Tusaidie kaka
Sent using
Jamii Forums mobile app
Ipo hivi kiongozi
1. Kujitoa
2. Weka malengo
3. Tengeneza ratiba ya msosi pamoja na mazoezi.
Kwa upande wangu mimi nilifanya na ninaendelea kufanya hivi:-
1. Nina amka saa kumi na moja na nusu, najianda kwa mazoezi. Saa kumi na mbili kasorobo naanza kukimbia kwa dakika 50 mpaka 1hr.
Ila nilivyoanza nilikua nakimbia 25 min ila nikawa naongeza mdogo mdogo.
2. Nikishatoka kukimbia na chemsha maji ya moto yenye limao kama lita moja na nusu. Nakunywa mdogo mdogo mpaka kwenye mida ya saa sita yanakuwa yameisha.
3. Baada ya hapo nina hakikisha lunch napata kwenye mida ya saa sita na nusu au saa saba. Lunch ipo hivi:- vyakula vyenye carbohydrate kwa mfano wali, ugali n.k naweka kidogo sana tena sana ila na hakikisha nakula mboga za majani, protein na matunda kwa wingi. Dinner hivyo hivyo ila napunguza zaidi.
4. Maji kwa siku nakunywa lita 3+
Vitu ambavyo nimeviondoa kwenye ratiba yangu ni:-
1. Chai
2. Soda
3. Bia nimeondoa ila mara moja moja huwa nashtua kiu ikinibana sana.
4. Juisi za viwandani.
Matokeo.
Nimeweza kupunguza 15kg ndani miezi miwili na wiki tatu.
Angalizo.
Kama una vidonda vya tumbo hii ni hatari kwa afya yako.
Usitegeme matokeo ya haraka haraka, uvumilivu unahitajika.
Kila la kheri.
Sent using
Jamii Forums mobile app