Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
Msanii yuleWapi RC mtetezi wa Wanyonge?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Msanii yuleWapi RC mtetezi wa Wanyonge?
ChawaMilad anafuatiliwa sana angekua serious vizuri, media nyingine ata bila kupost serikali wangenyooka
Kivipi? Nyie ndo mnafanya viongozi wanaojitoa wanyamaze!Msanii yule
Huu utawala sasa unataka kuzidi ule wa "Uliopita"Wapi RC mtetezi wa Wanyonge?
Uliopota ujinga wa kupotea watoto haukuwepo na utekaji ulikuwepo ila pia wanaharakati walichochea sana JPM aonekane mbaya!Huu utawala sasa unataka kuzidi ule wa "Uliopita"
Yule RC wenu wa Taifa anaejiita mtetezi wa Wanyonge Ajitokeze kusimamaia Haki ya huyu mnyonge anaedai kutendewa unyama na kigogo wa Polisi huko Mkoani kwake Arusha.
Kipimo sahihi Kwa hao watu wanaojigamba ni kutetea watu walioumizwa na wale wanaowalinda au kuwatuma ndio tutajua wanatetea wanyonge badala ya kuwa harass Watumishi wengine wasio husiana na vyombo vya Dola.👇👇
View: https://twitter.com/MwananchiNews/status/1826244030797377756?t=gYB78yAx9sKbGxkBWXXUOR8mfb4PzMY0aRfOAJ5L5bc&s=19
Na akimaliza kukutesa anapandishwa cheo.Kuna mambo yanaumiza, unateseka na mwenzio ni ana cheo.. Kuna muda unatamani uwe hata mchawi umtoe mtu kibusha mpate kuheshimiana 😂🤣
Mkuu haimanishi kwamba hayakuwepo sema tu yame Escalate na waharifu walijifunza tangu wakati hule. Sasa wamezoea hatuponi Kaka.Uliopota ujinga wa kupotea watoto haukuwepo na utekaji ulikuwepo ila pia wanaharakati walichochea sana JPM aonekane mbaya!
Ila hakuna muda matukio ni mengi kama saizi!
Masikango tena? Mimi mtu wa NjombeAcha masimango wewe Mzanzibari
Yule RC wenu wa Taifa anaejiita mtetezi wa Wanyonge Ajitokeze kusimamaia Haki ya huyu mnyonge anaedai kutendewa unyama na kigogo wa Polisi huko Mkoani kwake Arusha.
Kipimo sahihi Kwa hao watu wanaojigamba ni kutetea watu walioumizwa na wale wanaowalinda au kuwatuma ndio tutajua wanatetea wanyonge badala ya kuwa harass Watumishi wengine wasio husiana na vyombo vya Dola.👇👇
View: https://twitter.com/MwananchiNews/status/1826244030797377756?t=gYB78yAx9sKbGxkBWXXUOR8mfb4PzMY0aRfOAJ5L5bc&s=19
Tokea sakata la yule binti aliebakwa kama amekua serious kdg. Ila inabid aache uchawaChawa
Suala la Mahita lipo chini ya Polisi Makao Makuu, na Mwana sheria Mkuu wa SirikaliMimi sijui nachotaka ni kuona RC mtetezi wa Wanyonge anamtetea huyu bwana mdogo ambae ni mnyonge kutoka Mkoa wake.
Nyamitako mwenyewe ameua watu wengi sanaYule RC wenu wa Taifa anaejiita mtetezi wa Wanyonge Ajitokeze kusimamaia Haki ya huyu mnyonge anaedai kutendewa unyama na kigogo wa Polisi huko Mkoani kwake Arusha.
Kipimo sahihi Kwa hao watu wanaojigamba ni kutetea watu walioumizwa na wale wanaowalinda au kuwatuma ndio tutajua wanatetea wanyonge badala ya kuwa harass Watumishi wengine wasio husiana na vyombo vya Dola.👇👇
---
Aliyedai kuvunjwa mguu na kigogo wa Polisi Arusha, adai kutishiwa maisha
Arusha. Sakata la kijana Peter Charles (21) Mkazi wa kata ya Daraja Mbili jijini Arusha aliyedai kupigwa hadi kuvunjwa mguu na askari wa Jeshi la Polisi, amedai kupokea vitisho vya kukatishiwa uhai wake.
