Aliyefanikiwa kuondoa kitambi naomba anishauri

Aliyefanikiwa kuondoa kitambi naomba anishauri

Nimekimbia, nimeruka nk lakini nimeshindwa kabisa kukiondoa. Naomba wale ambao mlikuwa na kitambi mtoe maelezo hapa nini mulifanya ili kukiondoa?
Pole sana.
Screenshot_20191130-234949.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni wakiume,Stress kubwa zaidi akazini na mwanfunzi dheni amtie mimba,mbinu atakazotumia kulisovu swala hill hadi kuisha na kitambi kitakua kimeisha,natania tu.
Dana ya kitambi ni stress. Hey jitafutie stress kidogo utaleta mrejesho.

Luna kipindi nilikuwa nakula moo Mona turn kwa siku lakini wapi.

Nikajapigwa na stress za kazini. Kitambi hicho kikaondoka.

God save us

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa na kg 101 sasa 85 kg ambayo normal kwangu ,najiskia mwepesi. Nimepunguza sana misosi na bia ,
 
Tusaidie kaka

Sent using Jamii Forums mobile app
Ipo hivi kiongozi
1. Kujitoa
2. Weka malengo
3. Tengeneza ratiba ya msosi pamoja na mazoezi.

Kwa upande wangu mimi nilifanya na ninaendelea kufanya hivi:-

1. Nina amka saa kumi na moja na nusu, najianda kwa mazoezi. Saa kumi na mbili kasorobo naanza kukimbia kwa dakika 50 mpaka 1hr.
Ila nilivyoanza nilikua nakimbia 25 min ila nikawa naongeza mdogo mdogo.
2. Nikishatoka kukimbia na chemsha maji ya moto yenye limao kama lita moja na nusu. Nakunywa mdogo mdogo mpaka kwenye mida ya saa sita yanakuwa yameisha.
3. Baada ya hapo nina hakikisha lunch napata kwenye mida ya saa sita na nusu au saa saba. Lunch ipo hivi:- vyakula vyenye carbohydrate kwa mfano wali, ugali n.k naweka kidogo sana tena sana ila na hakikisha nakula mboga za majani, protein na matunda kwa wingi. Dinner hivyo hivyo ila napunguza zaidi.
4. Maji kwa siku nakunywa lita 3+

Vitu ambavyo nimeviondoa kwenye ratiba yangu ni:-
1. Chai
2. Soda
3. Bia nimeondoa ila mara moja moja huwa nashtua kiu ikinibana sana.
4. Juisi za viwandani.

Matokeo.

Nimeweza kupunguza 15kg ndani miezi miwili na wiki tatu.

Angalizo.

Kama una vidonda vya tumbo hii ni hatari kwa afya yako.
Usitegeme matokeo ya haraka haraka, uvumilivu unahitajika.

Kila la kheri.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza lazima ujikane yaani uchukie overweighting/obesity

Pili; udhamirie kutaka kupungua uzito

Tafuta support ya members of your family especially your wife/husband if any etc

Epuka kampani ya marafiki wapenda kulakula hovyo.

Jiwekee nidhamu na self control ktk kula na kunywa.

Ona kuwa unahitaji kuishi maisha marefu yenye afya njema na Amani.

Nunua mizani iwe nyumbani




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana kupungua sana kama utadhamiria .

Kwa kuanzia acha kabisa kula vyakula vya wanga kama vile ugali, wali, ndizi, viazi, magimbi, n.k

Kama shughuli Yani kazi yako ni ya kukaa kwenye computer asubuhi kunywa kikombe cha maziwa tu bila kitafunio chochote

Mchana samaki na salad au mbona za majani.

Jioni unaweza usile kabisa ukalala hivyo hivyo ukiweza kufanya hivyo wiki utaona matokeo yake.

Nimejifunza kuwa saingine kusikia njaa ni vile utavyoweza kuwaza akilini mwako.

Acha kabisa kunywa chai na vitafunwa


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuumwa ni kubaya sana na tafiti za kisayansi zinathibitisha kuwa magonjwa mengi yasiyoambikiza yanaweza kuepukika kama mtu ataishi kwa kuzingatia kanuni na afya ya lishe n.k


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom