Aliyedukua tovuti ya Chuo Kikuu aitwa akasome bure

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
Huko India Mwanafunzi mmoja amedukua tovuti za vyuo viwili ambavyo aliomba nafasi ya kusoma Degree ya Usalama wa Mtandao (Cyber Security) lakini akakosa kwa kuonekana hana vigezo. Baada ya kunyiwa nafasi aliingia kwenye website zao na kuzihack.

Vyuo hivyo ni Indian Institute of Technology Kanpur (IIT-K) na Indian Institute of Technology Madras (IIT Madras). Baada ya kuhack, imebidi Indian Institute of Technology Kanpur imuite na kumpa nafasi ya masomo bure.

Habari hii imenikumbusha mwaka 2023 baadhi ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Iringa waliokua wanasomea IT walihack mfumo wa chuo, wakaenda sehemu ya ada, wakajijazia wamelipa ada zote (wakati kiuhalisia walikua wanadaiwa). Wakasoma bure. Walipokuja kugundulika walifukuzwa chuo, kisha wakaburuzwa Mahakamani kwa uhujumu uchumi.

Umejifunza nini??
 
Mpaka hapo havina uwezo wa kumfundisha chochote kama kaweza kuwahack
 
Nimejifunza,mpe mchawi akulelee mwana!
 
Wenzetu wa naangalia potential ya mhusika
 
😳😳😳😳😳😳😳😳😳
 
Wale jamaa walijilipia ada wanafunzi wote wapo kama 200 πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Hao ndio wanajua kutumia vipaji, akihitimu anaajiriwa jeshi au RAW mbona mtakubali show zake
 
Wale vijana wa IFM walipewa kesi baada ya kudukua mfumo wa matokeo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…