Peter alidai amevunjwa mguu ndani ya chumba cha mahojiano kilichopo ndani ya kituo cha kati cha Polisi Jijini Arusha Juni 6, 2024 akilazimishwa kukubali kosa la kucheza kamari baada ya kukamatwa na askari watatu akiwa nyumbani kwao usiku.
Hata hivyo Jeshi la Polisi mkoani humo limemtaka kutoa taarifa kuhusu vitisho hivyo ili zifanyiwe kazi.
Akizungumza na Mwananchi leo Agosti 21,2024, Peter amesema kuwa baada ya kutoa taarifa kwa waandishi wa habari, amekuwa akipokea vitisho vingi kutoka kwa watu asiowafahamu.
“Nimekuwa nikipigiwa simu na watu wanaokataa kujitambulisha ikiwemo siku moja nikiwa nimekaa nyumbani kwetu nikapigiwa simu na mtu akisema kuwa nisionekane tena kituoni kwenda kutoa ushirikiano juu ya mashtaka niliyoyatoa, la sivyo itakuwa ni mwisho wangu duniani.”
“Zaidi ya hiyo, nilipigiwa simu siku nyingine na mtu mwingine akisema kuwa nisiendelee kutoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya tukio hilo kama nayapenda maisha yangu,”amesema Peter.
Amesema kuwa baada ya kupokea vitisho hivyo amekuwa na hofu kubwa ya maisha yake na kuliomba Jeshi la Polisi kuharakisha upelelezi wa kesi yake ili watuhumiwa waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kwa hatma ya watu wengine.
“Mimi sijakata tamaa hata wakiniua lakini sitarudi nyuma kikubwa mimi sina hatma tena duniani baada ya kuvunjwa mguu, lakini nitaendelea kufuatilia kesi hii ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kwa hatma ya watu wengine ambao wanaweza kuwafanyia hivi endapo likiachwa juu juu,”amesema Peter.
Akizungumzia suala hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo amesema kuwa upelelezi wa suala hilo unaendelea ukikamilika utafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili lichukuliwe hatua zaidi.
“Narudia tena kama nilivyosema awali, hakuna mtu yuko juu ya sheria hivyo naombeni mtuache tuendelee na uchunguzi na ikibainika kuna kosa limetendeka basi mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shtaka lake kwa wakati huo,” amesema Masejo.
Hata hivyo Kamanda Masejo amesema kuwa askari huyo bado anaendelea na majukumu yake ya kila siku ya kulitumikia Jeshi la Polisi kama kawaida.
“Unavyoniuliza kama bado yuko kazini unataka nijibu nini hapo, kwani mtu akituhumiwa ndio ametenda kosa? Subirini akibainika ana kosa Jeshi la Polisi litachukua hatua zake,” amesema Masejo.
Masejo ametumia nafasi hiyo, kumtaka kijana Peter kutoa taarifa kwa jeshi hilo kama amepokea vitisho kutoka kwa mtu yoyote na suala hilo litafanyiwa kazi.
Mwananchi
Wataje? Wewe ni muhuni tu Makonda hajawahi kuua mtu hata mmoja!Nyamitako mwenyewe ameua watu wengi sana
Huyo dogo amerithi ukatili kutoka kwa baba yake kama Sabaya alivyorithi ukatili na uuaji toka kwa baba yake. CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala.Omary Mahita
Kesi yake inaendeleaje?
RC anasemajeYule RC wenu wa Taifa anaejiita mtetezi wa Wanyonge Ajitokeze kusimamaia Haki ya huyu mnyonge anaedai kutendewa unyama na kigogo wa Polisi huko Mkoani kwake Arusha.