Bernard James
Jaji Kiongozi Fakihi Jundu jana aliliambia Mananchi Jumapili mahakama iliamuru kuchiliwa kwa mzee Sururu baada ya kuridhika hapakuwa na sababu za kutosha kisheria kutoa hukumu hiyo.
Muda mfupi baada ya kusomwa hukumu hiyo maofisa wangu walinipa taarifa na kuchukua hatua ya kuitisha faili la kesi. Jana majira ya saa kumi jioni ofisa wa mahakama alikuwepo gerezani kuhakikisha Bwana Sururu anaachiwa huru na kuungana na familia yake, alisema jaji kiongozi.
Aliongeza: Wakati Bakwata (Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania) wanahoji uhalali wa hukumu hiyo tayari tulikwishachukua hatuai. Hatukusubiri kusukumwa na mtu yeyote. Sisi tulihisi tatizo katika hukumu hiyo na kuchukua hatua mara moja.
Chanzo: Wavuti ya Mwananchi