yako ya kifungo na kubakwa
 
In short alichofanya ni kumtukana aliyemsamehe. Kwa trend hii, sheria ya msamaha ibadilishwe kulinda heshima ya rais!
Kosa la mtu mmoja haliwezi kusababisha sheria zibadilike ghafla. Mbona rais anateuwa wengi tuu kwenye nafasi nyeti halafu wanaiba na kufanya ufisadi mkubwa na hajapendekeza rais aache kuteua watu?
 
Polisi washamba sana.
Huyo jamaa alipaswa kuzawadiwa wananchi wamgawane.

Myu unaachiwa kwa msamaha na bado unatudi kulekule kulikkkusababisha ufungwe. Ni kipaji
 
Kwa hio kwa kutumia Sharia akipiga mapanga mwenzie na yeye apigwe mapanga?
we hukusukia ikisemwa " Ukiishi kwa upanga,utakufa kwa upanga?"
Ila kwa utaratibu wa Sharia Ni kuwa kisasi(retaliation) Ni Sehemu ya hukumu Katika kosa la mauaji
 
Mshtakiwa huyo alipopewa nafasi ya kujitetea kutokana na kosa linalomkabili, aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa hakuwa na fedha ya kujikimu baada ya kutoka gerezani, ndiyo sababu ya kupora.
Hapa ndio kuna point muhimu sana, magereza mengi yanatengeneza Tatizo Badala ya kutatua Tatizo. The guy was right in the wrong place and time
 
Ukibaka, unakatwa mashine tu ili wakati mwingine usibake au unafanywa kuwa hanithi mashine ibakie kuwa pambo tu...
 
huyu angenyongwa tu
 
Kosa si lake kwani amelazimika kutokana na serikali kitomuandaa jinsi ya kuishi uraiani, ametoka jela katembea kwa mguu mpaka kijijini na huko hana chakula wala pakulala, ataishije!
Panga kalipataje..?

Akili aliyotumia kupata panga la kufanyia ujambazi angeitumia kupata namna ya kujikimu mtaani.

Adhabu ya kifungo ingeambatana na kazi ngumu, she.nzi zake!!!
 
Panga kalipataje..?

Akili aliyotumia kupata panga la kufanyia ujambazi angeitumia kupata namna ya kujikimu mtaani.

Adhabu ya kifungo ingeambatana na kazi ngumu, she.nzi zake!!!
Mtu ambaye si mhalifu kwa sasa kupata mlo mmoja tu kwa siku ni shughuri, panga unaweza ukaazima kukatia kuni na ukalitumia vinginevyo.
 
Kosa si lake kwani amelazimika kutokana na serikali kitomuandaa jinsi ya kuishi uraiani, ametoka jela katembea kwa mguu mpaka kijijini na huko hana chakula wala pakulala, ataishije!
Hiyo si kazi ya mageraza kumuandaa mtu ujinga wake ndio umemponza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…