Aliyefanikiwa kuondoa kitambi naomba anishauri

Aliyefanikiwa kuondoa kitambi naomba anishauri

Halafu kwa mwanaume ili usisikie njaa mara kwa mara hususa mwanzoni pendelea sana kila mlo kula na mboga za majani au salad.

Sababu zina fibers kambakamba ambazo huyeka na kuachiliwa kidogo kidogo huko tumboni na kufanya kongosho kuto kuelemewa ktk kutema insulin n.k

Ukila mboga ya majani au saladi ya kutosha hutasikia njaa haraka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekimbia, nimeruka nk lakini nimeshindwa kabisa kukiondoa. Naomba wale ambao mlikuwa na kitambi mtoe maelezo hapa nini mulifanya ili kukiondoa?
anza kukimbia kila siku kilometa kadhaa na kupiga mazoezi ya kukata tumbo hutomaliza miezi mitatu kitambi kinakata chote
 
Kinachosababisha vitambi kwa watu wengi ni Pombe...Bia na Pombe kali ndo chanzo cha vitambi. Acha kunywa bia,.kula utakavyo..hutaona kitambi ng'oo
 
Mfollow Dr Boaz mkumbo md Facebook. anatoa ushauri mzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
Dr Boaz ni Sawa na Dr Ndodi tu ni Mpiga Dili kwa Kuuza Bidhaa zake hana kingine zaidi ya kuwaibia wajinga,hakuna ushauri anaoutoa, watu wanadanganyika na mwili wake kwamba anakula kwa formula kumbe mwili wake ni kama wa Nyerere au Warioba,Kuna watu ni Wembamba by Nature hata awe anakula hovyo hovyo,metabolic zao ni kubwa,kuna wengine watu wa kuridhika hata akiwa anakunywa maji 24/7 mwili uonaongezeka.

Dr Boaz ana mwili mwembamba by Nature na sio kwamba sayansi ya mapishi inamsaidia na ndio maana kutwa anashinda Gym aongeze mwili lakini wapi mwili hauji.

Kuna mtu Mwingine yupo Ujenzi ZOne Benny Innocent naye ni Mpigaji sana anawapiga Wajinga wasiojua baada ya Kumstukia Bei zake sasa amekuja na dhana ya jinunulie vifaa sie tutakujengea ukinunua vifaa hiyo bei ya ufundi ni balaa.

Hawa jamaa wa Online wengi ni WATAFUTA FURSA TU.
 
Inawezekana kupungua sana kama utadhamiria .

Kwa kuanzia acha kabisa kula vyakula vya wanga kama vile ugali, wali, ndizi, viazi, magimbi, n.k

Kama shughuli Yani kazi yako ni ya kukaa kwenye computer asubuhi kunywa kikombe cha maziwa tu bila kitafunio chochote

Mchana samaki na salad au mbona za majani.

Jioni unaweza usile kabisa ukalala hivyo hivyo ukiweza kufanya hivyo wiki utaona matokeo yake.

Nimejifunza kuwa saingine kusikia njaa ni vile utavyoweza kuwaza akilini mwako.

Acha kabisa kunywa chai na vitafunwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa napingana na nyinyi mnaopinga "kunywa chai" Kwa maana ya kupata breakfast!! Sijui ni akili ya wapi hii!!!

Kwa taarifa yako, breakfast huupa mwili na ubongo nguvu ya kufanya kazi siku nzima! Unapounyima chakula cha asubuhi unaudumaza. Utajiona umepungua kilo au umekonda, kukonda huko siyo Kwa afya bali ni utapiamlo!!!

Kula vizuri asubuhi (breakfast) na mchana (lunch), usiku unaweza kupotezea maana chakula hakina matumizi tena usiku!

Nikisema breakfast simaanishi "chai" kwa maana ya maji yenye sukari na majani, bali namaanisha chakula cha asubuhi kilichopangaliwa vyema (balanced diet).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dr Boaz ni Sawa na Dr Ndodi tu ni Mpiga Dili kwa Kuuza Bidhaa zake hana kingine zaidi ya kuwaibia wajinga,hakuna ushauri anaoutoa, watu wanadanganyika na mwili wake kwamba anakula kwa formula kumbe mwili wake ni kama wa Nyerere au Warioba,Kuna watu ni Wembamba by Nature hata awe anakula hovyo hovyo,metabolic zao ni kubwa,kuna wengine watu wa kuridhika hata akiwa anakunywa maji 24/7 mwili uonaongezeka.

Dr Boaz ana mwili mwembamba by Nature na sio kwamba sayansi ya mapishi inamsaidia na ndio maana kutwa anashinda Gym aongeze mwili lakini wapi mwili hauji.

Kuna mtu Mwingine yupo Ujenzi ZOne Benny Innocent naye ni Mpigaji sana anawapiga Wajinga wasiojua baada ya Kumstukia Bei zake sasa amekuja na dhana ya jinunulie vifaa sie tutakujengea ukinunua vifaa hiyo bei ya ufundi ni balaa.

Hawa jamaa wa Online wengi ni WATAFUTA FURSA TU.
Fact

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa napingana na nyinyi mnaopinga "kunywa chai" Kwa maana ya kupata breakfast!! Sijui ni akili ya wapi hii!!!

Kwa taarifa yako, breakfast huupa mwili na ubongo nguvu ya kufanya kazi siku nzima! Unapounyima chakula cha asubuhi unaudumaza. Utajiona umepungua kilo au umekonda, kukonda huko siyo Kwa afya bali ni utapiamlo!!!

Kula vizuri asubuhi (breakfast) na mchana (lunch), usiku unaweza kupotezea maana chakula hakina matumizi tena usiku!

Nikisema breakfast simaanishi "chai" kwa maana ya maji yenye sukari na majani, bali namaanisha chakula cha asubuhi kilichopangaliwa vyema (balanced diet).

Sent using Jamii Forums mobile app

Hiyo unayosema inawezakufanyika kwa mtu ambaye tayari yuko kwenye uzito stahiki kwa kuzingatia BMI yake.

Mleta mada akifanya hayo ulosema atachelewa sana kupungua uzito kama siyo kushikana kabisa kupungua au kuzidi kuongezeka uzito.

Kwa mtu mwenye uzito stahiki ambaye yuko kuhakikisha ana mentain asizidi BMI hayo usemayo yaweza kuwa sawa lakini siyo kwa mtu ambaye tayari anatatizo la uzito ulozidi kama mleta mada.

Kwa mtu ambaye hana tatizo la uzito ulozidi yana overweight/ obesity akifanya hayo ulosema ni sawa .

Lakini kumbuka mleta mada tayari ana tatizo la overweight/obesity na kwa hiyo kinachotakiwa kufanyika kwa haraka kwake ni mkakati wa kuondoa huo uzito ulozidi kisha akishafikisha kilo zinazotakiwa kwa mujibu wa BMI hapo akifanya hicho ulivyosema itakuwa ni sawa kabisa though kuna changamoto zake pia!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sishangai endapo urudipo ama uwapo mahali baada ya shughuli unaagiza nyama na bia

*** Acha kutumia vyakula/vimiminika vyenye sukari
** Kula mboga mboga na matunda, saizi ya chakula iwe ukubwa wa ngumi yako
** Kunywa maji ya wastani na endelea na mazoezi
Exactly.
Mm nilikuwa muhanga nimefuata yote kama ulivyoeleza nimepungua kutoka kilo 88 mpaka 77 sasa.nilikuwa siwezi hata kukimbia kwa Jinsi pumzi zilikuwa zinabana lkn kwasasa ni mwepesi.vyote hivi ndani ya mwaka mmoja.

Dawa ni kuacha vimiminika vya Sukari,wanga kidogo,mboga Za Majani na matunda kwa sana utaushinda umeme.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom